Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh. Abbas Kandoro akizindua kampeni ya kupanda miti katika eneo la Uwanja mpya wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe jijini Mbeya mwishoni mwa wiki. TBL ilitoa miche 4000 na kuipanda kwenye eneo hilo ikiwa ni mikakati yake ya kuboresha mazingira.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi akimwelekeza mtoto jinsi ya kupanda miti eneo la Uwanja mpya wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe jijini Mbeya mwishoni mwa wiki. TBL ilitoa miche 4000 na kuipanda kwenye eneo hilo ikiwa ni mikakati yake ya kuboresha mazingira.
Wafanyakazi wa Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) Mkoa wa Mbeya, wakiwa na miche ya miti kwa ajili ya kwenda kuipanda katika eneo la wazi katika Uwanja mpya wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe jijini Mbeya mwishoni mwa wiki. TBL ilitoa miche 4000 na kuipanda kwenye eneo hilo ikiwa ni mikakati yake ya kuboresha mazingira.
Mkazi wa Kijiji cha Ikumbi kilichopo jirani na Uwanja mpya wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, Mbeya, akipanda moja kati ya miche 4000 iliyotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupanda katika eneo la uwanja huo mwishoni mwa wiki.
Wakazi wa Kijiji cha Ikumbi kinachouzunguka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, wakipanda miti katika eneo la uwanja huo,mwishoni mwa wiki. Miche hiyo imetolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ikiwa ni kampeni ya kutunza mazingira.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Jamani huo uwanja mpya wa Songwe utaanza lini? Tuliambiwa ungeanza mwezi wa kumi na mbili mwaka huu unaoishia sasa au ilikuwa kumi na mbili ipi, ya mwakani?

    ReplyDelete
  2. Asante sana Mkuu wa Mkoa, Mhe.Abbas Kandoro kwa kutuonyesha mfano mzuri wa kuigwa wakati wa kupanda miti.

    Viongozi wengi wameonyesha mfano wa kupanda miti kwa kupiga makoti au kuchuchumaa kwenye mikeka, khanga au nguo yoyote ile.

    Baada ya hapo wananchi wengi wameshindwa kupanda miti kama walivyoonyeshwa kwa sababu hawana mikeka na khanga za kuweka chini wakati wa kupanda miti.

    Mfano wa Mkuu wa Mkoa ni rahisi kiasi cha watoto, kina Mama, vijana na watu wengine kuweza kupanda miti kwa haraka.

    Kwa wale walio karibu na Mkuu wa Mkoa huyu naomba wafikishe salamu za pongezi kwake kwa kurahisisha kazi hii ya upandaji miti. Sasa miti itapandwa.

    MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  3. Ni Juhudi inayofaa kupigiwa MFANO. Kila la heri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...