Mfumuko wa Bei umezidi kuongezeka kama taarifa ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu inavyoonesha kwamba, wakati mfumuko wa bei mwezi Julai mwaka huu (Bajeti ya mwaka wa Fedha 2011/2012 ilipokuwa inaanza) ulikuwa asilimia 13, umefikia asilimia 19.2 mwezi Novemba. 

Hii maana yake ni kwamba, Bajeti ya Serikali iliyopitishwa na Bunge mwezi Juni 2011, imepunguza uwezo wa kununua bidhaa na huduma kwa takribani asilimia 6. 

Hii ni sawa na shilingi 780 bilioni kuyeyuka katika Bajeti katika kipindi cha miezi Minne tu ya utekelezaji wa wake. Kutokana na kasi ya ukuaji wa Mfumuko wa Bei ni dhahiri kwamba, itakapofika mwisho wa mwaka wa Bajeti Serikali itakuwa imepoteza kwa kiasi kikubwa uwezo wa kununua bidhaa na huduma kwa zaidi ya robo ya Bajeti yake.

Hali ni mbaya zaidi kwa wananchi kwani Mfumuko wa Bei za vyakula umekua kwa kasi kikubwa mno. Ofisi ya Takwimu imeonesha kuwa wakati mfumuko wa Bei za vyakula ulikuwa asilimia 14.8 mwezi Julai, umefikia asilimia 24.7 mwezi Novemba 2011. 

Ukilinganisha na bei za vyakula mwaka 2010, mwananchi amepoteza uwezo wa kununua chakula kwa zaidi ya robo katika ya Novemba 2010 na Novemba 2011. Jumla ya vyakula ambavyo mwananchi alinunua kwa shilingi 10,000 mwaka 2010, sasa atanunua kiwango kile kile kwa shilingi 12,500. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Asante kwa kutuelimisha Mh. Zitto. Hii ni kero kubwa sana. Ila huu mfumuko wa bei unatokana na nini? Na kama ni kushuka kwa thamani ya shilingi, nako kunatokana na nini? Ni sababu ambazo zipo ndani ya uwezo wetu?

    ReplyDelete
  2. Haiwezekani kuchota maji kwa pakacha!

    Mfumuko wa bei kwa nchi zetu hizi unachangiwa zaidi na Wahujumu ktk sekta ya fedha kwa kuendesha udhalimu na ufisadi kwa vile Bank zinaendesha shughuli zao kwa maslahi ya wachache walio na mtandao.

    Hivyo Benki kuu itagharimu muda na jitihada ktk kuweka sawa mfumuko wa bei urudi ktk hali ya kawaida!

    ReplyDelete
  3. Hii inatokana uongozi unaopenda kujizolea misifa kibao kwa mambo ya watu, siku ya uhuru tumetumia mihela kibao, na kuimbiwa kuwa umeweza, ulichokiweza hakijulikani. Sherehe ya kifahari utafikiri kuapishwa kwa obama. Leo unashindwa kurekebisha uchumi. Mzee mkapa ameacha nchi ikiwa inmwelekeo lkn leo kama ndio siku ya kupata uhuru, maisha ya ujima, hali ngumu kwa watanzania wengi, wenye madaraka kwao mungu amewajalia. Sukari bei juu, vyakula juu. Kweli upinzani umetufunhua macho na akili

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...