Mwanasheria wa wakazi wa zilizokua kota za bandari Gerezani , Dkt. Sengondo Mvungi (kushoto) akizungumza na wateja wake. Dar es salaam leo kuhusu maendeleo ya kesi yao iliyo mahakama kuu ya Tanzania.
Baadhi ya wakazi wa zilizokua kota za bandari Gerezani wakimsikiliza mwanasheria wao Dkt. Sengondo Mvungi kuhusu maendeleo ya kesi yao iliyo mahakama kuu ya Tanzania.
Na Mwandishi Wetu
WAKAZI wa Kota za Bandari kata ya Gerezani Kariakoo wameitaka serikali kutowahamisha wala kuwavunjia nyumba zao hadi hapo kesi yao iliyopo mahakama kuu kitengo cha Ardhi itakapo kamilika.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa mtaa huo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuwa nyumba hizo walinunua kutoka serikalini na kupewa mkataba.
Alisema eneo hilo linataka kuchukuliwa na serikali ili kujenga kituo cha mabasi yaendayo kasi bila ya kujali kuwa nyumba hizo waliuziwa ambapo serikali iliingia mkataba na mtu mmoja mmoja.
"Tumesikia fununu kuwa serikali inataka kuja kuvunja nyumba zetu kinguvu ikiwa kesi bado ipo mahakamani",alisema
Kwa upande wake katibu mwenezi wa siasa wa chama cha Mapinduzi Bw.Akida Hafidhi alisema serikali ilifanya makosa kuingia katika eneo hilo ikiwa inajua kabisa kuna mgogoro na kuongeza kuwa wanaomba haki iweze kutendeka kwa kuiachia mahakama kutoa maamuzi kama katiba inavyoelekeza.
Alisema serikali inatakiwa kutambua kuwa wakazi wa eneo hilo wanamiliki nyumba hizo kimkataba na hakuna mtu aliyevunja mkataba huo ambapo walinunua kutoka kwao.
Hata hivyo walisema watashangazwa endapo watasikia kuwa kuna mtu anaingilia uhuru wa mahakama ikiwa ibara ya 4(1) na 107(a) ya katiba ya Tanzania inaeleza wazi kuwa chombo cha mwisho chenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki ni mahakama ya Tanzania.
"Tumesema hivyo kwa sababu tulisikia baadhi ya watendaji serikalini walisema tulienda mahakamani kimakosa huku wakijua dhahili kuwa ni mahala ambapo haki inapatika",walisema
Walisema wanamuomba Rais Jakaya Kiwete asije akadanganywa kwa hilo kuwa kuna makubaliano yaliofanyika huku wakisisitiza kuwa kesi iliyopo ni kuvunjwa kwa mkataba na sio madai ya fidia kama ambavyo baadhi wa watendaji walivyopeleka taarifa serikalini.
maajabu mafuriko picha zote ni wazalendo tu,huko mabondeni hakuna waarabu wala wahindi.hii ndiyo hali halisi ya bongo wahindi waarabu kishi mijini na upendeleo wa viwanja,lini wananchi watafaidi nchi yao?
ReplyDeleteKwakuwa wewe tayari ni masikini wa kufikiri na masikini wa mali basi itakuwa ngumu sana kuelewa.Nani kakwambia kama hakuna warabu walioathirika.Na hizo nyumba za mijini kwani zilijengwa na nani?Au hujui kama Nyerere aliwanyan'ganya wahindi nyumba na kuzisajili kama za serikali?Kwahiyo ulitaka wahamishwe kwasababu ya rangi zao?Mbona waarabu wanaishi mitaani na wengine vizuri tu na wamejichanganya na watoto wao wanasoma shule za walal hoi?Nani kakwambia nyumba za mjini ni za waarabu na wahindi tu?Kwani hujui kama wanaoishi wengine ni wapangaji tu?Wewe ni pesa yako tu na kama huja aaliwa kuwa napesa ya kuishi kariakoo na sehemu nyingine basi kaa kimya.Hao walizozinunua hizo nyumba unazozisema kwani wameuziwa na nani kama sio wazalendo.Kwani kunasheria zinasema kununua nyumba mwarabu au muhindi ni kosa?Kwani wazalendo wangapi wamenunua nyumba hizo sehemu unazosema na wamezikodisha.Kwanza wewe ni wa kutoka mkoa gani kwasababu ndio nyie mliokuja Dar na kujazana mpaka wazaramo wote sasa hawana pakukaa.Tumia akili na uache ubaguzi.
ReplyDeleteSasa nyinyi mukiambiwa muondoke mabondeni bado munakaidi, jee hilo ni kosa la wahindi na waarabu?
ReplyDeleteSasa mbona hujawataja Wazungu waliotunyan'ganya KIGAMBONI yetu au ndio mnawatukuza kwa kuwaletea dini?
ReplyDeletekaka acha hasira utanzania utakuwa nao ww? ukweli ni kwamba serikali inawalea wengetolewa tu kwa nguvu maendeleo hayaendi kwa kubembelezana inchi hiyo inatakiwa kuwa na uongozi kama wa puti russia ukweli ndio rais anatakiwa awe bakieni na demokrasia yenu ya uongo
ReplyDeleteSi kweli hAwa watu waishi bondeni Na wahindi na waarabu siyo hoja You moron !
ReplyDeleteHao Wahindi na waarabu ni watanzania na niwazalendo kama wewe. Kwanini uwabague kwa jinsia zao, wache na wao wafaidi kama wakina ngurume
ReplyDeleteNani alikuambia kuwa mahakama za Tanzania zinatoa haki?Sera za serikali za kujali kuchaguliwa badala ya kuangalia nini kitatokea baadae kwa wananchi ndio matokeo yake,lack of planning and corruption.Swala sio muhindi au muarabu ni kwamba viongozi wetu wako short sighted wanachojali ni kuiba tu.
ReplyDeleteMdau wa 2 hapo juu NYERERE ALINYA'NGĂNYA NYUMBA ,WAHINDI NA WAARABU KWA VILE WALIZIJENGA NYUMBA HIZO KWA KUIBA RASILIMALI ZA NCHI!
ReplyDeleteLakini maneno yako ni KWELI KABISA KUWA WAZALENDO NDIO WALIOUZA NYUMBA KWA WAHINDI NA WAARABU KWA TAMAA ZAO NA NJAA YAO!
Ndio maana hata hizo KOTA ZA BANDARI ANAZOPIGANIA WAKILI SENGONDO MVUNGI UKIANGALIA NYINGI WANAOKAA SASA WAMENUNUA NA HAWAKUWA WATUMISHI WA BANDARI KABLA!
SASA HIZI NJAA,TAMAA NA KUKOSA DIRA YA MAISHA NI TATIZO LETU BINAFSI SISI WAZALENDO!
KATI YENU HAKUNA HATA MMOJA ALIYESEMA LA MAANA. SIONI HOJA YOYOTE, BALI NI VIOJA TU KATIKA MALUMBANO YENU. SIONI MAUNGANIKO (LINK) YA PICHA HIZI NA UHINDI, UARABU, UZUNGU, UAFRIKA, WALA DINI KAMA TAAHIRA MMOJA (Dec 26 08:27:00 PM 2011) ALIVYOSEMA HAPO JUU. MKIKOSA YA KUANDIKA NI BORA KUSOMA YA WENZENU WENYE MANENO YA KUANDIKA YA KUELIMISHA. HAYA MENGINE NI UCHOCHEZI TU.
ReplyDeleteUkitaka kujua tofauti yako wewe na muhindi nenda india...alfu rudi ndo hao watu wajuwe
ReplyDeletebinadam wote sio sawa...But point sio kukataa kuhama,je una waamishia wapi?...na swala sio kuishi mabondeni tu,miundo mbinu ipo?Inatokea katrina watu wamekufa na maji yame jaa walikuwa wanakaa mabondeni...by the way its 13013.....Nobody is perfect
Mdau wa pili umenikuna kweli kweli! na wewe unaesema kuwa walinyang'anywa kwakuwa waliiba rasilimali za tanzania ni muongo! na juzi nimesikia maaskofu wanatamani azimio la arusha lirudi sijaelewa ndio wanaona waarabu au waislamu wameanza kujenga wanataka wanyang'anywe tena mali zao! loooh!
ReplyDeleteKuwatukana wahindi so wizuri jamani Wao pia no watanZania wakati wa mafuriko walisaidia waafrica wenzetu Shia ithnashri na ,singa singa Walitoa Masada wa chakula na waliokoa watu wengi! Pia wali gawa chakula kwa siku 5 je wenzetu walikua na moyo? Tafadjhali tujenge nchi bila chuki.
ReplyDelete