Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania,Bw. Albert Makoye ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa pingili za chini za uti wa mgongo kutokana na kutenguka alipokuwa akifanya mazoezi yake ya kawaida ya kila siku,akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Hoteli ya Giraffe Ocean View,Dkt. Charles Bekoni (kulia) wakati alipofika nyumbani kwake leo kumjulia hali.Bw. Makoye ambaye pia ni Mdau Mkuu wa Globu ya Jamii anataraji kwenda nchini India kwa Matibabu zaidi ya Maradhi hayo hivi karibuni.Globu ya Jamii inampa pole sana Mdau Albert Makoye kwa maradhi hayo yanayomsumbua na inamuombea aweze kupona haraka na kuendelea na majukumu yake kama hapo awali.
Home
Unlabelled
Hali si Shwari kwa Mdau Albert Makoye,anataraji kwenda india kwa matibabu zaidi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
That smells a bit fishy 'ametenguka akiwa akifanya mazoezi na rafiki yake' si mseme tu hadha baskula fi laisa kengele
ReplyDeletepole Albert tunakuombea Mungu akuponye
ReplyDeleteINSHAALLA M/MUNGU ATAMUAFU KAKA YETU MAKOYE APONE
ReplyDeletePole Mdau ndugu Albert Makoye.
ReplyDeletemuda umefika sasa matunda ndo hayo!!!
ReplyDeletepole albert bado uko vile vile kama nilivyokuacha nilivyoona tu picha yako nikajua nakujua kiasi fulani nakumbuka sana mapati uliyokuwa unayafanya mikocheni pale nyumbani kwako mwenyezi mungu awe nawe
ReplyDeletePole sana. Mungu akutangulie.
ReplyDeleteNaona Charles Bekon umepiga magwanda
ReplyDeletePole sana Makoye nakuombea upone haraka. Nakukumbuka tangu tuko wote Cordial Dar
ReplyDeleteCharlz Bekon,,,MAGWANDAZZZZZZZ!
ReplyDeleteIsipokuwa hizo luksi za mabegani zinatumika pale ''Mgambo'' anapochomeka Kofia yake baada ya kuikunja kama chapati, ili afanye masuala mengine kama kula n.k!
Na pia kifuani juu ya mfuko wa shati la gwandazzz upande wa kushoto Filimbi na kamba iliyosokotwa visikosekane!
Ni haki ya Kikatiba sio zambi Uhuru wa Kiitikadi!
Kwa hiyo yale mambo tena ndo basi tena. Maana kwa ugonjwa huu!
ReplyDeleteHahahaha Mdau shati la gwanda alilovaa Dr. Chalz Bekoni, kwa mashati ya mikono mirefu kama Bekoni hapo pana ile staili ya kukunja mikono huku na huku kwa kuviringisha kama wanavyofanya Mgambo wa Manispaa, ile babake ukitokeza kama pana Chinga lazima atastuka kidogo!
ReplyDeleteMagwandazzzz, jamani hii kasi na mwamko wa itikadi hiyo tafadhali na tuendelee kubadilishana mawazo, maoni na malumbano ya mezani na majukwaani na ktk social media kama hapa, ila tu wenzetu msije mkachukulia serious mkaingia Msituni!
ReplyDeletepole sana mdau lakini msiwachezee wapemba jamani watawaumiza lol
ReplyDeleteWAOSHA VINYWA.... MTU NI MGONJWA HALAFU WENGINE MNASEMA VYA AJABU, KUANZIA NGUO MPAKA VISIVYOELEWEKA! ADABU NA UBINADAMU MMEUWEKA WAPI????
ReplyDeleteMdau wa Sun Jan 08:44:00 PM 2012
ReplyDeleteAlbert Makoye ndugu yetu anapewa pole kwa kuumwa,,,nguo zinazojadiliwa ni za Dr.Chalz Bekoni Magwandazzz!