Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania,Bw. Albert Makoye ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa pingili za chini za uti wa mgongo kutokana na kutenguka alipokuwa akifanya mazoezi yake ya kawaida ya kila siku,akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Hoteli ya Giraffe Ocean View,Dkt. Charles Bekoni (kulia) wakati alipofika nyumbani kwake leo kumjulia hali.Bw. Makoye ambaye pia ni Mdau Mkuu wa Globu ya Jamii anataraji kwenda nchini India kwa Matibabu zaidi ya Maradhi hayo hivi karibuni.Globu ya Jamii inampa pole sana Mdau Albert Makoye kwa maradhi hayo yanayomsumbua na inamuombea aweze kupona haraka na kuendelea na majukumu yake kama hapo awali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. That smells a bit fishy 'ametenguka akiwa akifanya mazoezi na rafiki yake' si mseme tu hadha baskula fi laisa kengele

    ReplyDelete
  2. pole Albert tunakuombea Mungu akuponye

    ReplyDelete
  3. INSHAALLA M/MUNGU ATAMUAFU KAKA YETU MAKOYE APONE

    ReplyDelete
  4. Pole Mdau ndugu Albert Makoye.

    ReplyDelete
  5. muda umefika sasa matunda ndo hayo!!!

    ReplyDelete
  6. pole albert bado uko vile vile kama nilivyokuacha nilivyoona tu picha yako nikajua nakujua kiasi fulani nakumbuka sana mapati uliyokuwa unayafanya mikocheni pale nyumbani kwako mwenyezi mungu awe nawe

    ReplyDelete
  7. Pole sana. Mungu akutangulie.

    ReplyDelete
  8. Naona Charles Bekon umepiga magwanda

    ReplyDelete
  9. Pole sana Makoye nakuombea upone haraka. Nakukumbuka tangu tuko wote Cordial Dar

    ReplyDelete
  10. Charlz Bekon,,,MAGWANDAZZZZZZZ!

    Isipokuwa hizo luksi za mabegani zinatumika pale ''Mgambo'' anapochomeka Kofia yake baada ya kuikunja kama chapati, ili afanye masuala mengine kama kula n.k!

    Na pia kifuani juu ya mfuko wa shati la gwandazzz upande wa kushoto Filimbi na kamba iliyosokotwa visikosekane!

    Ni haki ya Kikatiba sio zambi Uhuru wa Kiitikadi!

    ReplyDelete
  11. Kwa hiyo yale mambo tena ndo basi tena. Maana kwa ugonjwa huu!

    ReplyDelete
  12. Hahahaha Mdau shati la gwanda alilovaa Dr. Chalz Bekoni, kwa mashati ya mikono mirefu kama Bekoni hapo pana ile staili ya kukunja mikono huku na huku kwa kuviringisha kama wanavyofanya Mgambo wa Manispaa, ile babake ukitokeza kama pana Chinga lazima atastuka kidogo!

    ReplyDelete
  13. Magwandazzzz, jamani hii kasi na mwamko wa itikadi hiyo tafadhali na tuendelee kubadilishana mawazo, maoni na malumbano ya mezani na majukwaani na ktk social media kama hapa, ila tu wenzetu msije mkachukulia serious mkaingia Msituni!

    ReplyDelete
  14. pole sana mdau lakini msiwachezee wapemba jamani watawaumiza lol

    ReplyDelete
  15. WAOSHA VINYWA.... MTU NI MGONJWA HALAFU WENGINE MNASEMA VYA AJABU, KUANZIA NGUO MPAKA VISIVYOELEWEKA! ADABU NA UBINADAMU MMEUWEKA WAPI????

    ReplyDelete
  16. Mdau wa Sun Jan 08:44:00 PM 2012

    Albert Makoye ndugu yetu anapewa pole kwa kuumwa,,,nguo zinazojadiliwa ni za Dr.Chalz Bekoni Magwandazzz!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...