Waziri wa Ujenzi Dakt. John Pombe Magufuli (katikati) akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Jan, 1,2012 kuhusu ongezeko la viwango vya nauli katika vivuko vyote vya serikali nchini, ambapo kuanzia Jan, 1 ,2012, Wizara yake kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) imeongeza viwango vya nauli kutokana na maeneo mbalimbali ya vivuko, , amezitaja nauli hizo kwa mfano MV. Magogoni na Mv. Kigamboni kwa Mkoa wa DSM ni kati ya shilingi 200 kwa watu wazima , watoto chini ya miaka 14, shilingi 50, na wanafunzi waliovaa sare za shule na vitambul;isho ni bure, Pia akatoa mfano wa Kivuko cha MV. Chato kitatoza nauli ya watu wazima shilingi 3,000/, watoto chini ya miaka 14 ni elf 50 ,na wanafunzi wenye sare za shule ni bure. Bei hizi zimepanda kutokana na gharama kupanda za uendesaji. (kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya TEMESA Prof, Idrissa Mshoro. (kushoto) ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Herbert Mrango.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Herbert Mrango (kushoto) akimkaribisha Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (katikati) alipokutana na waandishi wa habari hawapo pichani jijini leo na kutoa taarifa kuhusu ongezeko la viwango mbalimbali vya nauli katika vivuko nchini , (kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya TEMESA Prof, Idrissa Mshoro, (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Huyu ndiye anayestahili kuwa rais mpya wa TZ, maana hana mchezo.

    ReplyDelete
  2. habari za kazi!
    naomba upitie vizuri hivyo viwango vya nauli kuna sehemu inasema elf hamsini kwa watoto wenye umri chini 14.
    kazi njema!

    ReplyDelete
  3. Tafadhali rekebisha usafiri badala ya kupandisha nauli. Masaa mawili kwenye foleni. Je ukiwa na mgonjwa unamkimbiza hospitali si atakufia njiani? Mama akiwa kwenye uchungu si atazalia njiani? Mahali pa dakika 10 inachukua masaa 2 hamu sina. Viongozi wakipita traffic inazuia magari na viongozi wanapepea tu barabarani kwahiyo hawana uchungu maana hawaelewi taabu za wanachi. Tafadhali sikieni kilio chetu mfanye kitu. Kama mmeshindwa leteni ma expert wawasaidie kuwe na efficiency barabarani. Bara bara hiyo hiyo watu,pikipiki,daladala, bajaji tutafika kweli? Basi tuvae gamba la kobe tuende polepole tufike kesho.

    ReplyDelete
  4. Mngeboresha uvukaji wa magari kuwa wa haraka zaidi ingependeza, maana masaa mawili unasubiri kuvuka! Bakhresa lete kivuko chako utusaidie!serikali imeshindwa, kuvuka kwa guta guta ni ghali kuliko gari DUh!

    ReplyDelete
  5. Yaani mambo yanayofanyika kwenye vivuko vya Kigamboni na Magogoni ni ushenzi mtupu. Kuna watu wanajifanya serikari zaidi wenyewe wanatumia barabara yao na hawalipi hata shilingi9. Sisi makabwela ndo tunafia kwenye folen. Mimi nionavyo hakuna haja ya kuangeza nauli. Kinachotakiwa ni usimamizi mzuri sababu kila mtu gari akilipa shs elfu moja inatosha kuendesha vivuko. Sasa kinachofanyika sijui polisi ana gari halipi, mwanajeshi anagari binafsi halipi, askari magereza na gari yake binafsi halipi, STK, SU, DFP na wengine wengi hawalipi kwa mtindo huo huo. Utaratibu mzuri wa kusimamia mapato ya vivuko hela nyingi zitapatika, sababu kinachofanyika sasa hivi ni wezi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...