Bibi Harusi akipita juu ya migongo ya wakwe zake wakati wa kuingia ukumbini ikiwa ni ishara ya kukaribishwa katika familia, kabila la Wayao .
Bw. Harusi akipita juu ya migongo ya wazazi wake wakati wa kuingia ukumbini wakati wa harusi yake iliyofanyika katika ukumbi wa Mbezi Luxiry jijini ,Dar es Salaam.utamaduni huu hufanywa na watu wa lindi kabaila la wayao.
Makaka wa bwana harusi wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa sherehe ya harusi ya mdogo wao .Wakiwa na nyuso za furaha bwana harusi Samwel Daniel na mkewe Kaindi Taratibu wakiwa kwenye pozi la picha baada ya kufunga ndoa yao katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kibaha hivi karibuni na kufuiatiwa na sherehe kubwa iliyofanyika katika ukumbio wa Mbezi Luxiry jijini Dar es Salaam.
Bw.harusi Samwel akiwa na mkewe Kaindi wakishuka kutoka katika mlima kilimanjaro uliopo eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam, walipokwenda kufanya utalii wa ndani.Baada ya kufunga ndoa yao kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Januari 28.
Si kweli kwamba kijana anakanyaga migongo, ila anakanyaga viuno. Na anaowakanyaga sio wazazi bali ni dada zake. Hii naona haijakaa ki-maadili ya kiafrika. Na kwanini akanyage kwenye mabonde na sio hiyo milima?
ReplyDeleteKula muhindi wako 'Taratibu" kaka husiogope wala husisikie maneno ya watu kwani ukubwa wa pua sio wingi wa makamasi...!!!!!!!
ReplyDeleteHapo bwana harusi akiangukia magoti itakuwaje?
ReplyDeleteTamaduni zingine hatari!
ReplyDeleteHizo Nalitolela zimetulia kama zinatunga sheria
ReplyDeleteTHIS PIC IS REALLY COOL BROTHER MICHUZI, THE ANGLE was perfect, pia maharusi wako SWAGA, good stuff.
ReplyDeleteMdau UKEREWE
thnks
Mbona Bwana harusi mdogo kuliko Bi harusi. Je atamuweza huyo?
ReplyDeleteDaniel? Daniel sio jina la ukoo wowote wa kiyao, vizuri sana bibi harusi kwa kutumia jina lako halisi la ukoo Kaindi.
ReplyDeleteChe Mpunga
Hongera sana my classmate Kaindi Taratibu..
ReplyDeleteBora hao wanajua kuwakaribisha wakwe zao. Familia nyingine ukiolewa huko, eheee mawifi, mama mkwe wananuna utafukiri wameona kitu gani sijui! Hasa familia ambazo mama mkwe ana mke anaishi uke wenza......wasichana chunga sana hili. Ukiolewa familia yenye uke wenza kaa chonjo. Ukicheza vibaya hata mme hutamfaidi. Tabia kuu ya familia za namna hii, Mama mkwe huwa hapendi wake wa watoto wake ( wakwe). Hupendelea kuwabadirishia wake kila kukicha, na sijui huwa kuna nini...na watoto wao huwasikiliza sana mama zao hata akimwambia leo nenda umpige mkeo, hutii
ReplyDeleteKabila la Wayao linapatikana Masasi mkoani Mtwara na Tunduru mkoani Ruvuma. Lindi haina kabila hilo.
ReplyDeleteAnony unayeuliza kama Bwana Harusi atamuweza Bibi Harusi coz anaonekana ni mkubwa, kwani kakwambia anambeba kichwani!
ReplyDeleteHII IMEKAAA VIBAYA: Mimi ni Myao wa Chikunja Masasi-Mtwara, kidogo nina wasiwasi na taarifa zilizoandikwa hapa, kama bibi harusi Myao au si Myao ndiye anapaswa kupita juu ya migongo ya mawifi zake siku ya harusi ni mama zao hii ni ishara ya kumkaribisha katika ukoo wa Kiyao kimila, pia bwana harusi haruhusiwi kimila kamwe kupita juu ya migongo au kuwakanya mama zake kama ilivyoandikwa hapa, yeye atakwenda kumlaki bibi harusi na kumsaidia pindi aingiapo ukumbini huku akiwakanyaga mawifi migongoni.
ReplyDeleteHabari kaka,nahitaji kufahamu mambo kadhaa kuhusu wayao.naweza kupata mawasiliano yako?
Deletehaya majina ya kizungu bwana mwanaume eti unjiita john james au daudi kenedy au jane jackson hivi hamjui kuwa kuna koo za wazungu za kina George, Geofrey, Daniel na wengine? Acheni utumwa huo wa kijinga tumieni majina yenu ya ukoo kama michuzi, kitenge, mapunda, kingwendu masanja na hata jogoo
ReplyDeletemimi huwa sielewi logic ya kupiga picha kwenye huo mlima kilimanjaro pale mabibo.
ReplyDeleteukipita mandela road siku ya jumamosi ni traffic jam ya ajabu, ukiuliza utaambiwa kwamba maharusi wanapiga picha mlimani.
nahisi watanzania bila kujali usomi na exposure waliyonayo, hufanyiwa decision na wajinga wachache sana. hivi usipopiga picha hapo, harusi itagoma?
Hao ndio wabongo bana!
ReplyDeletewanaopiga picha pale sio wasomi,niwatu waliokalili vitabu na kupasi mitihani, Nchi hii ina wasomi wachache sana , lakini waliokariri vitabu na kupasi ni wengi sana na wao hawafikiri kwa kutumia kichwa
ReplyDeleteAise Bwana Dan na Kahindi karibuni kwenye chama chetu cha ndoano..Hongereni sana.Dan utawaona hao wadada wakishafunga ndoa wanakuwa na jeuri ndani ya nyumba inabidi uvumilie MZEE manake unaweza kujikuta unaoa kila siku,hakuna malaika..Mimi nina mwaka wa kumi sasa tangu nitoke pale St.Joseph.Na wewe Kahindi inabidi umheshimu huyo mume wako..
ReplyDeleteKila la kheri wote
David V
Mmh! hii ndiyo naiona leo: wadau pitieni blogu hii: mwafrika-nywele.blogspot.com.
ReplyDelete