Bibi Harusi akipita juu ya migongo ya wakwe zake wakati wa kuingia ukumbini ikiwa ni ishara ya kukaribishwa katika familia, kabila la Wayao .
 Bw. Harusi akipita juu ya migongo ya wazazi wake wakati wa kuingia ukumbini wakati wa harusi yake iliyofanyika katika ukumbi wa Mbezi Luxiry jijini ,Dar es Salaam.utamaduni huu hufanywa na watu wa lindi kabaila la wayao.
 Makaka wa bwana harusi wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa sherehe ya harusi ya mdogo wao .
Wakiwa na nyuso za furaha bwana harusi Samwel  Daniel  na mkewe Kaindi  Taratibu wakiwa kwenye pozi la  picha baada ya kufunga ndoa yao katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kibaha hivi karibuni na kufuiatiwa na sherehe kubwa iliyofanyika katika ukumbio wa Mbezi   Luxiry jijini Dar es Salaam.
Bw.harusi  Samwel akiwa na mkewe Kaindi wakishuka kutoka katika mlima kilimanjaro  uliopo eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam, walipokwenda kufanya utalii wa ndani.Baada  ya kufunga ndoa yao kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Januari 28.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Si kweli kwamba kijana anakanyaga migongo, ila anakanyaga viuno. Na anaowakanyaga sio wazazi bali ni dada zake. Hii naona haijakaa ki-maadili ya kiafrika. Na kwanini akanyage kwenye mabonde na sio hiyo milima?

    ReplyDelete
  2. Kula muhindi wako 'Taratibu" kaka husiogope wala husisikie maneno ya watu kwani ukubwa wa pua sio wingi wa makamasi...!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. Hapo bwana harusi akiangukia magoti itakuwaje?

    ReplyDelete
  4. Tamaduni zingine hatari!

    ReplyDelete
  5. Hizo Nalitolela zimetulia kama zinatunga sheria

    ReplyDelete
  6. THIS PIC IS REALLY COOL BROTHER MICHUZI, THE ANGLE was perfect, pia maharusi wako SWAGA, good stuff.

    Mdau UKEREWE

    thnks

    ReplyDelete
  7. Mbona Bwana harusi mdogo kuliko Bi harusi. Je atamuweza huyo?

    ReplyDelete
  8. Daniel? Daniel sio jina la ukoo wowote wa kiyao, vizuri sana bibi harusi kwa kutumia jina lako halisi la ukoo Kaindi.
    Che Mpunga

    ReplyDelete
  9. Hongera sana my classmate Kaindi Taratibu..

    ReplyDelete
  10. Bora hao wanajua kuwakaribisha wakwe zao. Familia nyingine ukiolewa huko, eheee mawifi, mama mkwe wananuna utafukiri wameona kitu gani sijui! Hasa familia ambazo mama mkwe ana mke anaishi uke wenza......wasichana chunga sana hili. Ukiolewa familia yenye uke wenza kaa chonjo. Ukicheza vibaya hata mme hutamfaidi. Tabia kuu ya familia za namna hii, Mama mkwe huwa hapendi wake wa watoto wake ( wakwe). Hupendelea kuwabadirishia wake kila kukicha, na sijui huwa kuna nini...na watoto wao huwasikiliza sana mama zao hata akimwambia leo nenda umpige mkeo, hutii

    ReplyDelete
  11. Kabila la Wayao linapatikana Masasi mkoani Mtwara na Tunduru mkoani Ruvuma. Lindi haina kabila hilo.

    ReplyDelete
  12. Anony unayeuliza kama Bwana Harusi atamuweza Bibi Harusi coz anaonekana ni mkubwa, kwani kakwambia anambeba kichwani!

    ReplyDelete
  13. HII IMEKAAA VIBAYA: Mimi ni Myao wa Chikunja Masasi-Mtwara, kidogo nina wasiwasi na taarifa zilizoandikwa hapa, kama bibi harusi Myao au si Myao ndiye anapaswa kupita juu ya migongo ya mawifi zake siku ya harusi ni mama zao hii ni ishara ya kumkaribisha katika ukoo wa Kiyao kimila, pia bwana harusi haruhusiwi kimila kamwe kupita juu ya migongo au kuwakanya mama zake kama ilivyoandikwa hapa, yeye atakwenda kumlaki bibi harusi na kumsaidia pindi aingiapo ukumbini huku akiwakanyaga mawifi migongoni.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Habari kaka,nahitaji kufahamu mambo kadhaa kuhusu wayao.naweza kupata mawasiliano yako?

      Delete
  14. haya majina ya kizungu bwana mwanaume eti unjiita john james au daudi kenedy au jane jackson hivi hamjui kuwa kuna koo za wazungu za kina George, Geofrey, Daniel na wengine? Acheni utumwa huo wa kijinga tumieni majina yenu ya ukoo kama michuzi, kitenge, mapunda, kingwendu masanja na hata jogoo

    ReplyDelete
  15. mimi huwa sielewi logic ya kupiga picha kwenye huo mlima kilimanjaro pale mabibo.

    ukipita mandela road siku ya jumamosi ni traffic jam ya ajabu, ukiuliza utaambiwa kwamba maharusi wanapiga picha mlimani.

    nahisi watanzania bila kujali usomi na exposure waliyonayo, hufanyiwa decision na wajinga wachache sana. hivi usipopiga picha hapo, harusi itagoma?

    ReplyDelete
  16. Hao ndio wabongo bana!

    ReplyDelete
  17. wanaopiga picha pale sio wasomi,niwatu waliokalili vitabu na kupasi mitihani, Nchi hii ina wasomi wachache sana , lakini waliokariri vitabu na kupasi ni wengi sana na wao hawafikiri kwa kutumia kichwa

    ReplyDelete
  18. Aise Bwana Dan na Kahindi karibuni kwenye chama chetu cha ndoano..Hongereni sana.Dan utawaona hao wadada wakishafunga ndoa wanakuwa na jeuri ndani ya nyumba inabidi uvumilie MZEE manake unaweza kujikuta unaoa kila siku,hakuna malaika..Mimi nina mwaka wa kumi sasa tangu nitoke pale St.Joseph.Na wewe Kahindi inabidi umheshimu huyo mume wako..

    Kila la kheri wote

    David V

    ReplyDelete
  19. Mmh! hii ndiyo naiona leo: wadau pitieni blogu hii: mwafrika-nywele.blogspot.com.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...