Rais Jakaya kikwete na Zitto Kabwe katika shughuli ya siku za awali huko Kigoma
1.      Baadhi ya vyombo vya habari vimehusisha kauli yangu ya kutaka kupunguza umri wa kugombea urais na mimi ‘kuutaka urais’. Mimi nikiwa mwanachama na kiongozi wa chama chama changu cha CHADEMA naelewa na kuziheshimu taratibu na kanuni tulizojiwekea za kuomba nafasi mbalimbali za uongozi, ikiwemo nafasi ya urais. Nafasi ya uongozi ndani ya CHADEMA haiombwi kwenye warsha. Iwapo chama change, wakati muafaka ukifika na kutokana na matakwa ya jamii, kikiona nipewe jukumu lolote sitasita kutekeleza wajibu huo niwe au nisiwe mgombea.
2.      Kwa hivyo, nilichozungumza jana ni kutoa maoni yangu kwamba muda umefika kwa Taifa letu kupunguza umri wa kugombea urais. Maoni yangu haya yanatokana na ukweli kwamba hakuna sababu zozote za kisayansi zinazomfanya mtu aliye chini ya umri wa miaka 40 akose sifa za kuwa Rais. Msimamo huu nimekuwa nao tangu zamani nikisoma shule na haujawahi kubadilika. Hakuna mahala popote katika maoni yangu niliyotoa jana niliposema kwamba nataka umri wa urais upunguzwe ili nipate fursa ya kugombea nafasi ya urais. Pia siwezi kutaka katiba iandikwe kwa ajili yangu. Vilevile kamwe isionekane kwamba matakwa ya muda mrefu ya vijana ya kutaka umri wa kugombea Urais kupunguzwa yanalenga kunipa fursa mimi kwani mimi ni binaadamu naweza nisiwe na sifa za kuwa Rais lakini kukawa na vijana wengine wengi wenye umri chini ya miaka 40 wenye Uwezo na Uzalendo wa kutosha kushika usukani wa nchi yetu. Ni maoni yangu kwamba tupate mabadiliko ya vizazi katika uongozi wa nchi yetu ili kukabili changamoto za sasa zinazokabili Taifa letu.
3.      Tunapojiandaa kutoa maoni kuhusu Katiba Mpya ni vizuri vyombo vya habari vikajikita kutoa taarifa bila kuweka tafsiri au kuwatafasiria maoni ambayo wananchi na viongozi watakuwa wanayatoa kuhusu maudhui ya Katiba Mpya.
Dar es Salaam
29 Februari 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Ankal Mhe. Zitto ananikumbusha Mwalimu mmoja wa Kinondoni Sec Hoya akihamasisha Mchezo wa Mpira alikuwa akisema yeye akiwa Uwanjani anaweza kupiga Mpira wa Kona halafu akawahi yeye mpigaji kona Golini na akafunga Goli!

    ''Mchakato wa Umri wa Uraisi''

    SASA KAULI YA MHE. ZITTO INAFANANA NA TAMBO NA MAJIGAMBO YA MWL. HOYA, INGAWA YEYE ZITTO ANAKATAA,,,LAKINI HOYA ALIWEZA KUPIGA KONA NA AKAWAHI KUFUNGA GOLI MWENYEWE!

    ReplyDelete
  2. Mimi naona kama umri wa kugombea urais unatajwa kuwa miaka 40 basi na wa kutogombea urais uwekwe(au upo?) mtu akishavuka miaka 60 asiruhusiwe kugombea urais,akili inakuwa imeshachoka(sina ushahidi wa Kisayansi lakini).Kuna mtu humu barani africa ana miaka 86 bado anang'ang'ania kugombea urais..jamani

    David V

    ReplyDelete
  3. JE KUNA SABABU ZOZOTE ZA KISAYANSI ZINAZOSEMA UMRI UWE 35? JE UNAJUA NI KWA NINI KATIBA YA SASA INAWEKA UMRI WA CHINI UWE 40? JE SABABU HIZO KAMA ZIPO, NI NINI KIMEFANYA ZIPITWE NA WAKATI SASA?
    NAOMBA MTOE HOJA ZENYE MASIKO NA SIO KUONGEA BILA KUTOA ANALYSIS.

    ReplyDelete
  4. Kwani mpaka 2015 huyo Zitto atakuwa bado kufikisha hiyo miaka 40? Mbona basi atakuwa hakui.

    ReplyDelete
  5. Wadau wote na Anonymous wa Wed Feb 29, 04:00:00 PM 2012

    UTHIBITISHO WA KISAYANSI NI 'KUCHEMKA KWA DAMU' KAMA 'MTALIMBO AU MTULINGA ALIONAO MTU WA MIAKA CHINI YA 40 !

    NADHANI SISI WOTE HUMU WADAU WENGI NI AT LEAST UNDER 40 AU AFTER 40 HIVI, SASA WENYEWE STAGES ZA MAISHA YA KUKUA MMEZIONA NA KUZISHUHUDIA TOKEA MKIWA AT 16 MLIONA DALILI ZA KUJITAMBUA NA BALEHE, MKAJA AT 20, AND AT 25 MMENONA.

    HIVYO SAYANSI YA MAUMBILE NA KUJITAMBUA SAMBAMBA NA KUKUA NDIO KIGEZO CHA KISAYANSI.

    KAMA KADRI UMRI UNAVYOENDA MTU HUPUNGUA UWEZO WA KUFIKIRI NA KUMBUKUMBU BASI KADRI UMRI UNAVYOKUWA MDOGO MTU ANAKUWA BADO 'KACHALA' KAMA MMWANAUME AU 'MCHARUKO' KAMA MWANAMKE.

    MWENYE DALILI ZA UKACHALA AU UMCHARUKO DAIMA HANA DHAMANA WALA UWEZO WA KUMUDU UONGOZI !

    ''HIVYO HII KITU KISAYANSI IPO LOGICAL UNDER ABOVE GROUNDS''

    HIVYO UONGOZI UNATAKA MTU WA KATI KWA KATI AT 40 (KIUMRI) SIO AT 60 OR MORE OR LESS THAN 40 ANAKUWA BADO

    ReplyDelete
  6. kwanini 35 na siyo 18, kama kurakebisha basi warekebishe ipasavyo, ni nini tofauti ya 18 na 35, na kwanini siyo 40 hiwe 35. kama mtu kutambuliwa mkubwa ni 18 basi kuanzia hapo sawa, na kama si hivyo bora ibaki kama ilivyo.

    ReplyDelete
  7. Sasa Slaa ndo anatoswa

    ReplyDelete
  8. Ni kama kusema, vigezo vilivyopo vinamzuia fulani kugombea urais hivyo, vipunguzwe ili fulani agombee. Binafsi sijaona sababu ya maana iliyotolewa ili umri wa kugombea urais upunguzwe.

    Kilichopo, nadhani ni janja tu ya Zitto kupima upepo ili aone watu wanasemaje kuhusu ndoto yake ya kugombea urais, kama anafaa au hafai kuliko ajenda ya umri. Nadhani pia anataka kuwaambia chama chake kuhusu nia yake, hivyo anategemea kusikia maoni ya viongozi na wanachama wa chama chake ili aanze kujipanga mapema.

    Ni haki yake kikatiba kutaka kugombea endapo anakidhi vigezo, lakini mbinu hii sio muafaka sana kichama, na kama chama chake kitakuwa makini ili kuepuka migogoro ya makundi ni KUEPUKA KUJADILI AU KUONGELEA ishu yake, hata hivyo 2015 bado mbali sana kwa hili.


    Kibanga Msese

    ReplyDelete
  9. Zito Kabwe ni hodari wa kukosoa. Lakini mimi naamini kwamba kukosoa ni kitu rahisi sana. Mara nyingi mtu kama yeye ambaye tayari anauwaza Urais hafiki mbali. Hizi ni tamaa kwamba anaona magazeti yanampamba.Kiongozi wa magazeti siku zote ni kama Starring wa michezo ya Kihindi ya Bollwood ambapo ikla siku Zito anapambwa na magazeti.Tunafahamu fika wanasiasa wa Bongo ambao kuhonga waandishi ndio kazi yao. Kila kukicha Zito kazi yake ni kulaumu. Hebu tumuangalie Mhe. Dk. Shein. Hakutaman kuwa hata Waziri wacha Urais. Leo angalia Mungu alipomfikisha. Anafanya mambo mazuri hana majungu wala ubaguzi.Amekaa Umakamu wa Tanzania hukusikia kukwaruzana na mtu wala kuhonga magazeti. Leo ni Rais wa Zanzibar. Ssa watu kina Zito na wenzake kina Januari wanafikiria wameiva.Urais jamani si mchezo. Watu hawa itakuwa aliyoyasema Gingrich wa chama cha Republican kwamba mtu ikiwa moto/mvuke wa jikoni kwane unamshinda kuhimili atahimili moto wa White House. Zito na Januari hebu fanyeni kazi majimboni kwenu mulete maendeleo kwanza kisha ndio mufikirie Urais na ukweli ni kwamba mutaonekana muna uchu wa madaraka na hamutafika mbali. Ina laha ma Sabiriin.

    ReplyDelete
  10. Nadhani Zitto anajiona kama mtu wa kitaifa - sikia maneno yake: vijana wanapodai hivyo hawaaminishi mimi. Hivi ni wapi huko kuna madai hayo? Ni yeye Zitto ndiye kinara wa madai haya. Asibebshe wengine.

    Zitto is a snob - yaani mtu anayeoona kwamba chake ni bora zaidi.

    Mwana Chadema hai.

    ReplyDelete
  11. siyo lazima mtu mpaka awe rais ndo aweze kuleta maendeleo na mengineyo ya muhimu ambayo wananchi wanayahitaji. kwa umri wake na kazi yake ya sasa mr kabwe ana nafasi nzuri kabisa ya kuleta mabadiliko ya maisha kwa wananchi wa jimbo lake na taifa kwa ujumla na siyo kukaa kuhudhulia warsha na kuandika makala tu..do something mr you got all the tools NOW !! acha blah blah..

    ReplyDelete
  12. Zitto you are very good, na mimi ni mmoja washabiki wako. Lakini unaongea zaidi ya kuliko unachokifanya. Lakini pia vyema ufahamu kuwa wadanganyika wa sasa tunajua mtu anapotumia media kwa sababu binafsi kwa uzalendo,chapa kazi tetea nchi yako nasi watazania ikifika mda tutaweka mawe barabarani kuwa tupeni Zitto kama mgombea uraisi na sio Mr. NYEPESI kama ulivyo na ndoto zako za sasa.

    Kibanga Msese

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...