Huyu ni muwekezaji kutoka china akikokota mkokoteni maeneo ta mtaa wa livingstone kariakoo Jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. Jamani lazima mufahamu kwamba malezi aliyokulia huyu muekezaji tofauti na sisi.Wenzetu wamezoea kazi wanafanya kwa vitendo na sisi ukiwa na senti kidogo basi wewe ni bosi na hushiki kitu hapo na kitambi kitaanza kukutoka kisa eti anakaa dukani hata kuinuka kumpatia kitu mteja inabidi amwite msaidizi wake ila pesa tu ndio unaipokea.

    ReplyDelete
  2. haya semeni sasa , mnaojifanya muko ughaibuni mnabeba mabox, kumbe mmeondoka bure huku, kazi hizo hizo hata huku ziko na wachina wanazifanya sambamba na sisi wabongo, fanya fanyeni mrudi jamani huku sasa maisha safi, sasa wachina wanazaliana huku na tutakuwa nao Dodoma bungeni. Zebedayo.

    ReplyDelete
  3. Hongera. Hapo anatoa mfano mzuri wa kusave hela. Hapa bongo mtu ukiwa na pesa, nyodo nyingi kiasi kwamba hata box kusukuma huwezi!

    ReplyDelete
  4. Ama kweli mkakataa pema pabaya pana mwita!

    Wandugu Wapiga BOX Majuu mambo Bongo kumekucha mnaona Mchina anawapiga bao rudini haraka kundini, sawa bei ya upigaji box huko iko juu zaidi ya Bongo ndio itakuwa sababu yenu kubwa...muelewe Upigaji Box wenu huko ugenini, licha ya kipato chenu unatutweza na kutushusha sana wote ninyi huko na sisi huku nyumbani!

    ISIPOKUWA MKUMBUKE KUWA,

    1.NGUO YA KUAZIMA HAISITIRI MATAKO!

    2.CHAKO NI CHAKO NA CHA MWENZIO SIO CHAKO!

    3.MKATAA KWAO NI MTUMWA!

    ReplyDelete
  5. Anhaa Idara ya Uhamiaji inabidi muimarishe Mipaka,Kanuni,Vigezo na Taratibu.

    Nina wasi wasi na aina ya Wawekezaji tulio waruhusu, ni vile mwekezaji moja ya Mashariti anatakiwa KUZALISHA AJIRA NA SIO KUBANA AJIRA KAMA HAPA MCHINA, ANAWAWEKA NJAA MAKULI WETU WA KIBONGO KWA KUSUMA KWAMA YEYE MWENYEWE!

    ReplyDelete
  6. kwa hiyo hata sisi tulio ughaibuni ni wawekezaji huku.Acheni bwana huyu jamaa kaja kubangaiza maisha. Kwao maji yalimfikia shingoni kaamua kuja kutafuta maisha bongo kama sisi tunavyoyatafuta huku tulipo.

    ReplyDelete
  7. watanzania tunajua sana kuponda kila kitu eti ooh wachina wanauza pipi ooh wachina wanauza urembo ooh.....;)lakini ukweli sisi ni wavivu hafu ukiwa na vijisenti kidogo nyodo, ubosi na majigambo waacheni wachina wapige box hafu mwisho wa siku wakifanikiwa tukaombe kazi kwao!

    ReplyDelete
  8. Mie nawashangaa sana hawa uhamiaji kwa kuwalea watu hawa! kwani waliomba kuja kama wawekezaji lkn wanaishia kuwa machinga K'koo wakifanya kile kile cha kuuza viatu rejereja kama vijana wa kichaga! tukiwachongea wanaishia kwenda kuchukua vihela na kuwaacha! Tunaapa ipo siku K'koo itakuwa 'tutafungua BUCHA' kwani tumechoka

    ReplyDelete
  9. Nyie fikirini wanasukuma box,,,muda ukifika wa kile wanachotaka kufanya ndio mtajua walikuwa wanasukuma box kariakoo au la! Wakati wabongo tunapanga mipango ya 5 years tena isiyotekelezeka, wenzetu wanapanga mipango yenye akili ya miaka 50-100 ijayo! Yetu macho!

    Eddy

    ReplyDelete
  10. Shame on us!!

    ReplyDelete
  11. Wasomi wetu hiyo ni changamoto kwenu, wengi mnalia ajira hakuna lakini mnaachia hizi fursa kwa wageni na kuanza kuwabeza, ni wakati wasomi muache kuchagua kazi na kuzibeza, kinachotakiwa ni kutumia elimu yako kujiendeleza bila kusubiri utumwa wa kuajiriwa huku ukijitapa umeajiriwa wizarani au shirika binafsi...ajira zipo lukuki kama izo za kubeba box, ukulima, ufugaji, nk...

    ReplyDelete
  12. most africans they dont plan even one day ahead
    sasa wewe unaelilia watu warudi kutoka ulaya eti bongo kumekucha unahustify nini hapo,wewe kama ulipigwa bomba sasa guilty usituzingue kila mtu atarudi kwa mda wake.
    pia upigaji box ulaya health and safety inazingatiwa huyo mchina hapo kwa kudra za mwenyezi alifika salama

    ReplyDelete
  13. wabongo kwa husda mwisho! hapo jamaa wa kichina sie anaebeba anamsaidia m'bongo mwenzetu na pia analinda mali yake ifike salama ,au mnauna huyo wa mbele pia ni mchina?

    ReplyDelete
  14. Analokota takataka za kuja kutuuzia sisi wajinga watanzania! Yaani hata Mimi nitaanza ku'package' mavi na taka nyinginezo nizi label vizuri 'made in China' niwauzie wajinga wenzangu Kama dawa, colgate, chakula n.k.. Hivi Tz hatuna 'bureau of standards'? Aise ngoja baada ya 10 years+ tutaoba madhara ya ujinga wetu! P.S. I won't be surprised hata hiyo 'newly-found oil' kwenye mkataba wamekubali kuipa the foreign company/country majority of the share! Kwahiyo waTZ hatutanufaika chochote na ujinga wetu. Sometimes I wish tungekuwa na watu Kama akina Mugabe hivi...

    ReplyDelete
  15. Haya nyie wabongo mliokwenda chukua uraia huko ughaibuni sasa sijui itakuaje ? Hivi mnaweza kuona jinsi gani bongo inavyobadilika? Huku kila mtu kushughulika kwenda mbele na ndio hivyo bongo inavyozidi kuendelea . Wazungu hawahesabiki, hao hao wamarekani mliowafuatia huko wao sasa wanakuja kwetu na wote katika ubebaji wa box, kama hamji kwenu eti ulaya kuzuri mtakiona hapa bongo siku huzi hakuna nyumba ya shangazi wala ya binamu yangu kila mtu kaamka hakuna terna ule undugu mliokuwa mkiujua ninyi! Bongo tofauti sana siku hizi, Wengine nasikia mmeukana utanzania kwa sababu ya kupata passport ya Ulaya mli msafiri kirahisi, mmejidanganya huku sasa mnakuja kwa VISA na ukioverstay unafungwa na kupigwa bomba huko makojifanya ni kwenu,Mmefulia washiukaji wengine hata kuja bongo ni issue eti mnawatunza wanawake wa kizungu huko majuu mnaona mmefika sana ,shauri yenu huku bongo kiwanja sasa cha nyumba hata kama ni Chanika au Nzega ni kuanzia million 100, kwa taarifa yenu. Rudini bongo acheni kuosha mikundu ya wazungu wazee huko kwenye manyumba ya wazee Ulaya, hio ndio elimu mlionayo!na kusahau kwenu hata mfanye kazi miaka 10 mfululizo mtu hata $ 1500 hana benki eti yuko ulaya, njooni tujenge kwetu bongo! msibweteke.

    mdau Temeke

    ReplyDelete
  16. Tuna matatizo kidogo kwenye ufanyaji wa biashara.Angalia historia yetu. Kuna wakati wafanya biashara nchini walikuwa wahindi na baniani na kiatu chake, kabla ya hapo alikuwa mmanga na kilemba chake.Sasa mchina naye yupo nchini.Miye siyo kama nawapinga ila nauliza kwa nini wabongo hawajishughulishi zaidi na biashara.Ikiwa wabeba maboxi ughaibunu kwa nini hawarudi bongo na kubeba hapa.Hapo juu naona kuna malalamiko na kauli zenye fikra, miye nawaambia. Take a look and see the man in the mirror.
    Anon, permanent kikapu resident

    ReplyDelete
  17. Binadamu siku zote hatukosi sababu. Kila mtu anatafuta riziki kivyake. Jamaa ameagiza mzigo anahofia mtaani watachakachua kwa hiyo analinda mwenyewe kwani kosa? Ni kweli kabisa mdau aliesema sisi tukipata hela kidogo basi miguu juu, kila jambo unatoa oda tu!!
    Warren Buffet na mihela yake yote bado anakaa kwenye nyumba yake ile ile mpaka kesho, leo hii sisi tukipata hivyo vijisenti basi tunataka kukanyaga watu wote.

    Tujifunze na tusilewe utajiri. Dunia yenyewe tunapita tu, leo tupo kesho hatupo.

    ReplyDelete
  18. Huyu si mwekezaji. Ni mchumaji. Naona tuna dhana ya kuwaona wageni wote wanaokuja Tanzania kama wawekezaji.Huyu kaja kuuza bidhaa zake na at the end of the day hawekezi chochote kwenye uchumi was Tanzania. Zamani huyu tulimwita mlanguzi.

    ReplyDelete
  19. Bongo Tambarale,

    Muelewe kuwa, mpaka Mchina kukubali kusukuma mkokoteni pamoja na Elimu yake yote na $$$$ Dola zake alizokuja nazo,

    Habari ndio hiyo!

    ReplyDelete
  20. Duhhh,

    Nchi imetekwa!

    Jamani tukale wapi?, ama kweli kwa sasa nguvu sio mali tena kama zamani!

    ReplyDelete
  21. Watanzania Majuu ahhhh,

    Mnaona hii?

    Heshima ya mtu ni kazi, baba Nyerere alituambia sasa ni wakati muafaka mje kukeba box nyumbani Tanzania badala ya kubeba box utumwani huyo Ughaibuni!

    ReplyDelete
  22. dah ama kuwa nje tunanyanyasika

    ReplyDelete
  23. MDAU WA TEMEKE PUNGUZA LUGHA CHAFU KWANI KUNA MTU WA ULAYA ALIYEKUOMBA PESA YA KULA?JAZBA IMEKUJAA NAHISI ULINYIMWA VIZA WEWE UKAE UKIJUA MAISHA NI KOKOTE.

    ReplyDelete
  24. mindset yetu wa-Tanzania ya ajabu.

    mchina huyu anaonyesha jinsi ya kuwa serious na kutafuta riziki kwa kufikisha mali yake kwa haraka kwa kumsaidia msukuma mkokoteni huku akizingatia usalama wa mali yake na usafiri wa nafuu.

    ReplyDelete
  25. Kweli binadamu wabinafsi na wabaguzi sana,hata chakula wasichotaka kula wao wanataka hata mwingine aliye na njaa asile bora kitupwe.

    Ninyi wengi mumekimbia kwenu na kuishi ugenini na kuona kwenu hakufai na hakuna kitu,sasa mgeni akijakuishi na kutafuta mlichokikimbia pia hamtaki.Mumeona TZ hakuna kitu na hapafai mkaenda majuu,leo mchina kaja mwataka uhamiaji imuondoe pabaki hivyo hivyo.Loooh!Ubinafsi huu mpaka tunatia huruma.

    Wachina wafukuzwe,mbona ninyi pia mko ughaibuni kwa wenzenu?Huko mnakokatalia na kufanya kazi zisizokusomea ndo kwenu?Wacheni kuchonga jamani,kila mtu mwacheni anapopaona panamfaa.Kikubwa tuulize anakibali cha kuishi na cha biashara na kulipa kodi?Ninyi mnauliza anawekeza,je ninyi huko mliko kwa watu mnawekeza?

    Mnapinga wengine kuja kwenu!Hivi mnajua kuna wa TZ wangapi China wanabangaiza!Kenya,Zambia ,Malawi,UK,USA,na kwingineko halafu hamtaki wengine waje kwenu.

    WEWE UKISEMA CHA NINI,MWENZIO ASEMA NTAKIPATA LINI.Ninyi rudini mkizeeka cha moto mtakipata.

    Kuponda kwiiingi,oooh TZ hakuna hki,oooh TZ watu wakoje!Wapi hakuna hayo.Wadanganyeni wasiokujua majuu.Jengeni mawzo nyie binadamu acheni kebehi,dharau,na majigambo uchwara.

    ReplyDelete
  26. NYIE MBWETEKE TU MKIPIGA GUMZO NA KUNYWA ULABU NA MAPARTY, NA KUSEMA ETI KAZI YA BOX.
    Wabongo tuna tabia mbaya sana kudharau kazi.
    Ulaya watu hawachagui kazi au mzungu au mgeni, na mara nyingi ukikutana na mtu mkasalimiana, hakuulizi unafanya kazi gani, bali ''HOW IS WORK?'',
    Ikionyesha kuwa cha msingi ni mtu kufanya kazi na kupata kipato. Hakuna kuishi kwa wizi wizi na utapeli, kila kitu ni kwa jasho lako kwa haki, ndio maana wenzetu wako mbali sana.
    ACHENI USHAMBA NA UJINGA.

    ReplyDelete
  27. Mdau wa Temeke inaonekana ulinyimwaga VIZA , tuliza ball uki-compare currency ya bongo na kokote nje ya nchi hata kwa watani wetu "KENYA" Tz /= shillings still ipo chini.Kwahiyo waache watafutaji wa Ughaibuni waendelee kutafuta. Kwa taarifa yako kuna Eatanzania waliopo ughaibuni wengine ni Walimu, Police officers, Makarani wa Bank , Engineer, Doctors nakadhalika. Wameamua kuondoka hapo Tanzania sababu kwa profesionals zao wameona malipo hayatoshelezi wala hawaheshimiwi ipasavyo. Na wengi tunaowajua wameinvest hapo bongo kama huna habari walinunu hivyo viwanja kabla wewe hujajua vitapanda hiyo price . Kwahiyo tuliza ball.

    Mdau Texas.

    ReplyDelete
  28. LOOL!!!HIVI KWANINI WALAVUMBI BONGO WANA JAZBA SAANA NA WABONGO WA UGHAUBUNI.NAFIKIRI UGUMU WA MAISHA TANZANIA,VUMBI,JUA KALI N.K../.LINACHANGIA MTU KUONGEA ONGEA OVYO KAMA HUYO MDAU WA TEMEKE.

    ReplyDelete
  29. Nadhani ujumbe umewafikia wanaoponda nchi na wenzao wanaobaki na kuchapa kazi TZ.Hao wasema ovyo kuwa hawana sera.

    Fanya ya kwako acha kufuata ya mwenzio.Wewe huku una ninin weweee.

    Mchina kaja TZ mwache aishi na afanye biashara mradi awe na kibali na alipr kodi.Na wewe ishi huko unakoona ni mali.

    Waangalizi wa sheria wako kule bongo waache na kazi zao.Huko ughaibuni mnakodhani ni makini zaidi mbona wako wanaendesha magari bila leseni,watu wa madawa ya kulevya,wezi wa magar,wagoni,walevi,wanaotelekeza familia,wameacha wake au waume.

    Kila kitu kibaya mnaipa TZ.kwa wasomi wote wanajua kuwa popote anapoishi bimadamu kuna kila kitu kama kwingine.Msichanganye maendeleo na tabia huo ni ulimbukeni.

    AKINYA BATA NI UCHAFU,LAKINI AKINYA KUKU NI MBOLEA.

    Acheni ulimbukeni wacheni watu waishi na wafanye biashara mlizozikimbia.Rukeni mkojo kanyageni mavi.TZ kumekucha kwa wanao jituma na kujihangaisha.

    Barabara TZ zateleza na ni nzuri.Nenda Mtwara,songea ,Bukoba,Arusha,Mbeya,Singida,Tabora kwa taxi.

    Karibuni TZ na mnaoishi huko jitumeni msibahatishe,biashara si utapeli walka majungu.Fanya unachoweza waacha ya mwenzako.

    ReplyDelete
  30. ngojeni 2025 tunaanza kuingiza mchina wa kwanza bungeni....taratibu mtatukubali tu sisi sio kama wahindi wanaowaogopa,sisi tuko nanyi,maji ya kiroba tunakunywa,lugha yenu ya kiswahili tunajifunza fasta,box tunasukuma wenyewe na uswahilini pia tunaishi mhogo wa kuchoma na tembele tunapeleka pwani.malengo yetu mtayaona kuanzia 2025 tukishaanza kuingia mjengoni na kuvuruga sheria zenu ziwe zinatoa haki zote kwetu.BONGO SHAMBA LA BIBI,KAMA HUJAWAHI KUWA TAJIRI MAISHANI MWAKO NJOO BONGO MARA MOJA UNAKUWA KIBOPA

    ReplyDelete
  31. Cha ajabu nini wachina kuja kuingia bungeni!Huoni huko ugahibuni na bunge lao unadhani wote ni waingereza asilia,au marekani?wewe bwabwaja tu.

    Kma sheri itaruhusu cha ajabu nini.Hapo mlipo mnataka uraia mbili kwa udi na uvumba na kuwatumia wazazi wenu vigogo ili muishi kwa wenzenu. sasa mkiupata bado mwabagua wachina.

    Pale ilipo roho ndo nyumbani mnataka nini.Ulaya wadhani ndombinguni.Sasa kama bongo mshahara mdogo au kuan matatizo ndo mkimbie kwenu.

    Sawa mumeondoka muko pazuri,sasa bongo mnaisakama ya nini.Kaeni na maisha yenu huko mliko na waacheni walioamua kufa na nchi yao na shida zake iwe jua,iwe mvua.Hao ndo wajenzi wa nchi.Midabwada ninyi.

    ReplyDelete
  32. Hata wewe umekimbia kwenu, wangapi kati yenu ni wenyeji wa Dar es salaam?? Maisha popote .

    ReplyDelete
  33. Ohhh

    Wabeba MA BOX Majuu , Mchina anawamalizia mzigo wote huku Bongo fanyeni haraka mrudi kuja kula naye sanahi moja hapo kwenye Godauni la Mizigo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...