Familia ya Mwanamuziki Whitney Houston ambaye alifariki Dunia Jumamosi ya wiki iliyopita,imewasikitisha maelfu ya mashabiki wa mwanamuziki huyo kutokana na utaratibu wa maziko ya mwanamuziki huyo kuwa ambayo yanafanyika leo kwa kuhusisha familia na wale watakaopewa mwaliko maalum tu.

Sehemu waliyopanga yafanyike mazishi hayo ina uwezo wa kuchukuwa watu 1,500 wakati awali kulikuwa na taarifa kuwa zoezi la kuuaga mwili lilikuwa lifanyike katika Ukumbi wa Prudential Center unaochukuwa watu 18,000.

Mume wa zamani wa marehemu, Bobby Brown ana uwezekano wa kukosa kuhudhuria maziko kwa kile kinachodaiwa kuwa familia haimuhitaji tena kwa sababu alishatengana na Whitney Houston.

Bado kuna wingu kubwa la maswali likiwa limetanda juu ya kifo chake kwani watu wa karibu na marehemu wameeleza kuwa siku chache kabla ya umauti kumfika alisema anataka kuonana na Yesu na alikuwa akisisitiza juu ya hilo pia shoo yake ya Mwisho kuifanya alivaa nguo nyeusi tupu.


Peter Tatchell ambaye ni mtetezi wa haki za watu wa jinsia moja wenye uhusiano wa kimapenzi aliandika katika mtandao wake kuwa, Whitney aliwahi kuwa mmoja wao lakini alifanya hivyo kwa siri miaka ya nyuma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Ila huyu dada alikuwa 'mkali' enzi za ujana wake hey??

    R.I.P Whitney...

    ReplyDelete
  2. R.I.P Whitney. We will always deeply missing you.
    You touched so many hearts across the world through your magical voice in your songs!

    ReplyDelete
  3. @2,"We will always deeply miss you"

    ReplyDelete
  4. anazikwa Sunday 19th February 2012

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...