Kamishna wa Maadili, Jaji Mstaafu Salome Kaganda akitoa maelezo kwa Waandishi wa Habari kuhusu zoezi la Uhakiki wa Mali za Viongozi wanaohusika na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Katibu Msaidizi Viongozi wa Siasa, Bibi Coletha Kiwale (wa kwanza kulia) akisoma maelezo kwa Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa Uhakiki unaotarajiwa kuanza tar 20 mwezi huu.
Waandishi wa Habari wakiwa “bize” kuandika habari kuhusu zoezi la Uhakiki.

Na Rocky Setembo - Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inatarajia kuanza zoezi la Uhakiki wa Mali za Viongozi, hususani wale wanaouhusika na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995.

Akiongea na Waandishi wa Habari Makao Makuu jana, Kamishna wa Maadili, Mheshimiwa Jaji Mstaafu Salome Kaganda amesema kwamba, zoezi hilo litahusisha Kanda zote, yaani Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kati, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kusini na Makao Makuu. Aidha, Uhakiki huo umepangwa kuanza tarehe 20 Februari hadi tarehe 1 mwezi Machi 2012.

“Kwa kuwa idadi ya Viongozi ni kubwa, Sekretarieti ya Maadili itaanza na uhakiki wa Viongozi 60 wenye nyadhifa tofauti. Hivyo, napenda kuchukua fursa hii kuwasihi Viongozi wote ambao wamepangiwa kufanyiwa uhakiki huo kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Maafisa wetu ili kuweza kufanikisha zoezi hili” Alisisitiza Mheshimiwa Kaganda.

Aidha, kutokana umuhimu wa uhakiki huo, Kamishna wa Maadili ameomba ushirikiano toka kwa wananchi, kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kugundua mali zilizofichika ambazo zinasadikika kuwa ni za Viongozi wa Umma wanaohusika na sheria ya Maadili.

“Katika zoezi hili, ushirikiano na uwazi ndiyo msingi wa utekelezaji bora wa uhakiki huu kwa kuwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inaamini kwamba, kwa ushirikiano wa pamoja Tanzania yenye Viongozi Waadilifu inawezekana.”

Naye Katibu Msaidizi Viongozi wa Siasa, Bibi Coletha Kiwale, ameeleza kwamba, zoezi la Uhakiki wa Mali za Viongozi ni moja kati ya majukumu ya Taasisi kupitia kifungu cha 18 (2) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, hivyo Viongozi watakaofanyiwa uhakiki huo waelewe kuwa wao si watuhumiwa, kwa kuwa zoezi hilo huwa ni la Viongozi wote wanaohusika na Sheria ya Maadili.

Pia, alitoa tahadhari kwa Viongozi hao, kuwa makini na watu wanaojulikana kama “matapeli” ambao hupiga simu na kujifanya Maafisa wa Sekretarieti ya Maadili wakidai kiwango fulani cha pesa, wapatapo simu za aina hiyo, watoe taarifa Polisi au Sekretarieti ya Maadili haraka iwezekanavyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Hivi nini faida ya kujua mali za viongozi?

    What actions wanachukuliwa wale walijilimbikizia?

    Na wale wanaoandikisha majina ya watoto zao, wajomba zao, ndugu zao?

    VERY FUNNY - ISN'T IT.

    ReplyDelete
  2. Mbona sijawai kusikia viongozi wanatangaza mali zao afadhari kuacha kuliko kupoteza muda mwingi

    ReplyDelete
  3. Samahani naomba nisieleweke kwamba mimi ni mbaguzi wa kijinsia lakini niko gender sensitive!

    Mbona inaonekana safu nzima ya sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma ni ladies tu?

    ReplyDelete
  4. Ni rahisi sana na haina Elimu iliyopindukia kutambua kati ya 'mali safi' na 'mali chafu'.

    Ni kupiga mahesabu ya thamani ya umiliki fedha na mali zisizoendesheka halafu halafu inatazamwa kwenye MAMLAKA YA KODI KAMA THAMANI ALIYOLIPA MUHUSIKA NI 18% YA MALI YAKE?,,,IKIWA SIYO MUHUSIKA ATAKUWA MWIZI ANATAKIWA AFIKISHWE KWENYE SHERIA AHUKUMIWE NA AFILISIWE MALI!

    ReplyDelete
  5. Kumkamata Kiongozi Mwizi wa mali za Umma hakuhitaji UJUZI!

    Ni kiasi cha Kumuomba Fundi cherehani wa ushonaji meta ya kupimia, halafu unazungusha kupima ukubwa wa tumbo lake ukikuta UKUBWA WA TUMBO haulingani na MSHAHARA wake elewa huyo ni Mwizi wa Mali ya UMMA!

    ReplyDelete
  6. badala yakufanya mambo muhimu wananza kupoteza muda kama vile hawana kazi. Ufisadi unajulikana kabisa watu gani wana mali kiasi gani. watu gani wamejiuzia majumba ya NHC na mengineo. Tafuteni kazi muhimu tuache kupoteza muda na resources.

    ReplyDelete
  7. au hiki kimekuwa kitengo cha umafia. ukiwa na nyumba kumi nipe mimi moja tuyamalize. Mafisadi wanajulikana..

    ReplyDelete
  8. Njia rahisi za kutambua Viongozi Wezi wa Mali za Umma ni:

    1-Kushirikiana na Kliniki za Mahospitalini, Viongozi wafunguliwe Kadi za Kliniki tokea wanaajiriwa,wawe wanahudhuria kila mwisho wa mwezi wanapimwa ukubwa wa matumbo yao na Rekodi kujazwa ktk Kadi zao.

    2-Wawe wanawekewa rekodi za Mahudhurio yao ktk ma Baa na sehemu za Ulevi.

    3-Wewekewe rekodi za muda wa kurudi majumbani mwao, na Mahudhurio yao huko nyumba zao ndogo.

    Kwa njia hizo za kurekodi taarifa kusoma mwenendo huo itakuwa rahisi kuwatambua Viongozi wezi!

    ReplyDelete
  9. chanzo cha ufisadi nchini si hao ministers na CEO,S ni system mbaya iliyoko hazina na idara za uhasibu kwenye mashirika na mawizara.kwa hiyo wajaribu kutazama kina cha tatizo siyo tunadanganywa hapa.Nadhani kuna haja ya kuelimisha watu wengi system ya pesa zao wanayoilipa serikali zinavyotumika,hata kama wahasibu wanafraud kuwapa report mbovu itajulikana tu.wapinzani nadhani mpo tu kwa kuangalia kuibiwa kura na siyo kuchunga hela za mwananchi.Zitto naona bado umelala,wahasibu wanakuchezea akili

    ReplyDelete
  10. waandishi...hiyo ni NOTE BOOK, DIARY AU DAFTARI LA MAZOEZI la mwanafunzi wa shule. too much. fani imevamiwa hii. balaa kitu.

    ReplyDelete
  11. yaaani bongo bwana kazikwelikweli ni kama comedy flani hivi,mkiwajua mtawakamata? au ndo chalimkaranga!,lol ukisitaajabu ya musa..........;)

    ReplyDelete
  12. Ahhh wapi kumchinja Kobe kwataka taimingi!

    Hawa jamaa mali zao wanaandikisha ndugu zao na jamaa zao wa karibu ama wanaweka nje ya nchi!

    ReplyDelete
  13. Hao wezi wa mali za Umma ktk Afrika yetu wengi wao ni Wasanii waliobobea na wenye akili za ziada.

    Anaweza mtu kubuni kitu ambacho kwa hali na mtazamo wa kawaida huwezi amini kutokea.

    Mfano Kenya usanii wa Kifisadi ulifanywa miaka ya 2000 na Wazito kadhaa wa Serikali ya awamu iliyopita.

    Walifungua miradi hewa miwili:

    1.DEEP GREEN HOLDINGS L.L.C
    2.ANGLO GOLDBERG INVESTMENT CO.

    Sasa kwa kipindi hicho hakukuwa hata na dalili kama Kenya itakuwa na dhahabu lich ya kuwa sasa imeonekana kuchimbwa karibu na mpaka wa Tanzania mwezi Disemba 2011.

    Lakini kwa majina hayo mawili ya Miradi hapo juu hela ndefu ilivutwa,,,mpo hapo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...