Ndugu Michuzi
Kufuatia mabadiliko mengi katika jamii zetu za kiafrika, hasa katika nyanja za kimaisha, napenda kuiuliza jamii yetu issue ya 'binti ku-propose kwa kijana anayempenda'. Wenzetu wa magharibi, ni jambo la kawaida kwa binti ku-propose kwa kijana anayempenda kuwa yuko tayari ku-engage naye na hatimaye kufunga ndoa na kuanza 'maisha' pamoja. Je katika jamii zetu ambazo zinakumbwa na kasi kubwa ya kile kinachoitwa kwenda na wakati, binti akifanya hivyo kwa kijana anayempenda bado ni sawa?

Salaam 
Jogoo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Hiyo kwa taratibu za Maadili yetu ya Kiafrika inakubalika ili mradi huyo anayempendekeza Binti awe ana vigezo vinavyokubalika kwa Jamii ktk mwenendo na sera zetu Kimaadili kama Waafrika.

    ReplyDelete
  2. Brother, sijui una maana gana na swali lako. Sasa kupata hako ka chance ka kwenda Ulaya sasa na wewe umebadilika na kuwa mzungu?
    Na mimi naomba nikuulize swali, "Hivi kwa kuwa wahehe wanakula mbwa basi watanzania wote wale mbwa? Please use your common sense.

    ReplyDelete
  3. Kwa Maisha ya Kisasa ama kweli Shughuli tunayo unakuta Binti anawaletea Mwanaume 'Kachala' kutoka kusiko julikana anataka aolewe!

    Mkikataa anasema atajiua au anaondoka na kwenda kuanza nae maisha mapya mwenyewe nje ya Ndoa na ridhaa za Familia na Wazazi!

    ReplyDelete
  4. we wa wapi?????? sio kila ki2 2naiga vingine vyaja AUTOMATICALY mwanamke kupropose ni kawaida na mwanaume nae sio kwakuwa mwanamke kaanza basi akubali hata km alikuwa hataki anaowezo wa kukataa vilevile.MAISHA YANASONGA

    ReplyDelete
  5. kwa upande wangu sioni kama kuna tatizo ila kwa jamii yetu ya kiafrica mtoto wa kike kuwa na huo ujasiri wa kupropose hata anayeproposiwa anamsoma huyo mdada tofauti. inawezekana ni kutokana na
    malezi, utamaduni au mila zetu.

    ReplyDelete
  6. Haya mambo inategemea na tamaduni za mahali hawa wanchi za magharibi tamaduni zao ndivyo zilivyo kwanza wao kitu kinachoitwa maadili hakipo lakini kwa destuli zetu za kiafrika mwanamke kumuanza mwana umme ni vigumu labda kwa siku hizi mijini wanaweza kufanya hivyo kulingana na maisha na wakati mfano mjini wasichana wanavaa suruali lakini ukienda uko vijijini wasichana kuvaa suruali wanaona haaibu basi inategemea mtu kama huyo kulingana na maadili yake sidhani kama anawezakuanza kumtongoza mwanaume

    ReplyDelete
  7. "usiige kunya kwa tembo, utapasuka msamba"

    ReplyDelete
  8. Ni sawa tuu Ankal mwisho wa siku Upendo ni Kati yao.

    ReplyDelete
  9. Ni sawa tuu Ankal mwisho wa siku Upendo ni Kati yao.

    ReplyDelete
  10. Ipo kinyemela, bado haijakuwa wazi wazi, kwa walio na fedha si tatito ila kwa kapuku utaanzaje?

    ReplyDelete
  11. Kwa asili ya Utamaduni Mila na Desturi zetu imekuwa kwa kipindi cha nyuma kuwa Msichana au Mvulana wana chaguliwa wachumba wa kuoana.

    Nakumbuka mwaka 1975 nikiwa ningali mdogo sana jirani Kijijini kwetu alikuwepo mtu mmoja akiwa anafanya kazi ya Kuchonga Vinu, Jamaa kwa Ujasiri na Uanaume wa Kipindi hicho akatoka Kiume kuja kwetu kumposa dada yangu ambaye ndio kwanza Msomi amepata Diploma yake ya Ualimu amekuja Kijijini kusubiri kupewa Posti ya mahala pa Kazi.

    Dada yangu lohhh kusikia jamaa ni Mchonga Vinu akakataa!

    Isipokuwa Wazee Kijijini hawakutegemea msimamo wa dada yangu, wenyewe walijua mwana wao amepata Mume tena Mchapa kazi na mwenye kuheshimika na kujiheshimu Kijijini.

    Matokeo yake dada akaolewa na Bosi wa Mjini ambaye ndoa yake ilikuwa ni ya Mzungu wa nne na mwenzie huyo kwa Maisha ya mshike mshike jamaa Bosi mkorofi na mlevi kupindukia ,mpaka ikaja tokea nikamsikia dada akilalamika na kujutia uamuzi wake wa kumkataa Mchumba wa kwanza aliyekuwa Mchonga Vinu,,,akisema ni bora angeliolewa na yule jamaa wa Kijijini Mchonga Vinu labda angekuwa na ndoa ya fuhara!

    ReplyDelete
  12. mbona wanapropose,ukisikia mitego ndo mwanzo wake mkishaanza ku_do ndio atakuganda kwa ndoa,SHIDA KWA SASA HAWA MABINTI HAWAPENDI TENA NI PESA,TAMAA,MAGARI,NYUMBA

    ReplyDelete
  13. Hio ipo brother mbona mimi mchumba wangu kani propose! Mbele ya Ofisi na wafanyakazi wenzangu na BOSS wangu alikuwepo , na yeye akishindikizwa na rafiki zake wawili. Nilishtukia kaingia na bunch la maua, moja kwa moja mpaka nyuma ya Desk la Bank ninayofanya kazi mimi, Na haukuwa siri alisema kwa sauti: I LOVE YOU AND I WANNA BE WITH YOU FOR THE REST OF MY LIFE, WILL YOU MARRY ME? niliingiwa na uoga kidogo lakini kutoka BUTTOM OF MY HEART nikajibu ndiyo L LOVE YOU TOO! hivi sasa tunasubiri kupanga tarehe ya kuthibitishan kama mke na mume. inawezekana kwani wasichana wasiwe huru kumpropose Ampendaye.
    Chris, Axim Bank
    dar

    ReplyDelete
  14. WEWE JAMAA WA EXIM USITUYEYUSHE, HUYO DADA KAPROPOSE SABABU INAONEKANA NI DEMU WAKO...LAKINI MSICHANA WA KIBONGO AKUONE NA KUKUPENDA INAKUWA NGUMU KUANZA KUKUTOKEA. ACHA SIFA WEWE HUYO DEMU WAKO 2

    ReplyDelete
  15. Mimi nadhani tulinde utamaduni wetu, kwani wenzetu wanao fanya hivyo hiyo ni tamaduni yao basi na sisi tusiige mwishowe tutapotea bure

    ReplyDelete
  16. Hakuna, tuendelee na utaratibu wetu wa zamani wa kuwatongoza dada zetu..inapendeza..unamtongoza anaangalia chini,anauma kidole..haaa haaa.Siku hizi hawaumi vidole tena..utandawazi

    ReplyDelete
  17. Sio kweli kwamba nchi za magharibi ni kitu cha kawaida!

    ReplyDelete
  18. KIUKWELI DUNIA IMEBADILIKA SIO KAMA ZAMANI. MAADILI HAYAPO KWA BAADHI YA WADADA, HUYU MTU YAWEZEKANA KWELI YAMEMKUTA.ZAMANI ILIKUWA NGUMU SANA MDADA KUANZA KUMUAMBIA MWANAUME KUWA ANAMPENDA ILI WAOANE/NDOA. MWANADADA AMEUMBWA NA AIBU NDIVYO ILIVYOKUWA ZAMANI NA ALIKUWA ANASUBIRI HADI KUCHUMBIWA LKNI SASA HIVI HAKUNA KITU KAMA HICHO. TENA UNAKUTA ANATAMBA NA KUWATAMBIA WENZIWE "AABABU NIMEMPENDA NA NIMEMWAMBIA KWANINI NIUMIZE MOYO WANGU?" MIMI NAONA WANAUME NI WACHACHE HALAFU WANACHAGUANA SANA, TAJIRI KWA TAJIRI, HOHE HAHE KWA HOHE HAHE, NDIO MAANA UNAKUTA MTU ANAHAHA HADI APATE WA KWKE ANGALAU AOLEWE. KIUKWELI NI NGUMU MWANAMKE KUANZA AGENDA YA KUOANA MWANAMKE ANATAKIWA KUPEWA REQUEST KUTOKA KWA MWANAUME THEN MDADA AKUBALI AU AKATAE. ISTOSHE SIKU HIZI WADADA WANA FEDHA ZAO KWA HIYO WANA POWER SANA NA WENGINE WANAWAPA SUPPORT WANAUME ZAO HADI KUWASOMESHA VYUO. MAISHA YAMEBADILIKA UWAZI NI MKUBWA WANAIGA NCHI ZA WENZETU. HIVYO MKUBALI MSIKUBALI HAYO YAPO SANA ILIYOPO TU NI MAKUBALIANO YENU NINYI WAWILI MWANAMKE NA MWANAMME.

    ReplyDelete
  19. Sasa jamani anon. wa Wed Feb 29, 01:34:00 PM 2012, ulitaka awe demu wako ndo aende ku propose kwa jamaa wa EXIM? Yeye kasema kuwa mchumba wake amekuja akapropose na jamaa akakubali..kwani shida iko wapi? Kama demu akipropose na hutaki unakataa tu hakuna shida. Hata wewe unaweza ku propose ukakataliwa vilevile.

    ReplyDelete
  20. Hawasemi moja kwa moja bali hutumia vishawishi fulanifulani hivi na mambo ya kona kona,ili mradi mwanaume ugundue kuwa demu kakuzimia.Nina rafiki yangu ambaye nilikuwa naye chuo kulikuwa na demu darasani kwetu ambaye alimzimia huyo rafiki yangu.Bila hiana siku moja tukiwa tuko mwaka wa tatu alimwendea peupeeeeee akamwambia ninakupenda kaka ningependa kujenga nawe familia.Jamaa pamoja na kwamba hakuwa na wazo lakini aliheshimu sana approach ya yule dada na akaingia laini, na hivi sasa wana watoto wawili. kaka yangu mimi niandikaye hapa alitongozwa na na ambaye ni mke wake, na alinitumia mimi kupeleka habari kwa kaka yangu.

    Kijumla inategemea na ujasiri wa mtu na focus yake kwa mtu anayemzimia kwa dhati.Kwa sasa hivi ndo kabisaaaaa kina dada wakikuona unazo mfukoni hawajivungi kukutafutia njia ya kukupata maana mnaooa miaka hii mna kazi maana wanawake wameangalia zaidi kipato kuliko upendo wa kweli.

    ReplyDelete
  21. jamani eleweni swali la mheshimiwa...hajauliza kama inafaa kwa mwanamke kumtongoza mwanaume ili waanze mahusiano....ameuliza kama inakubalika mwanamke kupropose kwa mwanaume anayempenda kama wanaweza kuvuka stage ya kuwa wapenzi na kuanza maisha ya ndoa kama mke na mume.... utapropose vipi kwa mtu ambaye hampo kwenye uhusiano??

    ReplyDelete
  22. nin maana ya kupropose kwa kishwahili?!naamin si sawa na kutongoza,ila nahisi ni kama binti kakutokea ghafla akasema anakupenda pasipo wewe kuwa na wazo la kumuoa wakati yeye kusema hivyo akimaanisha umuoe...je ni sawa kwa mila zetu?!

    Chibulu,
    Australia.

    ReplyDelete
  23. man proposes but God disposes:-

    NINI MAANA YA PROPOSE KWANZA?

    Halafu ndo tuendelee na malumbano!


    Malcom Nipo na wewe mkulu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...