Ukiangalia kwa maki kwenye hilo Tangazo hapo ukutani utabaini kitu na unaweza sema mwenye gari hili hakukosea kuegesha gari lake hapa,na itakuwa alilielea kama nilivyolielewa mimi na ndio maana akaegesha gari yake hapo.lakini kwa ustadi mkubwa wa kazi yao vijana wanaohusika na uegeshaji wa hovyo wa magari,wamefunga chuma lao kwenye tairi la gari hilo.sasa sijui inakuwaje hii??
Ukiangalia na picha hii utaona na magari mengine yameegeshwa katika eneo hilo hilo,lakini hayajapigwa pini wala nini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Anaweza akashinda kesi vilevile kwasababu lugha iliyotumika ni ya kigeni na sio wote wanaojua lugha za kigeni.Kwanini wasiandike kiswahili au wakachanganya zote mbili maana siku hizi wageni ni wengi

    ReplyDelete
  2. Jamani, mungu ibariki tanzania. Sasa mbona hiyo alama yenyewe iko kwenye jengo mbali na barabara. Alama za usalama barabarani si zinatakiwa ziwe wazi na katika barabara na sio majengo. Pia alama ya maandishi makubwa imeandikwa kwa kiingereza, jamani kama dereva haijui hiyo lugha utamlaumuje. mimi sitetei uvunjaji wa sheria, ila naona kuna utata katika hilo suala. Pia hii ya amri ya kutopaki hapo "imeidhinishwa na vyombo vya usalama barabarani" au mwenye jengo kaamua kujiwekea kiholela?

    ReplyDelete
  3. Nimeambiwa siku hizi wenye magari wanaweka hizo lock kuzuia yasiibwe.

    ReplyDelete
  4. Hapo wakikukamata sawa..Sisi tunapigia kelele zile sehemu ambazo hazina alama wala matangazo ya kuzuia kuegesha gari halafu mtu anajibanza pembeni..badala ya kukwambia..samahani eneo hili hauruhusiwi kuegesha gari anajificha,anakuacha unaegesha, unashuka unaondoka yeye anakuja kufunga gari..hiyo si ndiyo mianya ya rushwa na usumbufu jamani.

    David V

    ReplyDelete
  5. Aliyeweka tangazo ana mamlaka gani? Je kuna alama inyojulikana kisheria kuwazuia watu kupark hapo au kila mtu anaandika tu akijisikia? hao wanaofunga magari nao wanaangalia tu hilo tangazo linaloweza kuwa ni la mwenye nyumba tu hapo?

    ReplyDelete
  6. Tangazo hilo nimuendelezo wa upuuzi uleule. Ni alama za barabarani pekee zinazoonesha authority na si matangazo ya kwenye private building.

    Kama eneo haliruhisi kupark ilitakiwa barabara iandikwe kwa kwa maandishi meupe yanayotumika kwenye alama za Pundamilia 'NO PARKING'. Au kuwe ka kibao cha duara chenye P iliyowekewa cross.

    Hapo ukutani maandishi hayo nani ataona?. Ni muendelezo ule ule wa 'Predatory law enforcement', yaani unamfanya mtu asijue kama eneo linakatazwa ili umkamate na kumpiga fine. WIZI wa mchana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...