Salam,
Urban Pulse Creative Inapenda kuwalatea Mahojiano maalum kutoka kwa waziri wetu wa nishati na madini mh William Mgaga Ngeleja wakati alipofanya ziara fupi jijini London. Hii ilikuwa ni fursa pekee ya kuweza kupata majibu sahihi na kujifunza kwa undani zaidi kutoka kwa waziri mwenye dhamana namna ambavyo changamoto mbalimbali zinazozikabili Taifa letu pamoja na wizara ya nishati na madini, vilevile mipango madhubuti ya serikali katika kutoa ufumbuzi endelevu kwa ajili ya kutatua sakata sugu la Umeme nchini Tanzania.
Mahojiano haya yalifanywa na Baraka Baraka kutoka Urban Pulse na yatarushwa rasmi kutoka katika kituo cha STAR TV jumapili hii tarehe 4 Machi 2012 katika kipindi cha Medani za Siasa na Uchumi kuanzia 10.30-11.30. Usikose Kuangalia.
Asanteni,
Urban Pulse Creative


Maojiano yake Baraka maranyingi ni kama anafanya utani. Inabdi awe anajianda ndio uwandishi mzuri, Na pia kama anataka kutumia lugha ya kingereza inabidi atumie lugha hiyo na kama ni kiswahili afanye hivyo pia na siyo kuchanganya hiyo inaonyesha upungufu wake wa lugha zote mbili yani kiswahili na kingereza.
ReplyDeleteHuyu mheshimiwa kazoea kweli kuongea kiswanglish (kiingereza na kiswahili anachanganya mno)
ReplyDeleteNOTHING PERSONAL HERE, KUSEMA UKWELI BARAKA INABIDI UJIANDAE SANA JINSI UNAVYOULIZA MASWALI..YAANI NI KAMA UNA RAP..KUNA KITU UNA MISS,MDAU WA KWANZA AMEELEZA PIA..HUWA NAPENDA KUSIKILIZA MAHOJIANO KAMA HAYA ILA UKIANZA KUULIZA MASWALI TU HAMU YA KUKUSIKILIZA TENA INASHA...KAMA UNATANIA WAKATI HIYO NI KAZI YA KUWA SERIOUS....ANGALIA KWANZA KINA LARRY KING UTAJIFUNZA KITU.
ReplyDeleteSuluhisho la Wizara ya Nishati na Madini juu ya Umeme wa uhakika ni suala la 'MNYAMWEZI ABEBESHWE MZIGO'.
ReplyDeleteUmeme una wenyewe,SWEDEN,NORWAY,CANADA, GERMANY,FRANCE....
Sio WACHINA na WAHINDI!
Muulizaji ana maswali mazuri lkn ka muhuni flani, jinsi anavyoouliza maswali yake!
ReplyDeleteNafikiri maoni yetu yanafanana, jirekebishe Ndg. Baraka!
huyu mwandishi gani jamani?? kama anaamua kutumia kiswahili atumie kama ni kiingereza atumie
ReplyDeletepili...attire...embu vaa vizuri basi...miwani gani ya kuvaa
tatu be serious na kazi sio unafanya utani mwingi kazini
paul andrew