MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, kanda ya Dar es Salaam leo imetoa hukumu ya kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini ya Sh Bilioni 21 kwa washitakiwa wawili Raia wa China waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uvuvi haram katika Bahari ya Hindi ukanda wa Tanzania.

Kesi hiyo iliyokuwa maarufu kama kesi ya samaki wa magufuli leo imefikia tamati baada ya hukumu hiyo iliyotolewa na Jaji Agustino Mwalija ambaye pia aliwaachia huru washitakiwa wengine watatu.

Waliopewa adhabu hiyo ni Nahodha wa meli hiyo ya Tawaliq 1, Hsu Chin Tai kwa mashitaka yote mawili ambayo ilikuwa ni uvuvi haramu wa samaki katika Bahari Kuu ya Tanzania bila kuwa na kibali. Na shitaka la pili akiwa pamoja na wakala, Zhao Hanquing.

Shitaka la pili ni la kuchafua mazingira ya bahari kwa uchafu wa samaki na mafuta ya meli.

Jaji Mwalija ametamka kuwa meli iliyotumika kwa uvuvi huo ambayo inadaiwa kuanza kutitia, serikali iitaifishe.

Mahakama hiyo pia imesema samaki kwasababu serikali iliwagawa bure mahakama hiyo imeridhia.
Mahakama hiyo imesema kuwa nahodha anahusika zaidi kwa mashitaka yote kwasababu anatakiwa kabla ya kuanza uvuvi ajue vibali vyote vimekamilika.

Hata hivyo walipokamatwa walitoa vibali ambavyo vinaonyesha jina tofauti na lililoandikwa kwenye meli na vilikuwa vimeisha muda wake.

Washtakiwa hao wakiwa na wenzao walikamatwa na timu ya doria ya nchi tatu ambazo ni pamoja na Tanzania, Kenya Msumbiji na Afrika Kusini, Machi 8 mwaka 2009 wakiwa na tani zaidi ya 196 za samaki wa aina mbalimbali.

Walioachiwa na mahakama hiyo ni Cai Dong Li, Chen Rui Hai na Hsu Sheng Pao. Wakati wengine 31 waliachiwa mwezi Julai baada ya kukutwa hawana kesi ya kujibu.

Wakili anayewatetea Ibrahim Bendera amesema kuwa hajaridhishwa na uamuzi huo hivyo anataka kukata rufaa ingawa hukumu hiyo imeonyesha furaha kwa mawakili wa serikali kwasababu kwao wanahesabu kama ni ushindi na kuiomba serikali kuongeza ulinzi katika bahari ili kukomesha waharamia kama hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Habari imeandikwa hovyo hovyo, sasa naanza kuwa na hofu juu ya tasnia ya uandishi wa habari nchini.

    ReplyDelete
  2. Duh, wanatia huruma, lakini ndio hivyo tena sheria msumeno.

    ReplyDelete
  3. SERIKALI HAIJAWATENDEA HAKI HAWA JAAA,MBONA EPA ,RICHMOND WAMESHINDWA KUTOA SULUHU?

    ReplyDelete
  4. Safi kabisa, wametuibia sana hawa. Sheria imechukua mkondo wake, tena walicheleweshwa sana.

    ReplyDelete
  5. washitakiwa hao wakiwa na wenzao walikamatwa na timu ya doria ya nchi tatu ambazo ni pamoja na Tanzania, Kenya Msumbiji na Afrika kusini

    siku zote tunapiga kelele za kiswahili kibovu kumbe hata na hesabu pia ni tatizo kwenye blog hii. Unasema nchi tatu halafu unataja nchi nne? au kuna nchi mpya inayoitwa Kenya msumbiji maana umeshindwa kuweka koma baina ya nchi hizo mbili ulizipozitaja.

    ReplyDelete
  6. uonevu huo jamani kweli wamefanya makosa lakini miaka ishirini?

    ReplyDelete
  7. Ni kweli wanastahili adhabu lakini nadhani adhabu ni excessive ukilinganisha na kosa...nadhani miaka 20 ni ku over-do....!! Wapeni miaka mitano na faini...!! Mdau-USA

    ReplyDelete
  8. this is not FAIR OK!

    ReplyDelete
  9. Safi sana..hongera jaji pamoja na mawakili wa serekali...bado maharamia walioko ndani ya govt yetu nao tuwaone mahakamani wakinyeshewa mvua kama hao wachina

    ReplyDelete
  10. Mwenye Meli ndio vipi?

    Je, kwa nini tusiitaifishe Meli yake?

    Hasara waliyotuletea ya wizi kwa muda wote waliokuwa wakituibia samaki wetu tutaifidia vipi?

    SIONI NI KWA SABABU GANI MMILIKI HATAJWI KUHUSIKA WANAFUNGWA NAHODHA NA WAKALA!

    ReplyDelete
  11. Miaka 20 kwa uvuvi kharam na billion za kulipa hii adhabu au ni kuuumizana? kwani wangelipishwa faini wakarudishwa kwao ingekuwaje? Uchafuaji wa mazingira toka lini watanzania tunajali mazingira? hawa watu wana makosa lakini hili si la kufungwa miaka 20 na billlion fain....

    ReplyDelete
  12. 100% confidence levelFebruary 24, 2012

    Jamani mahakama,japo kuwa hawa wachina wamekutwa na makosa ya jinai,hivi huyu mzee mwenye zaidi ya miaka 70 hawezi kufikiriwa kupewa adhabu nyingine zaidi ya kifungo ukilinganisha na umri wake?? Wana haki za binadamu na wanaharakati hamuwezi kushirikiana na mtetezi wao kumnusuru huyu babu ambaye nahisi atafia jera??

    ReplyDelete
  13. miaka 20!! hiyo adhabunikubwa sana nchi za ulaya hiyo miaka20 wanaoukumiwa ni watu wanao waua binadamu wenzao, hata kama hakimu anaonyewsha mfano kwa watu wengine wasiige bado hiyo hukumu siyo ya haki!!!

    ReplyDelete
  14. SAFI SANA!!! Big up TZ!! Hii adhabu ni sawa kabisa nifundisho kwa wengine wote... especially wachina ambao wameingia kwa speed kali sana TZ. Bado wale wasafisha viatu Kariakoo sidhani kama wana WORKPERMIT. WATANZANIA TULINDE MALI ZETU

    ReplyDelete
  15. MIAKA 20! MINGI KWA HAWA WATU LABDA MSAMAA WA RAISI UKIWAPITIA.

    ReplyDelete
  16. La umakini ni kuwa tuangalie Gharama za Magereza kama Mdau Mmoja alitupigia hesabu humu wakati wahamiaji haramu Wahabeshi wanahukumiwa Morogoro.

    Hesabu ilipnyesha mfungwa anaingiza gharama ya Tsh. 3,500/= kwa siku ukiacha anavyozalisha kama atakuwa mfungwa mzalishaji.

    Sasa hapo tupige hesabu kama vifungo vyetu ni siku 1 kwa 2 ina maana jumla ya kifungo ni miaka 10

    Hivyo:

    Tshs.3,500 X 10 X 365=Tshs.12,775,000/=

    Hivyo Wajameni Gharama ya Dona letu na Maharage kwa kodi tutakayolipa Wachina kufungwa kwetu ni Tsh. 12,775,000/=

    Ahhh, ili iweze kurudisha gharama itabidi tuwabebeshe zege kwenye Miradi ya Ujenzi kama Daraja la Kigamboni Kuvunja kokoto na Kuchana Mbao KALIUWA-TABORA!

    ReplyDelete
  17. Adhabu jamani iwe na uwiano na umri wa mtu.Sasa mtu wa miaka 70 afungwe miaka 20 ndo kitu gani halafu sisi tunafaidi nini na kifungo hiki.

    Tuchukue fedha maana itaongeza pato la taifa,na tuchukue meli maaana nayo tutauza serikali ipate fedha kufidia hasara waliyotutia kwa kuchukua samaki wetu siku zote.

    Badala ya kifungo cha miaka yote hiyo tuwarudishe kwao bila faida.Au twafundishe adabu miaka mim 3 waende zao.

    ReplyDelete
  18. Hiyo ni danganya toto. Hawa watakaa jela miezi michache halafu tutasikia wamerudishwa kwao kumalizia vifungo vyao. Changa la macho hilo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...