TAARIFA ILIYOIFIKIWA GLOBU YA JAMII HIVI PUNDE,INAELEZA KUWA MELI YA MV. MAENDELEO INAYOFANYA SAFARI ZAKE KATI YA UNGUJA NA PEMBA IMEKWAMA ASUBUHI HII NJE KIDOGO YA BANDARI YA PEMBA (MITA KAMA 180) WAKATI IKIJIANDAA KUPAKI KATIKA BANDARI YA PEMBA ILI ABIRIA WALIOPO NDANI YA MELI HIYO WAWEZE KUSHUKA.

KWA MUJIBU WA NAHODHA WA MELI HIYO NA MDAU AMBAYE YUPO NDANI YA MELI HIYO ANAELEZA KUWA CHANZO CHA KUKWAMA KWA MELI HIYO NI KUTOKANA NA BOYA ZINAZOKUWEPO KWENYE BANDARI HIYO KWA AJILI YA KUELEKEZA MELI SEHEMU YA KUPITA ILI KWENDA KUPAKI,ZILIKUWA ZIMEHAMA KATIKA MAENEO YAKE KUTOKANA NA UPEPO MKALI ULIOZISUKUMA KUTIKA ENEO HILO NA KUPELEKWA ENEO LINGINE.

MPAKA SASA HAKUNA MADHARA YEYOTE TOKEA,KWANI TARATIBU ZA KUINASUA MELI HIYO MAHALI HAPO INAENDELEA HIVI SASA,HUKU ABIRIA WOTE WAKIWA BADO HAWAJASHUMA MELINI HUMO.

GLOBU YA JAMII INAENDELEA KUFUATILIA KWA MAKINI TUKIO HILO NA TUTAENDELEA KUPEANA TAARIFA KADRI ZITAKAVYOKUWA ZIKITUFIKIA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. siku Hizi GPS ya mkononi inpatikana kwa US dollar 200... Hata simu nyingi zinazo GPS.. Kama shirika halija invest kwenye kitukidogo namna hio kinachoweza kusaidia kiongozi wake haiwezi kazi

    ReplyDelete
  2. JAMANI TANZANIA,TUNAWAOMBEA ABIRIA WAFIKE SALAMA TUU,TUMECHOKA NA MAAFA YA HIZI MELI.

    ReplyDelete
  3. Ni aibu sana kwa kapteni wa Meli, pengine alikuwa kalala. Njia ya kuingiza meli Bandari ya mkoani, ila land marks kibao ambazo hazihitaji kampasi au GPS, hata usiku wa manane wenye giza kubwa unaweza kuigiza meli! Shame on us
    Muathirika wa MV Spice Islander!!

    ReplyDelete
  4. Sasa yule Mtaliana aliyekwamisha meli ya kitalii hapo kwao Italia alikuwa na kila kifaa cha GPS. GPS haionyeshi kina cha maji!!

    ReplyDelete
  5. Tatizo kubwa ktk mambo mengi yanayopelekea Ajali na mambo kuharibika ni UBAHILI na RUSHWA!.

    Hebu angalia mtua anamiliki Meli ya thamani ya mamilioni ya Shilingi halafu anashindwa kuweka System makini ya kusimamia mwenendo wa Chombo(UBAHILI),,,huku akitumia fedha kuendesha Biashara kinyume na Kanuni na Taratibu(RUSHWA).

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...