Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wazee wa Dar es salaam leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee hall jijini Dar. Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo Mh Saidi Meck Sadick na shoto ni Mwenyekiti wa Wazee wa Dar es salaam Mh Iddi Simba
Sehemu ya maelfu ya wazee wa Dar es salaam waliojitokeza kumsikiliza Rais Kikwete leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Mimi nadhanii JK aanze sasa kuongea na waandishi wa habari, wachumi, na vijana wa dar es salaam. Kisha atoe nafasi ya mwaswali na majibu ili isiwe oneway, badala yake kuwe na dialogue. kwa njia hiyo atakuwe kweli "amezungumza na taifa" na kupata mawazo mapya.

    ReplyDelete
  2. Mimi nadhani JK sasa aanze kuongea na waandishi wa habari, wachumi na vijana wa nchi hii na kuwe na nafasi ya kuuliza maswali. Namna hiyo, itakuwa sio "oneway" ila itakuwa dialogue, itakuwa mazungumzo. Pia kutakuwa na nafasi zaidi ya kupata mawazo mapya.

    ReplyDelete
  3. Nakubaliana na mchangiaji wa kwanza, kwa maoni yangu naona kama hii platform siyo sahihi kwa issues zinazopelekwa mbele yake. Hao wazee wanauliza hata maswali kweli? Wanatoa maoni yao? Au wanaishia kuwa wasikilizaji tu?

    ReplyDelete
  4. Bw. Mjengwa aliuliza kupitia blog hii kwamba wazee wa DSM ni nani? nadhani baada ya mkutano huu jibu amelipata kwamba ni wazee wastaafu wa TANU na CCM ingawa walikaribishwa pia viongozi wa dini. Ushahidi wa wazi ni kuwepo na mwenyekiti wa CCM wa DSM bila wenyeviti wa vyama vingine kukaribishwa. Jambo linalofuata ni viongozi wa "wazee wa DSM" wanapatikana namna gani maana sikuwahi kusikia uchaguzi uliompa uongozi Bw. Idd Simba. Pia naona vijana wadogo wenye umri chini ya miaka 40 ambao bila shaka walikuja kuongeza ushangiliaji. Kwa hali hii nadhani tafsiri ya wazee bado haijajulikana.

    ReplyDelete
  5. kweli nakubaliana na wadao hapo juu. its time J.K aonane na vijana ambao ndiyo tunawategemea kujenga nchi yetu. Senior citizen wamekwisha contribute wapumzike. Changamoto la mawazo na senior citizen liko kwenye ngazi tofauti na vijana wanaotafuta ajira au kuendeleza maisha yao.

    ReplyDelete
  6. Hebu jamani tuache kuwa na akili mbovu, yaani vichwa maji. JK alizungumza na wazee wa Dar es Salaam na sio wa mkoa mwingine wowote. Sasa ukiangalia historia ya Dar es Salaam kisiasa hapo zamani unategemea kukutana na wazee wa itikadi gani kisiasa? Hili Kwa maana hihyo hili suala la sijui aliokutana nao ni wanaCCM ni hoja ya kipuuzi. Wazee aliokutana nao ni wa Dar es Salaam na wala sio wa Kilimanjaro ambao historia inatueleza kuwa wengi wao (sio wote) walikataa hata kupingana na mkoloni wakati wa mapambanomo ya kudai uhuru!
    Kuhusu kukutana na waandishi wa habari kwanza hii nayo inatia shaka mbona mlikubaliana na 'subjectivity' ya akina Mkopi na 'ndugu' Ulimboka na mkaripoti kufuatana na maoni yao bila hoja yoyote? Sasa nyinyi mlikuwa na lipi? Au ni waandishi wa aina ya Samsom Mwigamba ambaye ni Mwenyekiti wa Chama fulani cha siasa katika ngazi ya mkoa? je ukikutana na waandishi wa aina hii ndio wa kuhoji ndio amani itapatikana kweli hapo, si watakuwa na mawazo sawa na akina Ananilea Nkya au Helen Kijo Bisimba? Let's be objective please, JK katoa kilichokuwepo, vinginevyo labda tuombe press conference.

    ReplyDelete
  7. Na wala tafsiri ya ni nani hasa wazee wa Dar HAITOPATIKANA KAMWE.
    Kila mmoja ataielewa tafsiri hiyo kulingana na mtazamo wake wa kimaslahi

    ReplyDelete
  8. Hivi nchi hii wazee wapo Dar es salaam tu?
    kwa nini asiongee na watu wa caliber tofauti tofauti ili apate mawazo mapya? maana naona pia jana aliwaponda wanaharakati sijaelewa alitumia mantiki ipi.
    halafu wazee wanatofautiana mitazamo na uelewa siku moja ingekuwa vizuri kama angeongea na wazee wa Mbeya, Moshi, Mwanza na arusha anaweza akarudi na mawazo mapya.
    afanye dialogue kupata feelings za wananchi si kuhubiri kama mchungaji

    huu mfumo unabagua wazee wa mikoa mingine.

    ReplyDelete
  9. NIMECHUNGUZA KWA MAKINI NIMEGUNDUA KUWA NJAA INATESA WATU SANA

    JIJI LA DAR LIMEJAA WATU WA MAKABILA MENGI SANA KUNA WARABU NA WAHINDI WENGI SANA

    WAZEE WA KIHINDI NA WARABU NI WENGI SANA LAKINI HUTOWAONA SEHEMU KAMA HIZO

    KUTOKANA NA KUWA HAWANA NJAA NA NDIO MAANA HATA SIKU ZA KUPIGA KURA HUWEZI KUWAONA WANAPANGA MISTARI KUPIGA KURA

    AU WACHONGA VINYWA MTASEMA HAO SIO WATANZANIA? WATU WANAZEEKA WANA WATOTO NA VIJUKUU WALIOZALIWA TANZANIA

    LAKINI KUTOKANA WAMEGUNDUA KUWA SIASA YA BONGO NI NJAA TUPU HAKUNA AHADI ITAKAYOTEKELEZWA NDIO WAKAONA NI BORA WATULIE MAKWAO TU

    SASA HAO WAZEE WALIOFIKA HAPO HIVI KWELI WATAKUWA NA MASWALI GANI KWA MHESHIMIWA RAISI?

    HAWANA MASWALI ZAIDI YA KULALAMIKA NJAA INAZIDI NA BADAE WATAPATIWA KILO ZA SUKARI NA KHANGA FULL STOP.

    WATANZANIA TUBADILIKE VIONGOZI TUNAOMBA MUACHE UFISADI MTUFIKIRIE NASISI TUNAOPATA MISHAHARA YA ELFU 80 HAPO KUNA KULA KULIPA KODI KUSOMESHA WATOTO MWE!

    ReplyDelete
  10. Ni kweli kunahitajika uwazi wa viongozi na tafsiri ya wazee ila uwepo wa vijana si tatizo kama wameingia kihalali kama wasindikizaji. Kumbuka wazee wengine wanahitaji msaada kutokana na kutokuona vizrui au kutembea kwa matatizo, kama umeshawahi kuishi wa watu wa aina hii au kuwaona utanielewa.

    SeAtka

    ReplyDelete
  11. Waandishi tofautisheni "kuzungumza" na "kuhutubia". JL alikuwa anahutubia na si kuzungumza au kuongea na wazee hao!

    ReplyDelete
  12. Nyie jamaa wote mliotoa maoni ya kwamba Rais aongee na waandishi wa habari, wachumi, na vijana wa Dar es salaam. Waandishi wenyewe bure-waoga au ni chama kile kile. Labda vijana wanaweza kusema kero zao,kwani vijana wameshoka, hamna kazi wala mwelekeo. Wengine wote mnaowasema hata wakiwa na ujasiri wa kutoa maoni yao wanawekwa jela au kama unavyojua, wanazushiwa kesi za uongo.

    ReplyDelete
  13. How often anaongea na hao wazee kama vile juzijuzi tu aliongea nao na je wanampya gani zaidi ya kudai pension zao za miaka illlleeeeee.
    Mi nadhani aongee na vijana pia kwani wana mengi na ndo taifa la kesho hili taifa la jana tuliache kwanza

    ReplyDelete
  14. Nafikiri ukitulia utaona Jk anafanyakazi vyema sana, na anatumia busara na hekima kabla ya kuamua jambo ijapo una mapungufu ya kutofanya maamuzi haraka au kutofanya kabisa hasa yale magumu. Pili kinacho mwangusha ni wasaidizi wake, wakiwa wanatatua mapema matatizo yasingefika kwake kwaajili ya maamuzi, hivyo ni ushahidi tosha kwa yeye kuwawajibisha.

    Tanzania tuna kawaida ya kulalamikia tulipo angukia bila kutazama kilicho sababisha kuanguka, wito umetolewa kuwa madaktari wasigome tena (nakubaliana nao) lakini hatua zipi ZA WAZI KABISA zitachukuliwa kwa wale wote waliosababisha madaktari kugoma na maisha ya watu kupotea?

    Kibanga Msese

    ReplyDelete
  15. Hii Dar es Salaam ina wenyewe, sio wakuja wanangu. Nenda New York pale huwezi kufanya lolote bila kuwatambua wazee wa pale, unawajua ni nani? Kila siku huwa nasema someni mambo mujue, fanyeni utafiti katika mtandao. Usije kuwa umetoka kijijini umekwenda shule Dar es Salaam, basi umeshakuwa mji wako, huu mji una wenyewe. Usione watu wanakwenda na kurudi.

    Kwendeni huko mnapayuka ovyo tu nini kwa sababu mnataka utajiri wa harakaharaka. Mtauwa wazee wenu ili mrithi mapema ndio nyinyi. Eti kwa sababu umesoma miaka 5 bull shit mnasupp masomo yote halafu unataka usiitwe daktari mwanafunzi. Hata ukiwa una miaka 35 wewe ni mzee tayari, unafikiri una ujana gani. Mradi ukiukubali uzee basi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...