![]() |
Lutengano Mwakispile "LUTE" ni msanii mchoraji na Graphic Designer ambaye zamani alitamba sana kwa ustadi wake pale Nyumba ya Sanaa jijini Dar es salaam. Leo ametutumia kazi zake za sanaa alizochora yeye mwenyewe moja ikionyesha mama anavyonyanyaswa na mumewe {anapigwa} na nyingine baba anamsaidia mama kazi ya kupika {upendo kw mama} ikiwa ni mchango wake katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani siku ya Alhamisi Machi 8, 2012 |
Home
Unlabelled
mchango wa mchoraji LUTE katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
mwenye kibalaghashee ni mgomvi na asiye na kibalaghashee ni mwerevu. ujumbe wako umefika kijana.
ReplyDeleteHizi picha ni nzuri mno. Hongera sana.
ReplyDeleteHivi waliovaa barghashiya ndio wapigaji hapa Tanzania, sio watu fulani Wewe ulikaa lini jikoni kusonga ugari, Hali hii haiko ulaya sikwambii Afrika. Mimi ni Mwanamke na nimefanya kazi miaka mingi na natunza Mume na watoto, na wote wamefanikiwa, Mwanamke bado jukumu lake la kifamilia hawezi kuliacha hata akiwa mke wa rais, bado ana jukumu la kumwangalia mume, nyumba yake na watoto.
ReplyDeleteThey said "one picture thousand words"
ReplyDeleteMimi sidhani kama ktk hiyo picha ya kwanza huyo baba anamtandika mama; mkononi kakamata kitu kama gazeti; na huyo mama kajikunja kama anayakata mayenu! na kama unabisha angalia mabega ya baba alivyopandisha juu kama vile na yeye pia anayarudi mayenu! inavyoelekea tu dogo hao hawajafurahia huo mziki labda wao vijana wa leo walitaka zile za kufokafoka!
picha nzuri mno mno ongera sana
ReplyDeleteMsanii anatoa taswira ya Uchochezi wa Kiimani na Ki Utamaduni ,Mila na Jadi za pia kupindisha utaratibu wa Maisha kwa misingi ya Uafrika!
ReplyDelete1.Picha ya kwanza juu Msanii anaashiria uchochezi wa Kiimani dhidi ya kundi fualni kuwa wao ndio wasiowatendea haki Wanawake kitu ambacho sio kweli.
2.Picha ya pili ndio ni wajibu kusaidiana na Mke ktk shughuli ikiwemo majukumu ya nyumbani lakini inapobidi kwa vile Jamii yetu ya Kiafrika imepanga Mwanaume kuwa mtafutaji na Mwanamke majukumu ya familia ikiwemo kupika,,,hivyo kwa mpangilio huo nilioutoa hapo juu, atakae fanya hivyo bila sababu zinazobidi mara zote sehemu nyingi huitwa MUME BWEGE!