
Tume inachukua fursa hii kuuarifu umma kwamba chuo hiki hakitambuliki kwa mujibu wa sheria na kwamba wamiliki wa Japan Bible Institute Graduate School of Theology hawana kibali cha kutoa elimu ya chuo kikuu ambayo inatambuliwa hapa nchini. Tume inatoa tahadhari kwa umma kuepuka ulaghai ambao unafanywa na watu katika eneo hili la elimu ya juu na hivyo umma unashauriwa kuchukua tahadhari kwani vyeti watakavyotolewa havitambuliwi na Tume na hivyo haviwezi kutumika hapa nchini.
Pia, wamiliki wa chuo hiki na wawakilishi wake waliopo Tanzania wanapewa onyo kuacha mara moja kutoa matangazo ya shahada za aina hiyo hapa nchini bila kufuata taratibu. Hatua za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakaye kwenda kinyume na tangazo hili.
Aidha, Tume inapenda kuwaarifu watu wote wenye lengo la kuanzisha vyuo vikuu nchini au kutoa programu za vyuo vikuu wawasiliane na Tume ili kupata maelekezo juu ya taratibu zinazotakiwa kufuatwa. Pia umma unasahauriwa kutoa taarifa kwa Tume ama vyombo vingine vya dola pale ambapo wana wasiwasi na uhali wa programu ama tuzo inayotangazwa au kutolewa na taasisi yoyote bila kufuata taratibu.
Imetolewa na:
Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
S.L.P. 6562
DAR ES SALAAM
dini hapa ni kivuli cha ulaji, wameelewa somo la wakoloni. nao pia dini ilikuwa ulaji, ila sisi imetudaka vizuri.
ReplyDeletePHD za akila Dr. Slaa
ReplyDeleteHii yote ni Njia ya Mkatao ambayo Wanasiasa wengi Dunia nzima hupendelea sana mipango ya namna hii ili kufikia Malengo ya viwango vya Elimu kwa njia fupi.
ReplyDeleteDaima Mwanasiasa Duniani ni mtu mpenda kufikia malengo kwa njia ya mkato!
Upigaji umezidi sana Bongo, kila kukicha na mabunduki mapya ya kiusanii.
ReplyDeleteMamlaka zimelala usingizi wa kukoroma.
Ohhh yetu macho!
Marekani wanahangaika kusambaza uongo kwa aina yeyote ile. Hapa Afrika wanajua wala hamjui kudhibiti utitiri wa makanisa na vyuo vinavyoibuka kila kukicha. Vichochoro hivyo ndivyo vinavyotumiwa kuparaganya amani ya nchi. Watanzania wenye uchu wa elimu wanaingia kichwa kichwa.
ReplyDeleteHili ni tatizo kubwa nchini watu kubeba shahada feki na wakapewa misifa.
ReplyDeleteTume ya Vyuo vikuu ianze pia kuwashughulikia wale waliotajwa na kufahamika kuwa wana PhD za kubumba tunawafahamunhata wakijinyamazia leo. Ipo siku atakuja mtawala asiyeangilia nyani usoni mtaumbuka kwa kutakiwa kulipa fedha na hadhi yote mliyopewa ambayo hamkustahili kwa ajili ya kuonyesha vyeti feki!!!
Wachungaji na Maaskofu kuweni macho msiingie mkenge na hicho chuo cha Uongo na kweli wala msisogee katika mahafali yake!!