Ndugu zangu ambao ni mashabiki wangu!!

Juzi wakati nimerejea kutoka Tanga, majira ya jioni ndugu zangu Ballet Wallet(mtupori) , Adam Lumbe na Twenty Percent (20%) walitoka na gari yangu, kwa bahati nzuri au mbaya wakapita maeneo ya NMB hapa Morogoro, wakapaki gari kwa haraka kwa kuwa Adam Lumbe alimuona kijana ambae alimtapeli katika mauziano ya pikipiki, likatokea zogo!!

Polisi waliokuwa Lindo pale Bank wakaja kuizuia gari na pia wakawaweka chini ya Ulinzi Ballet Wallet na Adam Lumbe, licha ya maelezo waliyowapa hawakuwaelewa, 20% akataka kuchukua gari wakamkatalia, ikabidi akodi pikipiki aje nyumbani kunifuata nikafuate gari, nimefika pale Bank polisi wakakataa kunipa gari ili niende kituo kikubwa cha polisi kuwawekea dhamana ndugu zangu kwa kuwa muda huo Ballet na Adam walikua washapelekwa kituoni.

Kilichotokea baada ya hapo nilielezwa nisubiri gari ya doria nipewe Eskoti mpaka polisi lakini baada ya kufika gari ya doria wakiwa na wanamgambo wa manispaa walituvamia na kuanza kutupiga marungu na kutujerehi, wananchi ambao ni kama ndugu zangu wanamorogoro wakasogea eneo la tukio.

Polisi wakafyatua risasi hewani kuwasambaratisha tukapelekwa Polisi kituoni, pale hatukuchukuliwa maelezo haraka, baadae tukatoa maelezo baada ya wale mabwana wadogo askari kupata amri toka kwa wakubwa wao!! Jana (juzi) tukafikishwa mahakamani tukakosa dhamana, tukapelekwa ngome (jail) tukiwa kama mahabusu, leo  (jana) kwa bahati nzuri tumepata dhamana, na tumeweka wanasheria makini kusimamia HAKI yetu.

Si kweli hata kidogo kuwa kwenye gari yangu kulikua na silaha za kijadi kwa lengo la kumdhuru mtu, walikuta fimbo yangu ile ya Mfalme wa rhyemes na kisu au kama panga ambao ni kitu cha kawaida kuwa nacho kwenye gari, na si kweli hata kidogo kuwa Ballet alikua kavaa kic..p* tu.

Ndugu zangu wapendwa watanzania wenzangu,na mashabiki wetu kiukweli hali za jela na selo zetu ni mbaya mazingira mabovu ndugu zetu wanateseka. Nilitumia muda mchache niliokua kuwa kule kuwafariji na kuwapa moyo ingawa nilienda kwa Matatizo, na muda huu nipo hapa Nyumbani Misufini na Twenty Percent na Ballet pamoja na ndugu wengine!

Tumechinja Mbuzi kama Sadaka au dhabihu kwa Mungu na kuchoma, kuelekeza moshi kwake kama ishara ya kumpenda na kushukuru kwa yote!! mwisho tunaomba radhi kwa mashabiki wetu wote kwa usumbufu mulioupata.

ASANTENI KWA FARAJA ZENU KWANGU WAKATI WOTE ,Ni mimi

SELEMANI ABDALLAH JUMA MUTABHAZI MSINDI .. KING OF RHYEMEZ. (AFANDE SELE).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Sasa wewe afande unataka kule selli kuwe kuzuri itapelekea kila mtu kuwa mhalifu ili apelekwe maisha uraiani magumu!!!jail sio club sawa wacha watie akili wakitoka adabu Kama wewe hutochezea tena nguvu ya dola.

    ReplyDelete
  2. Na wewe afande kwa kupenda kuelekeza moshi huko juu hehehe wewe moshi tuuuu...!

    ReplyDelete
  3. Duu Bongo noma sana,na Moro kumekuwa kwa ovyo ovyo sana hakuna mpango.Wajanja wote walishaama Moro hamna muelekeo na wale wajanja zaidi walishahama Tanzania,hamna mpango huko hamna hali kabisa rushwa tu.

    ReplyDelete
  4. Sasa we Afande Sele,jaribu kutia akili nchi inaongozwa na sheria,mara nyingi wasanii wetu mkipata umaarufu tu mnataka kujichukulia sheria mkononi,pamoja na hayo maahala palipotokea zogo ni karibu na benki,zogo lenu lingesababisha fedha za wananchi zitekwe,acha mkondo wa sheria ufanye kazi yake,kaa kimya,kama maisha yako ya kawaida unashindwa kuyaongoza! ndio ubunge utauweza?

    ReplyDelete
  5. wewe afande si rasta, na unakula nyama? ama rasta koko?

    ReplyDelete
  6. Moshi unafuka kutokana na kuungua Majani,

    Pia Majani ni Dawa,,,isipokuwa Utafiti wa Kisayansi unathibitisha kuwa 'Sigara kubwa' inayotoa moshi mzito ina ukomo wake kulingana na maumbile ya mtu na umri wa mvutaji.

    Kama kanuni hii isipozingatiwa, ndio pale unakuta mtu anazimikaaa au anakata pumzi ghafla halafu (inawezekana) ikawa ndio kimoja au akazinduka tena !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...