Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa taarifa ya kifo cha Msanii wa filamu Steven Charles Kanumba kilichotokea usiku wa kuamkia leo Jumamosi ya Tarehe 07/04/2012 baada ya kuanguka ghafla akiwa nyumbani kwake Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.

BASATA inaungana na familia za wafiwa na wasanii wote nchini kwa maombolezo ya msiba huu mkubwa na wa kihistoria. Kufiwa na msanii huyu mahili kwenye tasnia ya filamu ni pengo kubwa kwa familia, Sekta ya sanaa na Taifa kwa ujumla kutokana na ukweli kuwa, aliweza kuutangaza utamaduni na sanaa yetu nje ya mipaka.

Kanumba atakumbukwa kwa moyo wake wa kujituma na kuthamini kazi ya Sanaa toka akiwa Kundi la Maigizo la Kaole ambapo moyo wake huo ulimfanya awe miongoni mwa wasanii walioleta mageuzi kwenye tasnia ya filamu kwa kuifanya kuanza kupendwa na wadau wengi zaidi.

Aidha, atakumbukwa kwa juhudi zake za kuinua vipaji vichanga katika tasnia ya filamu ambapo mara kadhaa katika kazi alizoziandaa alishirikisha wasanii wachanga ambao BASATA inaamini watakuja kuwa hazina kubwa kwa taifa letu.

BASATA linatoa pole kwa familia ya marehemu na Wasanii wote katika kipindi hiki kigumu. Ni vema wasanii wote tukatumia kipindi hiki kutathimini kwa pamoja michango yetu katika kukuza sekta ya Sanaa ikiwa ni pamoja na kuimarisha umoja wetu lakini pia tukiyaenzi yale yote mema yaliyofanywa na Steven Charles Kanumba.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Steven Charles Kanumba mahali pema peponi. AMEN

Sanaa ni Kazi Kwa Pamoja Tuikuze na Kuithamini.

Ghonche Materego

KATIBU MTENDAJI, BASATA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. mungu amlaze pema.amin haya je lilu ndio amemsukuma kweli au publish tu?aama kweli majuto mjukuu!!!Poleni sana wafiwa kwa kkuondokewa na pengo lisilozibika

    ReplyDelete
  2. Hivi ni kweli????????
    I can't believe this. Inahuzunisha sana sana. Maisha kwa kweli mafupi hatujui saa yetu.
    MUNGU AIWEKE ROHO YAKE PEMA PEPONI AMEN!

    ReplyDelete
  3. This is soooo shocking. ingawa sikumjua kanumba kabisa mbali ya kuwa mfuatiliaji wa habari zake tu, hata juzi tu nilikuwa naangalia mahojiano yake na kipindi cha Mkasi cha Salama Jabirr lakini bado nipo shocked. Kweli hujafa hujaumbika. Mungu amlaze pahala pema peponi. Yaani Mungu kweli yupo.

    ReplyDelete
  4. RIP Kanumba jamani hooooo!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. Iam so sad to hear this, Mola akulaze pema peponi Kanumba. May god be with your family in this hard time. Rest in Peace brother.

    ReplyDelete
  6. If We Really Love Kanumba we Would B praying that Allah Atamlaza Pahali AnapoStahik Kulazwa and not Talk About His Past And what his Career Was Because His Punishment in the Grave Will Start Before He Enters the Grave iF We Don't Mention The Good Things Then let's Not Say Anything At All . Allahu Akbar :'( :'( O:)

    ReplyDelete
  7. Pole wa familia na marafiki zake Steve Kanumba. Mungu amlaze pema peponi. Amina

    ReplyDelete
  8. Ni wakati wa kutulia na kusubiri ripoti ya daktari na polisi si wakati wa kumuhukumu lulu

    ReplyDelete
  9. hii habari naona kama naota vile i can belive this yaani nimekuwa fan wa yuhu kijana kwa muda mrefu japo sijawahi kumwana kwa macho lakini blog yake kila siku lazima nipitie hata zaidi ya mara mbili kwa kwa siku hiyohiyo jana nikuwanasoma blog yake na maneno yake ambayo haachagi kumtaja Mungu ambayo ni nzuri sana yaani huyu kija sijuii hataniseme nini maana nimepata mshtuko kama vile ni mtu wangu wa karibu nimeumia sana tu siwezikuelezea maana haielezeki sipati picha kwa wazazi wake inakuwaje na ndugu na marafiki wa karibu yake na wanafilm wenzake huyu kijana alikuwa tu anaonekana hataishi kwa mudu mrefu kwa jinsi alivyokuwa na roha nzuri alikuwa mtu wawatu hanakinyogo anapenda kumtaja Muumba wake kila wakati jana nilikuwa nasoma baadhi ya blog nikakutana hii habari hakaki sikuweza kuamini nikajiuliza leo ni siku ya wajinga duniani?lakini nikasema hata kama nisiku ya wajinga hawawezikumtamkia mtu kifo sikuami haraka nikaja ktk blog ya dada mange nikaamini kidogo jana lakini nikawa mashaka kidogo sasa nikaja ktk blog ya jamii ndio naaamini sasa kweli maisha ya minadamu ni mafupi sana laiti huyu kija kama amepata muda wa kutubu makosa yake mungu amuweke pema peponi sisi tulimpenda lakini mungu alimpenda zaidi pole sana familia ya marehemu najua kwa kiasi gani mmeumia hasa ukizingatia kijana hajaugua loh! inatisha kwelikweli

    ReplyDelete
  10. Unajua inahuzunisha sana kwa mtu unayempenda na kumkubali.
    Nilimkubali sana K, uncle JJ...movie zake ukiangalia zinasisimua utafikiri hafanyi acting,ni kama real life. Nilitamani ni act nae ila ndo hivyo Mungu kampenda zaidi ya nilivyom-maindi.

    Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake libarikiwe.
    By
    John Ben Zom

    ReplyDelete
  11. This is unbelieveable but kwakuwa ni ukweli basi hakuna kipingamizi,(very hurtful my dia kanumba)
    =WE LOVED YOU BUT GOD LOVED YOU MORE,REST IN PEACE.
    Amen!

    ReplyDelete
  12. Kwa kweli Watanzania na Wapenzi wote wa Filamu tumeumizwa sana sana na habari za kifo cha ghafla cha mpendwa wetu Steve Kanumba!How could this happen?How could we know it would happen so untimely!Kweli tumeumia rohoni,lakini tayari limetokea hatuna cha kufanya.Mungu bado anatukumbusha tena kwamba Yeye ndiye Muweza,ndiye Muumba,na yeye ndiye mwisho wa yote!Siri yote amekwenda nayo yeye mwenyewe Steven Kanumba!Ameacha kovu kubwa katika Tasnia ya Uigizaji Filamu.He started from Nothing,from Scratch,but with tremendous determination and commitment he succeeded where a lot others failed! Ameonyesha njia,ameacha mfano wa kuigwa na vijana wetu wote nchini na kote alikojulikana!Siwezi kuyamaliza niliyo nayo moyoni, Rambirambi na Pole sana ziwafikie ndugu,marafiki na Familia ya Kanumba!Ndivyo alivyopanga Mwenyezi Mungu,sisi sote ni Waja Wake,hakuna mwenye uwezo wa kuyazuia haya,nasi sote tuko njiani!Tuyaenzi yote mema aliyotufundisha Steven Kanumba kupitia uigizaji wake katika filamu!Tuyaendeleze zaidi na zaidi!Na tusichoke kuchukua tahadhari zaidi katika maisha yetu ya kila siku.Kila kitu kiwe kwa Wastani na huku tukimshukuru Mungu kwa mema yote,Amina.Hatutakusahau Kanumba!

    ReplyDelete
  13. Que descanse en paz- Apumzike kwa amani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...