HABARI TULIZOPATA USIKU WA KUAMKIA LEO NA KUTJHIBITISHWA ASUBUHI HII NI KWAMBA MWIGIZAJI MAARUFU NCHINI STEVE KANUMBA (PICHANI) AMEFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA LEO HUKO NYUMBANI KWAKE SINZA 'VATICAN' JIJINI DAR ES SALAAM.
HABARI ZA AWALI AMBAZO HAZIJATHIBITISHWA ZINASEMA UMAUTI UMEMKUTA MAREHEMU KANUMBA BAADA YA KUTOKEA TAFRANI KATI YAKE NA MWANDANI WAKE WAKIWA WANAJIANDAA KUTOKA KWENDA OUT MILANGO YA SAA SABA USIKU. KATIKA PURUKUSHANI HIO MAREHEMU ALIGOTA UKUTA NA KUZIRAI BAADA YA KUUMIA KISOGONI.
HABARI ZAIDI ZITAFUATA BAADA YA KUTHIBITISHA KILA KITU. MSIBA UPO NYUMBANI KWA MAREHEMU SINZA 'VATICAN' AMBAKO NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WAMEKUSANYIKA HIVI SASA
KUJIANDAA NA MIPANGO YA MAZISHI. MWILI WA MAREHEMU UKO HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI.
MOLA AIWEKE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU - AMINA.
GLOBU YA JAMII IMEPOKEA HABARI HIZI KWA MSTUKO NA MAJONZI YASIYOSEMEKA, IKIZINGATIA KWAMBA TAKRIBAN MASAA 48 YALIYOPITA TULIRUSHA MAHOJIANO YETU YA MWAKA 2009 BAADA YA KUREJEA KUTOKA BIG BROTHER AFRIKA YA KUSINI. NA PIA ALIKUWA RAFIKI WA KARIBU WA ANKAL AMBAYE INAMUIA VIGUMU KUAMINI KWAMBA HATUNAYE TENA.
Kupata mengi ya Marehemu
Kanumba tembelea Libeneke lake
BOFYA HAPA
HABARI ZA AWALI AMBAZO HAZIJATHIBITISHWA ZINASEMA UMAUTI UMEMKUTA MAREHEMU KANUMBA BAADA YA KUTOKEA TAFRANI KATI YAKE NA MWANDANI WAKE WAKIWA WANAJIANDAA KUTOKA KWENDA OUT MILANGO YA SAA SABA USIKU. KATIKA PURUKUSHANI HIO MAREHEMU ALIGOTA UKUTA NA KUZIRAI BAADA YA KUUMIA KISOGONI.
HABARI ZAIDI ZITAFUATA BAADA YA KUTHIBITISHA KILA KITU. MSIBA UPO NYUMBANI KWA MAREHEMU SINZA 'VATICAN' AMBAKO NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WAMEKUSANYIKA HIVI SASA
KUJIANDAA NA MIPANGO YA MAZISHI. MWILI WA MAREHEMU UKO HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI.
MOLA AIWEKE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU - AMINA.
GLOBU YA JAMII IMEPOKEA HABARI HIZI KWA MSTUKO NA MAJONZI YASIYOSEMEKA, IKIZINGATIA KWAMBA TAKRIBAN MASAA 48 YALIYOPITA TULIRUSHA MAHOJIANO YETU YA MWAKA 2009 BAADA YA KUREJEA KUTOKA BIG BROTHER AFRIKA YA KUSINI. NA PIA ALIKUWA RAFIKI WA KARIBU WA ANKAL AMBAYE INAMUIA VIGUMU KUAMINI KWAMBA HATUNAYE TENA.
Kupata mengi ya Marehemu
Kanumba tembelea Libeneke lake
BOFYA HAPA
Inaumiza sana nafsi kusikia kifo cha Kanumba na pia ni ngumu sana kuamini kirahisi. lakini kazi ya Mungu haina makosa Mungu atupe faraja katika kipindi hiki kigumu.
ReplyDeleteKwa kweli usingizi umekata wote hii taharifa imenistua sana! Umri ulikua bado unaruhusu ila Mwenyezi kampenda zaidi. Marehemu Steven Charles Kanumba alazwe pahala pema peponi.
ReplyDeleteUlale Mahali Pema peponi Kanumba.Amina.Tulikupenda lakini Mwenyezi Mungu amekupenda zaidi!
ReplyDeleteNi mtu muhimu kwa taifa lakini alipangalo mola binadamu hatuwezi lipangua ,but pengo lake ni kubwa kwa tasnia ya filamu bongn even east africa. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi amen.
ReplyDeletePoleni sana kwa Familia ya Steven Kanumba...Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
ReplyDelete/Mdau Vumbi Dekula
Kifo cha Kanumba na vifo vingine vyote, ndugu zangu tunakumbushwa kila siku na Mungu wetu kwamba uhai huu siyo wetu,tupo hapa kwa muda mfupi tu. Na Mungu wetu anatutaka,kwa kipindi hiki kifupi anachotupa kuishi,tuzingatia (1) Ibada,tuwe ,wapenda amani,tuyafuate maadili na maagizo yake Muumba,tuishi kwa furaha. urafi,ukorofi na ufisadi vyote hivi ni kinyume kabisa na matakwa yake Mungu. Tatizo letu sisi wanaadamu, siku mbili baada ya kuwazika ndugu zetu wanaotutoka ,basi tunarudi kwenye business as usual,kuiba ,kutukana,kuongopa,na machafu yote yanayoendana na uchu wa pesa. Mungu hapendezewi na matendo yetu. basi ndugu zangu,siku za majonzi kama hizi,pia ziwe siku za kujikumbusha na kutafakhari matendo yetu na mienendo yetu,Kama tunataka kuuingia ufalme wa mbinguni. NI mimi Zebedayo wa Magomeni
ReplyDeleteUwiiiii why why why you kanumba jamani????ill always mis u jamani machozi yananitoka kila nikufikiriapo Kanumba.May your soul rest in peace
ReplyDeleteNi masaa machache tu niliangalia mahojiano yake na Ancle kuhusu Big brother na kile kipindi cha Mkasi cha Salam Jabir.
ReplyDeleteRIP Steven. Mungu akusamehe makosa yote kwani hakuna mkamilifu katika uhai wa mwanaadamu.
Kazi yake Mola haina makosa na kila alipangalo yeye hakuna mwenye kulipangua hapa duniani.
ReplyDeleteKanumba alikuwa mcheshi sana na ndo maana watu tulizipenda kazi zake za film. Poleni sana familia ya Steven Kanumba. Sisi soteb safari yetu ni moja isipokuwa yeye ametangulia. Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu. Amen!
By DM.
Jamani Wasanii mliofanikiwa katika umri mdogo muwe makini.
ReplyDeleteTanzania ina maadui wengi wa mafanikio.
Kaeni karibu na Mungu na kupata meombi kwa watumishi wa Mungu.
Poleni sana wote mliofiwa!
poleni sana familia ndugu ilaze pema roho ya marehemu kanumba
ReplyDeleteama kweli alipangalo muumba hakuna wa kulipangua kanumba ulikuwa na mengi ya kutufanyia watanzania katika nyanja mbali mbali ikiwemo ya filamu
umetufanya watanzania kujivunia kwa uingizaji wako filamu
nje ya nchi tunajigamba kuwa na muuingizaji mzuri wa filamu
nakumbuka vile mlivyopokelewa kule burundi ilitufanya watanzania tujione tupo mbele sana na kujivunia kuwa na wewe.
DR.REMMY ALIIMBA KIFO HAKINA MMOJA KANUMBA UMETANGULIA NASI TUNAFATA
KILA NAFSI ITAONJA UMAUTI.
HABARI NDIYO HII...!
ReplyDeleteKWANZA KABISA NAPENDA KUTOA POLE KWA NDUGU FAMILIA RAFIKI NA WAPENZI WOTE WA NDUGU YETU MPENDWA KAKA YETU NA KIJANA WETU STEVE KANUMBA, NACHUKUA NAFASI HII PIA KUKUPA POLE NDUGU YETU ISSA MICHUZI KWA KUMPOTEZA RAFIKI NA KAKA MPENDWA, NI HAKIKA TUTAENDELEA KUKUKUMBUKA SANA KANUMBA, IT IS SAD THAT YOU HAVE LEFT US WHEN WE NEEDED YOU MOST. SASA BASI NDUGU ZANGU WAPENDWA HUU NI WAKATI MUAFAKA TUAMBIANE UKWELI NA NINI TUMEJIFUNZA NA KIFO CHA NDUGU YETU STEVE,NDUGU ZANGUNI NI VEMA BASI TUANZE KUWA NA TABIA NJEMA KINA KAKA NA KINA DADA.TUJIANGALIE KWENYE KIOO KAMA MTU UNA MAHUSIANO NA KAKA AMA BINTI BASI TUJARIBU KUWA WAKWELI NA KUAMINIANA. TABIA YA UDANGANYIFU KWENYE MAHUSIANO IWE NI YA GIRL FRIEND AMA BOY FRIEND KWA KWELI SI NJEMA MARA NYINGI INAKUJA NA COST ZAKE KAMA MAGONJWA, KUPEANA TARAKA NA PENGINE KUCHUKUA UHAI WAKO. SASA NDUGU ZANGU WAPENDWA NAWAOMBENI NA KUWASIHI KAMA UKO KWENYE UHUSIANO BASI KAKA DADA BABA MAMA ANGALIA NA CHUNGA UHUSIANO WAKO KWA UWAMINIFU KWANZA SI KWA SABABU YA KUMCHUKIZA MUUMBA WETU BALI INATUWEKA KATIKA MAZINGIRA MAZURI YA KUISHI KWA FURAHA, KUEPUKA MAGONJWA NA MARUMBANO YASIYO NA MSINGI. NIMEAMUA KUANDIKA HUU UJUMBE ILI KUKUMBUSHANA MAJUKUMU YETU KAMA BINADAMU. KAKA MICHUZI NARUDIA TENA KUKUPA POLE WEWE BINAFSI NA WAPENZI WOTE WA KAKA YETU STEVE.MUNGU AILAZE PEMA PEPONI ROHO YA STEVE.
Kazi ya mungu haina makosa, inasikitisha sanaaaaaaa. we real miss u. no more kanumba's move jamani. Rest in peace Kanumba
ReplyDeleteInasikitisha na inauma sana. Nataka mufahamu kabisa. Kwa utaratibu wa Mungu mtu yeyote anatakiwa aishi miaka sabini na akiwa na nguvu miaka 80. Huu utaratibu wa watu kufa na miaka 20+, 30+, 40+ sio wa Mungu. Nilazima hizo roho zikemewe na kikimbizwa. Nazikemea hiyo roho ya kuwaua vijana kwa jina la YESU. Ishindwe na iwaache vijana waishi miaka yao.
ReplyDeleteMaze hii mbaya sana. Hivi utu umekwenda wapi? Kwanini tusimhofu mungu na tukaishi vizuri kwa fura na amani? Mwanadamu yeyote duniani ana maamuzi na maamuzi ya mtu yaheshimiwe na kila mtu. Ikiwa ni hivi basi hatuna umuhimu wakuishi duniani ikiwa juhudi zetu na ujiepushaji wetu na mambo au vitu mbalimbali visivyo muhimu hauna matunda. Kila myu ataondoka laikini nifura ukiondoka kwa mda mwafaka na kihalali jamani.
ReplyDeleteMwita.Arusha
Nami nasema natumkumbuke Mungu sio tunaangalia maisha haya ya dunia tu hapa tunapita, sasa ndio wakati wa kuangalia dini yako inakuambia nini hapo ulipo ni sahihi? kama sipo ufanyaje? hili ndio swali tunatakiwa kujiuliza maana kifo kipo nasi kila wakati. Na maisha ya kesho ni marefu kuliko ya hapa duniani. Sasa tujiulize tunataka kuishi kistarehe kwa muda mfupi au mrefu. Yangu ni hayo kwa jamii ya hao wasanii na sisi wengine pia. Ahsante poleni wazazi wa Kanumba,nduguze na wale wote walioguswa na msiba huu.
ReplyDeleteIs so sad, nilikuwa nimesoma mahojiano yake jana ucku then leo amekufa, ooh i wish ungeamka uone watu wanavyoomboleza, Poleni watz na familia nzima
ReplyDeleteMarehemu Steven Charles Kanumba Mwenyezi Mungu akufungulie mlango wake, ukapumzike salama. Amina
ReplyDeleteTumempoteza mzalendo wa kweli. Ukiangalia mahojiano yake ambayo mzee Michuzi ali post siku chache zilizopita hata leo ame post tena inasikitisha. Kuna maneno mengi alitoa ya busara ambayo kusema kweli sisi watanzania inabidi tuyafuate. Watanzania wengi hatupendani, watu wana chukiana pasipo na sababu za msingi, tunakosa uzalendo, kuwa na roho mbaya kuto kufurahia maendleo ya mwenzako vyote hivi havi mpendezi mwenyezi mungu. Kwa kinywa chake yeye mwenyewe alituasa tupendane sisi watanzania na tuwapende na kuwapa vijana wetu au wasanii wetu na kuwapa support badala ya kuwakatisha tamaa. Mungu amsamehe yale yote aliyofanya kinyume na mapenzi ya mwenyezi mungu maana hapa duniani sisi binadamu ni dhaifu hamna ukamilifu, na ampokee kwenye pumziko la milele Amina.
ReplyDeleteIMENISHTUA SANA KWA KIFO CHA MWANAWANE KANUMBA,R.I.P BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE,POLENI SANA WAFIWA,IMENIGUSA KAMA MICHAEL JACKSON,LUSIA KUPELELWA
ReplyDeleteTuache kutunishiana vifua na kutishana huku tukifanyiana ubaya DUNIANI,
ReplyDeleteHAPA NI MAKAZI YA MUDA TU, Kwa kuwa sote tupo njiani, ametangulia ndugu yetu SK na sisi tupo katika Foleni hiyo hiyo!
HIVI ANKAL ULIKUWA UNAWAZA NINI ULIPOAMUA KUIRUDIA HII CLIP KARIBU MSAA 48 KABLA YA KIFO CHAKE. INATIA UCHUNGU SANA. RIP KANUMBA
ReplyDeleteI did know this guy ..but he seem like he was a nice guy, very smart and intelligent...RIP bro
ReplyDeletePoleni sana wanajamii ya Sanaa, na hasa fani hii ya uigizaji. Too soon to depart for real, gone like a candle in the wind. Wito wangu kwa jamii ni kukumbatia biblia na Quoran, vitabu hivi ni nyenzo, silaha na majibu ya mapito yeti hapa duniani. Na hii ni mahususi kwa wale wenye kunyanyukia na kupata umaarufu( fame). Kitabu cha Isaiah, Yakobo (James) na Waefeso ni nguzo imara ya jinsi gani ya kuhimili dharuba, udhalimu na umaarufu katika dunia yetu iliyojaa ubatili.
ReplyDeleteSomeni Waefeso 6 : 10 -18
Mungu akulaze Pena Steven, amen.
Ni huzun Kanumba amefariki, sote tupo nia moja ila yeye katangulia!
ReplyDeletekikubwa mimi na wewe tujiulize tunatanguliza nini kwa ajili ya maisha ya akhera na tunaacha nini hapa dunian ambacho mungu amekibariki???
FILM? I DONT THINK SO!!!
will miss this young man so much R.I.P STEVEN
ReplyDelete