Asalaam aleykum Ankal na timu nzima ya Globu ya Jamii,
 
Habari za shughuli na mahangaiko ya kila siku kaka .
 
Naomba  kutoa hoja yangu kuhusu hali ya kiwanja cha ndege cha Dar es Salaam. (Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere). Ninachotaka kukiongelea ni kuhusu kukosekana kwa eneo la watu wa kupokea wageni kukaa na kupumzika. 

Hivi kweli hali ambayo imekuwepo pale kwa watu kuwa wanasimama na kusubiri wageni wao ndio sawa? Mi nadhani kuna tatizo hasa ikizingatiwa si kweli kwamba mtu anaweza kufika uwanjani muda mfupi tu kabla ya ndege kufika na hivyo kusema eti hatochukuwa muda mrefu kusimama na kusubiri.

Lakini mbali na hivyo, wapo watu wa hali tofauti ambao huja kupokea wageni wao pale. Hebu fikiria walemavu wa miguu, kinamama wajawazito na hata watu wenye umri mkubwa. Hawa wote ni watu wasio na uwezo wa kusimama muda mrefu sasa je sio kuwanyanyasa.
 
Hi kweli inashindikana  kupata nafasi ya kuweka banda angalau dogo na viti kwa ajili ya watu wanaokuja kupokea wageni.
 
Naomba nitoe hoja kwa leo na nasimama kukosolewa kama kuna upungufu katika hoja yangu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Mdau hakuna upungufu katika hoja yako. Uko sahihi kabisa.
    TATIZO kubwa linaloikumba jamii yetu ya Wabongo ni kufanya kila kitu kwa MAZOEA (yaani hakuna ubunifu. na elimu yetu hawaandai vijana kuwa wabunifu). Utasikia hata viongozi wakuu wakijitetea kwa kudai kuwa 'mbona hata enzi za Mwalimu mambo yalikuwa hivyo!!!!" Basi unatamani kuzimia - Please give me a break.

    ReplyDelete
  2. Not surprised. JKIA was voted the 5th WORST airport on the world!!!

    ReplyDelete
  3. Huo ni uwanja wa ndege WAKIMATAIFA ndiyo maana hakuna sehemu za kupumzikia wakati wa kusubiri wageni.

    ReplyDelete
  4. Jamani walisema wakiweka sehemy kumpuzikia watu ndio watageuza "makazi" yao kwa hiyo ndio maana waliengua hiyo sehemu. Siku hizi unalipia kule VIP unaweza kupumzika.

    ReplyDelete
  5. Jamani ,lakini nyie mnaokosa kila jambo na kulaumu viongozi, hebu tutajieni wapi kuna sehemu ya kupokelea wageni ,au huko Ulaya ??? maana hata huko nimefika sikuona sehemu ya namna hiyo ,nilichoona ni sehemu za wasafiri na wasindikizaji wanasubiri ndege zao kuruka na siyo kusubiri abilia. Hapo uwanjani kwetu kwa chini ipo sehemu na soda sambusa zinauzwa hapo na viti vipo (mabenchi) wewe mtoa maoni naona husafiri mara kwa mara. Zebedayo

    ReplyDelete
  6. Hakuna uwanja wenye banda la wageni duniani, pale JkNIA mbona kuna space kubwa na viti.banda la nini mwishoe utadai mama ntilie pale.please hicho kitu hakipo duniani labda ungesema lijengwe ubungo bus terminal kwa kuwa mabasi bongo hayana muda muwafaka kutokana na sababu nyingi.

    ReplyDelete
  7. Mtoa mada ungetupa na mifano ya viwanja vingine vyenye sehemu ya kukaa kusubiri kupokea abiria. Pengine unaweza kuleta na picha kabisa tena utuletee picha za sehemu ya kupokelea abiria za Ulaya kama Heathrow na Amsterdam

    ReplyDelete
  8. Nimepita Cairo, uwanja wao ni mkuuuubwa saaaana ila hata sehemu za kupumzikia WASAFIRI ni chache saaaana. Nimesimama mpaka miguu imetaka kuingia tumboni. Ila ndo hivo cheap is expensive. Isitoshe nililala hotel kwa kuwa ndege ilikuwa ya ku connect ilikuwa siku inayofuata. Nlichoka narudi jamaa kanodaka tena kavaa uniform kanielekeza wapi nkachukue passport yangu. Huwezi amini ile nataka kucheck in ananambianimpe bakshishi. Nimegundua Cairo bakshishi ni part ya maisha na wanaomba waziiii kabisaaaa. Hata wadhungu nimeona wanajisachi kutoa bakshishi.

    ReplyDelete
  9. Kabla ya sehemeu ya kusubiria wageni,Transit lounge ipo??au kwa sababu hakuna ndege za 'ku-connect' hadi Nairobi..!!

    David V

    ReplyDelete
  10. Mbona Kipawa airport ipo sehemu ya kupumzika kwa wanaosubiri wageni! Sijui mwanzisha mada amefika lini airport lakini kwa kifupi huduma hiyo inapatikana pale nje kwenye mabench, labda kama unataka kuzungumzia kutosheleza au kutokutosheleza kwa huduma.

    ReplyDelete
  11. Hakuna utaratibu wa aina hiyo popote duniani na kama upo ni kwa upendeleo tu. Nimepita Nairobi, Heathrow, Beijing, Amsterdam, Doha, Dubai, Melbourne, Toronto, na Vancouver...Hakuna huduma kama hiyo! Wakati mwingine tuache kushambulia mambo ambayo hayana mashiko!

    Eddy
    Vancouver

    ReplyDelete
  12. aCHA KULALAMIKA MDAU. KWA UFINYU WA JNIA, NDIO MAANA SERIKALI IMEONA NI VYEMA UWANJA MPYA UKAJENGWA. WAKAZI WA KIPAWA WAMEONDOLEWA ILI UWANJA UTANULIWE.

    LAKINI KAMA WADAU HAPO JUU WALIOTANGULIA KUSEMA, AIRPORT NYINGI HAZINA SEHEMU YA KUPUMZIKIA ETI SABABU UNASUBIRI KUPOKEA MGENI. LABDA UKASUBIRI KWENYE RESTAURANTS, UNUNUE VYAKULA UKAE ULE WAKATI UKISUBIRI MGENI WAKO KUFIKA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...