Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia wananchi wakati alipokuwa akiingia katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kuongoza maadhimisho ya mika 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo asubuhi.
Amiri jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mama Maria Nyerere leo katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba wakati alipowasili katika uwanja wa Uhuru kuongoza sherehe za Muungano zilizofanyika leo jijini Dar es salaam.


BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Sioni faida ya muungano hasa kwa bara!

    ReplyDelete
  2. Hongera JK na watanzania wote kwa ujumla popote mlipo duniani.Muungano kitu kizuri sana..Yaani THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA..inapendeza sana kwenye passport na sehemu nyingine..Yaani "We are united"..siyo nchi nyingi ziko "united" hapa duniani tumesikia ya Juba na Khartoum.Mungu Ibariki Tanzania

    David V

    ReplyDelete
  3. I cant wait this bomb to finish his term he is a joke...

    ReplyDelete
  4. Tanzanians we should be proud and defend our union. God bless Tanzania and God Bless our union

    ReplyDelete
  5. Mdau David V pole pole baba msijidai watanzania mko united na mna amani pole pole baba na kutu pond sisi wa khartoum pole pole baba,angalia pemba watu wanavyoishi aangalia mikoa minginewe umasikini umekisiri na huku dar wako mafisadi ndo maana dar ina ngara pole pole baba na huu mungano unajua historia yake, wazanzibar hawautaki wanaona wanazulumiwa wanadanganywa kama watoto nenda kaishi zanzibar ulize hasa kama kweli wanautaka huu mungano wanaomba mungu leo hii ufee na wajiendeleze na nji yao na bara bila za mungano hawaendi because wananufaika sana

    watu wameshasoma sana nakuchambua sana siri hii ya munganao wee acha, watanzania msijidanyanye mko united hamko united kwa midomo watu wanatafuta mali tu siku hizi

    lala nacho David karibu khartoum usijoneee mwenyewe

    ReplyDelete
  6. Shein yuko wapi?

    ReplyDelete
  7. Napenda sana ndugu zetu wabara wanavokua na imani sana na sisi wazanzibari na hawataki kabisa kusikia muungano unavunjika,

    hivi watanganyika wanakazania kuwepo kwa muungano kwa imani yao ya kibinaadamu au kwa manufaa hapa sifahamu, kwa kuwa wazanzibari wengi hawautaki kwa sababu yamanufaa na pia wameanza kubagua mambo ya dini.

    hapa kuna video nzuri sana na fupi kuhusu Muungano http://www.youtube.com/watch?v=K5HnzidIdg0 mdau Nuramo Bradford

    ReplyDelete
  8. Sherehe za muungano kwangu ni "More Reason to stay in Bed" Tunasherehe nyingi na mapumziko mengi mno Tanzania + Gharama zinazotumika kuandaa sherehe zenyewe, ni wakati sasa zipunguzwe. Huo ni wangu mtazamo.

    By Mlipakodi Hohehahe

    ReplyDelete
  9. mkuu please hapo juu hebu tuwekee hiyo link ya website vizuri ili iwe rahisi ku click na kuona hii clip ya mungano please nimejaribu ku type kama ulivyoandika lakini hakubali please mdau wa 9;43 thursday apr 26, thanks man

    ReplyDelete
  10. Mdau Nuramo wa Bradford, Anonymous wa Thu Apr 26, 09:43:00 PM 2012

    Wengi wa wapinga Muungano ni ajabu kuona mpo nje ya nchi kama si Wakimbizi, ni Wabeba Ma-box nje au ni Wazamiaji nje ,hata huo Uzanzibari wenyewe mmeshaupoteza kitambo tu, hata Uraia kamili wenu kwa sasa haujulikani!

    Kitu cha kushangaza ni kuwa kama uwezo wa kuvunja Muungano mnao kwa nini msifanikishe kuuvunja?,,,mnangoja nini?

    Msimtegemee Mwarabu ,mvunje Muungano ili mumwangukie mtawala wenu aliyewatawala hapo zamani, yeye Mwarabu amefilisika KIFEDHA NA KIUCHUMI pamoja na nchi za Magharibi!,,,zaidi ya hapo ana vurugu za Mapinduzi kwao wala hana haja ya Unguja na Pemba yenu isiyo na mafuta ,ina uchumu wa kumilki samaki watatuna (3) tasa (wasio zaa) na gunia moja la karafuu chafu!

    Kingine mliowengi huko Majuu inasikitisha kuona hamfuatilii masuala ya kidunia ktk vyombo vya habari mpo kama mlio usingizini mnawaza usiku uishe muwahi madukani kubeba Ma-box tu!

    Angalia hiyo video ya you tube.... http://www.youtube.com/watch?v=K5HnzidIdg0 .....unayoitoa hapa ni 'animated' cartoon yaani ni kama ya kichekesho sio halisi na Kiukweli inapotosha kwa vile inahusu Siasa za Marekani na sio za Afrika na Zanzibar,

    INAONYESHA PIA KUWA ELIMU YENU NI SIFURI KABISA NA HATA KAMA UONGOZI HAMUUWEZI AKILI ZENU ZIMELALA.

    MUULIZENI MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD YEYE ALIKUWA MPINGA MUUNGANO ZAIDI YENU NINYI LAKINI SASA NI MDUMISHA MUUNGANO. YEYE NDIO ATAKUWA PROFESA MZURI WA KUWAFUDNISHA FAIDA ZA MUUNGANO.

    NURAMO WA BRADFORD NA WENZIO,

    MPO HAPO?

    ReplyDelete
  11. Mdau Nuramo wa Bradford Anonyomus wa Thu Apr 26, 09:43:00 PM 2012

    Muungano uvunjike mjitegemee:

    Hivi hebu tueleze Uchumi wa Zanzibari mnamiliki vifuatavyo:

    1-Punda wasiozidi saba (7)

    2-Ng'ombe wawili (2) wapo Pemba wanakokota mikokoteni kubeba abiria na mizigo.

    3-Gunia moja (1) la Karafuu yenye kiwango cha chini ya Ubora wa Kimataifa.

    4-Kuku tisa (9) Unguja wapo (7) na Pemba wapo waili (2)

    5-Masoko ya vyakula yapo wazi Wapemba wote wapo masoko ya Bara wanafanya biashara.

    6-Mabasi yote yapo bara mmeyapandisha Majahazi kuleta yawe Daladala

    7-Benki ni moja tu PBZ (Peoples Bank of Zanzibar) ambao mtaji wake ukilinganisha na Benki za Bara inakuwa kama SACCOS tu (Credit Union)

    HUKU MWARABU MNAYEMTEGEMEA (OMANI+YEMENI+UAE) MKIVUNJA MUUNGANO ATAWABEBA ANA MATATIZO MAKUBWA MAWILI (NYETI)

    1-YEYE AMESHAFILISIKA KIUCHUMI NA KIFEHDA PAMOJA NA NA NCHI ZA ULAYA NA MAREKANI.

    2-ANA MACHAFUKO YA KISISA YA MABADILIKO 'ARAB SPRINGS' YA KWAKE MAZITO YANAMSHINDA NDIO KWANZA RAISI ABDULLAH SALEH WA YEMENI AMEIKIMBIA NCHI JUZI.

    SASA JE , KWA UWEZO WENU WA KIUCHUMI WA MWENDO HUO WA KOBE...(Uchumi wa kutegemea bahati, na nguvu za 'Falaki') HAPO JUU MTABEBWA NA NANI?,,,HAPO MTAKAA WAPI?

    ReplyDelete
  12. Kuuvunja Muungano:

    SI NDIO YATAKUWA YA MKATAA PEMA PABAYA PANAMWITA?

    MKISEMA MRUDIE MUUNGANO WA AFRIKA YA MASHARIKI MTAJIKUTA TUMEKUTANA TENA SISI TUKIWA TANGANYIKA,,,JE HAMJAUMBUKA HAPO?

    MTAPATA AIBU MWISHONI!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...