Leo ni siku ya Sheikh Abeid Aman Karume, Rais wa kwanza wa Zanzibar ambaye siku ya Ijumaa ya Aprili 7, mwaka 1972, aliuawa kwa kupigwa risasi wakati akicheza Dhumna yeye na maswahiba wake wa karibu katika makao makuu ya chama cha Afro Shirazi Kisiwandui, Unguja, ambayo sasa ni Makao Makuu ya CCM, Zanzibar.
Leo ni siku ya mapumziko na viongozi wa juu serikalini pamoja na wananchi wa visiwani wanakutanika hapo Kisiwandui kuzuru kaburi la Hayati Karume ambaye alizikwa hapo hapo makao makuu ya chama.
Eh, eh, eh, anatoa alama ya 'v' ina maana Hayati Karume naye alikuwa mwana Chadema?
ReplyDeleteAlama ya ''V'' itakuwa CHDM wamekopi kwa Hayati Mzee Karume !
ReplyDeleteBwana Muhidin Issa Michuzi,
ReplyDeleteahsante sana kwa kunipa fursa ya kupata habari kushusu tukio hilo.
Nina suala moja: leo umehudhuria sherehe hii wakati ambapo viongozi na wananchi wamejumuika kuadhimisha kumbukumbu ya Karume?
Mimi pia nina kurasa yangu ya blog na ningependa kujua zaidi ili kuandika makala moja! (ukitaka kuona tovuti yangu ni anuani hii: http://historicite.over-blog.com/ - mimi ni mfaransa)
Ahsante sana!