Wiki chache kabla ya mambo mazito yaliyomsibu au yanayomsibu,Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, alipata nafasi ya kuongea na Salama Jabir katika kipindi maarufu cha Mkasi kinachorushwa na East Africa Television(EATV) kila siku ya Jumatatu saa tatu na nusu (9:30pm).
Ni wazi kwamba tangu Lulu aongee katika kipindi hiki, ni mengi yametokea.Mengine ni tofauti na alichokisema au “kukiweka wazi”. Bila shaka hata yeye,kama binadamu wengine,hakujua chochote kuhusu kile kilicho mbele yake.Leo hii ni mtuhumiwa ameshashtakiwa.
Jambo muhimu linaloombwa hivi sasa ni uvumilivu.Tunavyo vyombo vya sheria.Tunavyo vya dola kama Polisi na Mahakama.Endapo Polisi watamuona analo la kujibu kuhusu kilichotokea katika usiku ule,basi Mahakama zitaamua,tena kwa mujibu wa sheria na wala sio hisia. Hivi sasa ni vyema kuegemea ile dhana ya kisheria ya Innocent Until Proven Guilty(Asiye na kosa mpaka itakapothibitishwa). Ni haki ya kimsingi na kikatiba. Ni vyema ikabakia hivyo kwani sote hatujui kesho!
Hii hapa Episode ya Mkasi hususani kwa wale ambao hawakupata kuiona iliporushwa Jumatatu iliyopita.
Huyu mtoto bwana, everything about her ni uongo uongo, uongo tu,mara miaka 18 na party akafanya mara sasahivi anadai 17, na watu hawajui kwamba kwa mazingira ya kesi na ushahidi utakao patina anaweza kuhukumiwa kama mtu mzima, na hata kama siyo hivyo basi hata jela za watoto zipo, angalau akajifunze basi hata kusema ukweli, yaani ooh sina boyfriends, mimi boyfriend wa nini, mimi bado mdogo, haya kifo kimemuumbua, kwakweli utoto mbona imekuwa kazi basi, hata wakimsamehe sidhani kama kuna atakalo jifunza
ReplyDeleteAngalia hii kideo huyu bint anasema ana miaka 18 na kwenye kesi anasema ana miaka 17
ReplyDeletena hata kama ana miaka 18 ina maana kaanza starehe za kwenda makumbi ya starehe akiwa na miaka 13 au 14
sasa hivi kweli jamani hawa watoto wa sikuhizi watasoma saa ngapi?
jambo lingine nasisi wanaume tuangalie wanake wakuwanao na umri wao jamani chonde chonde mtoto hajakomaa akili anaweza kufanya lolote
ushauri kwa wenzetu waigizaji waliofikia kiwango cha kukubalika kama rest in peace kanumba
ushauri wakijiona wana uwezo wa kuoa ni bora waoe kwani kuishi na vimada tena watoto wadogo ni kujishusha thamani yao
jambo lingine ukishajiona umekubalika kwa jamii basi tafuta mwenza mwenye hadhi na umri wa kutosha ili upate ulinzi kwenye maisha
maana nasema hayo kwa sababu ukishakuwa una umaarufu basi ujuwe maadui pia wanakuwa ni wengi sasa basi tuishi kwa kujiepusha na kufanya mambo kienyeji
pole sana bint mungu atakusaidia na haki itachukua mkondo wake
ushauri wa bure kwa mabint wadogo kama lulu jaribuni kutulia tafuteni elimu kwani elimu ni ufunguo wa maisha na pia hufuta ujinga na tamaa za maisha zisizo na misingi
Rest in peace kanumba.
Hongera kwa msafisha kucha,highly professional,mchapa kazi asiye na majungu.
ReplyDeleteVIAPO VENGINE SI VYAKUAPA MSIAPIE UTADANGANYA BINADAMU ILA SIO MWENYEZI, ZAIDI YA HAPO NAMUOMBEA HUYU MTOTO ATOKE ALIPOKUWA WAMPELEKE NJE KUSOMA AANZE MOJA ANAHITAJI MSAADA MKUBWA ANKAL MICHUZI HUYO MTOTO NAUHAKIKA ATABADILIKA TU WAMPE NAFASI. MZ
ReplyDeleteHuyu ni mtoto wala hajui hata anaongea nini bado ana akili ya kitoto kabisa. Mchakato mzima wa uchunguzi wa polisi katika masuala ya kifo lazima ubadilike.
ReplyDeleteKwanza kabisa kutokana na uchunguzi wa kisasa inabidi mwili usitolewe hadi polisi na wapelelezi wamefanya uchunguzi, kama alikuwa hana nguo, vyombo vyote vilivyotuma vingepimwa kabla mwili haujatolewa kwa hiyo kitendo cha kuubema mwili wenyewe na kugusa maeneo kifo kilipo tokea kuna uwezekano wa kufuta ushahidi au kuleta utata.
Pili lulu angetakiwa apimwe majeraha yake yapigwe picha yachunguzwe ni nguvu ipi na jinsi gani aliumizwa au kuumia, kuna majeraha ya aina nyingi ambayo kwa vipimo vya kitaalamu vya kisasa unaweza kugundua yalitokana na nini, kama ya kwenye tukio ama ya kutengeneza.
Mwisho kabisa utaratibu wa kwenda kujichukulia PF3 mara sijui nini ubadilike, system nzima ifanyiwe overhaul kuanzia polisi, hospitali haswa katika masuala ya mauaji. Kuna watu wengi wenye hatia wanaachiwa au wasio na hatia kuhukumiwa kwa uchunguzi finyu.
Ahahaha huyo demu (Mtangazaji) alivyo-pronouns Lexus... demu kasema Leksusi ahahaha Bongo tambarare.
ReplyDeleteAnonymous wa Thu Apr 12, 05:33:00 AM 2012 big up. Lulu ni mtoto in the sense kuwa tufahamu kuwa alipokuwa 13 au 14 ndio tulianza kumuona lakini anasema alikuwa ameanza akiwa mdogo zaidi mfahamu kuwa hata mzazi wake alitakiwa awe na uwezo wa kumprotect otherwise system ifanye hivyo. angalia wakina Charlote Church mpaka Bieber. RIP kanumba ila nadhani hata yeye alitumia utoto wa Lulu. I hope in time ataweza kupewa elimu na sio kuwa condemed.... hata kama atakwenda jela.
ReplyDeleteyaani we kwa akili yako salama hajui kutamka neno lexus!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteWabongo bwana!!!
ReplyDeleteKila mtu anajua. Huyu anon wa 05:33am unajifanya unajuwa saaaana!!!
Wewe ni forensic expert? Si jiunge na polisi basi kama una utaalam huo!
Wacha kubwatuka ovyo ovyo kwa vitu vya kiutaalamu. Unaanika ujinga wako mzee....
Afande Sibagui Sichagui amefurahi chakula kipya alichokuwa anakikodolea macho kimeingia. Huyu Mwanamke janja sana anadanganya umri. Kama kweli ana miaka 17 wazazi wake wako wapi wawekwe ndani, vikundi vya kutetea watoto vilikuwa wapi au vipo kwa sababu ya kutafuta wafadhili kwa nini havikuingilia kati kutetea watoto kuajiriwa kwenye film industry. Huyu mwanamke ana miaka zaidi 18 anasema 17 ili hata akifungwa afungwe kama mtoto. Mwanamke kama huyu twanga tu ndani selo na wapo tu wengi hapa dar
ReplyDeleteWote kuanzia mdogo wake RIP Kanumba na hao waliombeba kupeleka mwili muhimbili wakamatwe na polisi wahojiwe kwa kina bila kumsahau daktari wake ahojiwe kama alikuwa na magonjwa sugu km vile pumu, kifafa nk. Sio kumkandamiza lulu peke yake. sheria hapa ichukue mkondo wake.
ReplyDeleteSalama anajua kutamka Lexus ila kama unamfuatilia vipindi vyake alimwoji Bhoke katika ku-joke bhoke ndo akasema baba yake huwa anatamka Lexus kama alivyotamka Salama
ReplyDeleteLulu asamehewe kwa umri wake hata kama ni 18, wanaume wanachukua advantage ya umri wake...asihukumiwe eti kwa sababu kwenye kipindi cha mikasi hakumtaja mtu wake wa ndani, hayo ni maisha yake binafsi alikuwa na hiari ya kutaja au kutokutaja...Cha msingi wazazi wa lulu, ndugu, jamaa na marafiki wamsaidie ili abadilike aendelee na maisha she still has great future...Halafu hii "Mijibaba" ambayo inaheshimika kwenye jamii halafu inatumia umaarufu na umashuhuri wao kuwalaghai watoto ndo jamii inapaswa kulaumiwa...Ni bahati mbaya jamii yetu inakwaida ya kulaumu sehemu mtu alipoangukia badala alipojikwaa
ReplyDeleteWapiga boksi wanajifanya wanajua kuongea sasa jamani, Dada Salama sema lexus
ReplyDelete@ anonymous Thu Apr 12, 07:56:00 AM 2012.
ReplyDeleteWabongo wa leo, Huna haja ya kutumia kiswaEnglish. Kwanza kiingeleza ulichotumia ni kibovu ambacho kimegubikwa na makosa katika herufi.
-Condemned siyo Condemed
-Charlotte Church siyo Charlote Church.
Sioni tofauti katika matumizi ya lugha uliyotumia na Elizabeth Michael alivyokua akiongea katika kijiwe cha urembo.
'Ama kweli Nyani haoni kundule'
Kama unataka kujua chanzo cha Salama kusema Leksus nenda kwenye kipindi chake na Bhoke!!
ReplyDeletejamani ndugu zangu,kwa utamaduni wetu sisi wanaume wa kiafrica au mazoeea ya wengi wetu natena baada ya pombe,mtu unaweza kabisa kufikiria inawezekana kilitokea nini, tumuonee huruma huyo binti , yupo kwenye wakati mgumu sana, hata marehemu anaweza kuwa anamakosa pia japokua tunampenda sana na tusingependa kumpoteza kama hivi , usiku wa manane na katoto kama hacho ambacho kichwani ni sifuri kabisa kwa super star kama yeye ?poleni sana wazazi wa huyo binti , natumaini chama cha haki za kinadada kitatia mguu pia.
ReplyDeletendo hapo sasa hata mie namshangaa uyo anaemkosoa salama. wabongo bwana kujifanya tunajua, humfikii salama hata kidogo wewe..toa point za maana sio kuandika mambo hayana kichwa wala mguu. asijue kusema lexus salama? unamjua au unamsikia?
ReplyDeletemichuzi kaka yangu hivi mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi?? je walijua ilitokana na nini? maana wamemzika mapema hata sababau hazijulikani rasmi ni kichwa ubongo moyo or what kimesababbisha?
ReplyDeletei am only 18,mudder
ReplyDeleteKwakweli Mwenyezi Mungu ndiye anajua ukweli wote mm kwa upande wangu naona kifo kilipangwa tu, ila kiuchunguzi kuleta haki sio Lulu peke yake mimi naona ata mdogo wa marehemu awekwe kwenye uchunguzi je vipimo funavyo vyote kwenye inchi yetu kwasababu dunia imearibika usimwamini mtu ata ndugu yako anaweza kukumaliza. ni kweli labda Lulu alimsukuma ila inawezekana mtu mwingine naye akammalizia fuatilieni eli sana kifo kinapotokea msimwamini mtu yeyete aliyekuwepo kwenye tukio afatiliwe na vipimo, kosa limefanyika kumzika mapema,
ReplyDeletemdau Moscow
ni kwali mdau uliyesema wamemzika mapema ni kweli kabisa mimi sijuii kwanini hawakumwacha angalau kwa siku sita wakiendelea kumfanyia uchunguzi mtu labda hata amezimia tu tayari wamemkimbiza kaburini kumzika sijuii wanaharakisha nini na mbaya zaidi wanakamati wanajua fika ya kuwa huyu aliye fariki ni movie star anawashabiki wengi sana na mtu alikuwa anapendwa sana na watu kutokana na tabia yake nzuri sasa sijui kwa nini hawakutoa siku mbili za kumuaga marehemu na siku ya tatu ndio azikwe watu wametoka mikoani kujakumuaga mpendwa wao alafu hawakuweza kumwona kwa ajili ya mpangilio mmbovu kwnn wezingempeleka uwanja wa taifa ili watu watoshelee hii ni watu wajifunze kutokana na makosa
ReplyDeleteAnon 10:45 I salute you!!!...sio just because mlikuwa mnampenda Kanumba ndio imekuwa lulu wee lulu, huyu jamaa yetu alijichanganya, lulu was most likely defending herself in whatever...most likely this will wind up as manslaughter.
ReplyDeleteHuyu mtt anajua nn kilitokea sema anavyoanza chenga za maneno mara aliumizwa so inamaana palikua na ugomvi! maan mkisema ooh jamaa alianguka c'mon! haingii akilini.Labda hakujua km ingekuwa hivyo na aseme ukweli na watu wataridhika na kumsamehe lkn she lies days n' nights trying to sneak against the law. She gt 2 com up wit a sincerly sorry!I don knw anythng about her bt wat i can tell there ar some Tyson girls in n' out.
ReplyDeleteKIGEZO KUITWA MTU MZIMA NI KUTIMIZA UMRI WA MIAKA 18:
ReplyDeleteHuyu Binti ana fosi ukubwa kwa Usanii ili apate Uhuru wa kufanya mambo ya Kikubwa kama Starehe na mambo mengine ya Ushiriki ktk gemu 'sinema' akijinadi kama 'mtu mzima' badala ya 'mtoto'
Hakuna nini wala nini!.
lulu apewe adhabu ya kuigwa na watanzania wote,kwanza akanyongwe kwenye uwanja wa fisi please.
ReplyDeleteWadau, mimi nashangazwa na maelezo ya baba yake Lulu. Kwa njia moja au nyingine anaonekana kumlaumu Kanumba kwa kutobaki 'mwwalimu' kwa Lulu na badala yake kuwa 'mpenzi'. Nadhani anachojaribu ni kumtoa Lulu katika kosa analohusishwa nalo. Lulu si mtoto mdogo wa kutojua umri wake. Kwa mdomo wake bila kulazimishwa na mtu ameeleza kuwa ana umri wa miaka 18. Iweje leo anapunguzwa umri? Katika sheria za usalama barabarani hakuna mtu yeyote mwenye umri chini ya miaka 18 anaeruhusiwa kuendesha gari. Lulu anamiliki na kuendesha gari. Hapa itabidi tuanzia na aliyeidhinisha upataji wa leseni yake.Kama kweli ana umri anaoutaja baba yake basi alikua anahatarisha maisha yake na watumiaji wote wa barabara. Endapo sheri zilipindishwa basi AWAJIBISWE. Lulu alipataje ajira bila kuwa na usimamizi wa mtu (manager) alietambulika? Ajira kwa watoto ni kosa la jinai kwahiyo wale wote waliomuajiri Lulu WAWAJIBISHWE. Ilikua mapema sana kumzika Kanumba siku ya jumanne hasa tukizingatia mazingira ya kifo chake. Uchunguzi wa kifo kama kile unahitaji muda mrefu na si siku 3. Naamini madaktari waliofanya uchunguzi wanasema kweli kuhusu sababu zilizopelekea kifo cha Kanumba. Kama itabidi tunaomba uchunguzi huru kuhusiana na umri wa Lulu kwa sababu ni mtu ambaye hana sifa ya uaminifu.
ReplyDeleteMwisho tunaomba sheria ifuate mkondo wake. Mdau huru.
mi jamani naona kuna jambo mbona wa2 wanamtetea sana hasa wanaume kama kweli huyu mtt kahusika na hicho kifo na mnamtetea ataendelea kuwamaliza au vile chakula cha wababa wa mujini? ni upuuzi eti anajidai ana miaka 17 leo alitoka wapi kwa mwanaume ucku wa kiza kingi ka yy ni mtoto! sheria ifate mkindo wake cyo kutetea 2, pili je huyu mtoto yeye ndo angefia kwa kanumba wangemtetea hivi, people think big, this is a serious case acheni mambo yakutetea tu vile anawaliwaza leo imemtokea kanumba kesho itatokea kwa ndugu yako, mtt wako au jirani yk utatetea tu hivi? ni hayo tu... uncle ucbanie comment yangu wa2 lazma wa angalie both sides of the coin huyu mtoto ni muongo sana ukiangalia interview zake nyingi ni muongo muongo..
ReplyDelete