Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisoma malezo ya awali kwa waheshimiwa wabunge namna ambavyo uchaguzi huo ulivyotakiwa kuendeshwa na taratibu zitakazofuatwa.ambapo uchaguzi ulifanyika na Wabunge tisa walipatikana watakaowakilisha nchi yetu kwenye Bunge la Afrika Mashariki ambao ni Bi. Angela Kizigha, Bi. Shy-Rose Bhanji,Bw. Mwinyi Hassan, Bw. Yahya Ussi, Bw. Taslim Issa,Bw. Kesi Papetua,Adam Kimbisa, Bernard Murunya na Makongoro Nyerere.
Zoezi la Uchaguzi likiwa linaendelea.
Mgombea Ubunge wa Afrika Mashariki katika Kundi la wanawake ambaye amefanikiwa kuchaguliwa,Bi. Shyroze Bhanji akijinadi kwa wabunge wakati wa zoezi la uchaguzi lililofanyika jana Bungeni Dodoma.
Naibu waziri wa Ujenzi Mhe. Harison Mwakyembe akimuuliza swali mmoja wa wagombea wa Bunge la Afrika Mashariki.
Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Joshua Nassari akimuuliza swali mmoja wa wagombea wa Bunge la Afrika Mashariki.
Mgombea Ubunge wa Afrika Mashariki katika Kundi la Upinzani John lifa chipaka wa TADEA akijibu mojawapo ya maswali yalikuwa yanaulizwa na wabunge wakati wa zoezi la uchaguzi lililofanyika jana Bungeni Dodoma.
katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akitoa maelezo ya mwisho kwa wagombea wa Bunge la Afrika Mashariki kabla ya kuanza kwa zoezi la kujinadi Bungeni jana. kulia kwake ni Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge Nd. John Joel.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Namuombea kwa Mungu shyrose banji ashinde yani nitafurahi sana tuuu!
    mdau canada

    ReplyDelete
  2. Kwa nini wabunge wa EAC wachakuliwe/wachaguane bungeni? wanawakilisha bunge au wana nchi? ilipaswa wachakuliwe na wana nchi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...