Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (wa katikati mstari wa mbele) akiwa na Mhe. Hussein Mwinyi (Mb.), Waziri wa Ulinzi pamoja na Mhe. Harrison Mwakyembe (Mb.), Naibu Waziri wa Ujenzi kwenye moja ya vikao vya majadiliano vya ujumbe wa Tanzania kabla ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika mjini Arusha tarehe 25 Aprili, 2012.
Mhe. Samwel Sitta, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Dkt. Stergomena Tax-Bamwenda akiongoza moja ya vikao vya majadiliano vya ujumbe wa Tanzania (haupo pichani) kabla ya Mkuano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo uliofanyika Arusha tarehe 25 Aprili, 2012.
Bw. John Haule, Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akibadilishana mawazo na Bw. George Masaju, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Masahriki mjini Arusha jana.
Mabalozi wa Tanzania katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika moja ya vikao vya majadiliano wakati wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo uliofanyika jana mjini Arusha. Kutoka kushoto ni Dkt. Batilda Buriani, Balozi wa Tanzania, Kenya, Mhe. Marwa Matiko, Balozi wa Tanzania, Rwanda, Mhe. James Nzagi, Balozi wa Tanzania, burundi na Mhe. Dkt. Ladislaus Komba, Balozi wa Tanzania, Uganda.
Mhe. Samwel Sitta, Waziri wa Afrika Mashariki, akiwa na baadhi ya Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakisaini Ripoti baada ya kufikia makubaliano katika mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo uliofanyika jana mjini Arusha.

Na Mwandishi Wetu, Arusha

Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umefanyika mjini Arusha jana kujadili na kukubaliana agenda mbalimbali zitakazowasilishwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo tarehe 28 Aprili, 2012.

Miongoni mwa agenda muhimu zilizojadiliwa na Mawaziri hao ni pamoja na mapendekezo ya kuteua Naibu Katibu Mkuu mpya kutoka Uganda kufuatia aliyekuwepo Bibi Beartice Kiraso kumaliza muda wake; kuongeza mkataba wa miaka mitatu kwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Bw. Jean Claude Nsengiyumva kutoka Burundi; kupitia ripoti kuhusu maombi ya Jamhuri ya Sudan Kusini ya kuwa mwanachama wa Jumuiya na kupitia Mswada wa sheria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu uangalizi wa uzito wa mizigo inayobebwa na magari ili kulinda barabara za nchi wanachama zisiharibiwe.

Masuala mengine yaliyojadiliwa ni Rasimu ya Itifaki ya Kupambana na Rushwa kwa nchi wanachama; Rasimu ya Itifaki ya Ushirikiano katika masuala ya Ulinzi na ripoti ya Kamati ya Fedha na Utawala.

Awali akifungua Mkutano huo wa Baraza la Mawaziri, Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Dkt. Richard Sezibera aliwaomba Mawaziri watoe maoni yao kuhusu agenda hizo ili baadae zifikishwe na kuridhiwa na Wakuu wa Nchi.

Mkutano huo wa Mawaziri ulitanguliwa na vikao vya Maafisa Waandamizi kutoka nchi wanachama kilichofanyika tarehe 20-22 Aprili kikifuatiwa na kikao cha Kamati ya Uratibu chini ya Makatibu Wakuu kutoka nchi wanachama kilichofanyika tarehe 23 na 24 Aprili, 2012.

Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo uliongozwa na Mhe. Samwel Sitta (Mb), Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kuwahusisha pia Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Hussein Mwinyi (Mb), Waziri wa Ulinzi, Mhe. Perreira Ame Silima (Mb), Naibu Waziri wa Fedha na Mhe. Harrison Mwakyembe (Mb), Naibu Waziri wa Ujenzi.

Wengine ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. George Masaju, Dkt. Stergomena Tax-Bamwenda, Katibu Mkuu wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. John Haule, Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Herbert Mrango, Katibu Mkuu wa Ujenzi, Bw. Job Masima, Katibu Mkuu wa Ulinzi, Mabalozi wa Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi na Maafisa Waandamizi kutoka Serikalini.

Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utafanyika mjini hapa tarehe 28 Aprili, 2012.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Je huyu Muheshimiwa Mwinyi kalala? au ni macho yangu? Kama kweli amelala basi Tz tuna kibarua kigumu mbele yetu! Mungu ibariki Tz, Amen.

    ReplyDelete
  2. Waheshimiwa wanasoma kwa umakini wa hali juu kweli hadi wengine kuonekana kama wamesingizia.Mwinyi hajasinzia angalia picha 2 za kwanza kutoka juu 'watu' wanavyosoma kwa umakini mkubwa..Inaonekana kilikuwa ni kitu 'very sensitive'.Someni sana kila kinacholetwa mezani tusijwe kuingizwa mkenge na wasiotupendea mema

    David V

    ReplyDelete
  3. sudani ya kusini ikingia eac tutaingia kwenye vita kila kukicha badala ya kufanya kazi,ni migogoro tuuu isiyokwisha. wamalize vita kwanza ndio walete maombi ,...hatuitaki ni wakorofi.

    ReplyDelete
  4. We acha hizo, au umetumwa na Sudan Kaskazini? Sudan Kusini waingie mapeeema. mwarabu si mtu. Angalia babu zetu waliopelekwa utumwani Uarabuni hakuna aliyeko huko hata mmoja, angaliw walichofanya Dafur and Sudan Kusini. Wacha kabisa maneno hayo Kasome historia!!!!!

    ReplyDelete
  5. Documents za mikutano yote ya EAC zinaandikwa kwa kimombo. Sasa kama Husein Mwinyi ni Kayumba mwenzangu, ataweza wapi kuzisoma. Badala yake ni bora alale ili wanaojua kimombo wasome kwanza. Wakishamaliza, kama naye anatakiwa kutia sahihi, basi atafanya kazi hiyo iliyompeleka. BONGO MAMBO SAFI SANA!

    ReplyDelete
  6. HAHAHAHAHA

    Niacehni nichekeeee!

    Wadau Anonymous wa kwanza Thu Apr 26, 06:14:00 PM 2012 na Anonymous wa Fri Apr 27, 11:00:00 AM 2012

    Mhe. Hussein Mwinyi sio 'KAYUMBA' kama sisi, yeye ni Msomi Dakitari kamili tena wa Tiba!

    Inawezekana kusinzia kwake kulitokana na uzito wa yaliyoandikwa ktk makabrasha anayoyasoma!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...