MIMI NI MTANZANIA NINAEISHI NJE YA TANZANIA,NA NINAMILIKI PASI YAKUSAFIRIA YA ULAYA...OMBI LANGU NINAOMBA MSAADA KWA WATANZANIA WANAOISHI HAMBURG GERMANY AU VITONGOJI VYA KARIBU VYA HAPO, NIKO NA NIA YAKUTAKA KUHAMIA MJI HUO ILA SUALA LA KWANZA LITAKALO NIWEZESHA KUINGIA NA KUKUBALIKA KISHERIA NA ILI KUMUDU GHARAMA ZA MAISHA NI KUPATA KAZI,
SASA BASI KAMA KUNA MTU YEYOTE ANAEWEZA KUNIELEZA UPATIKANAJI WA KAZI HAPO, NAJUWA KWAMBA ILI KUINGIA KIURAHISI NISICHAGUWE KAZI, NA NIKO TAYARI KUFANYA KAZI YEYOTE ILE HATA KAMA YAKUSAFISHA NIKIZINGATIA SIJUI LUGHA,
MUHIMU IWE NI KAZI YA MDA MREFU KIDOGO ILI KUWEKA MAMBO SAWA KUMUDU KUTAFUTA CHUMBA NA MENGINE NITAHITAJIA KAZI YA MDA MREFU, ISIWE KAZI YALEO ,KESHO USUBIRIE SIMU NYUMBANI,
NINAOMBA SANA KWA WALE WENYE KUJUWA ZAIDI KUHUSU GERMANY KUNIPATIA MAELEZO ZAIDI KUPITIA E MAIL YANGU HII ...mmbongo5@hotmail.com
NATANGULIZA SHUKRAN ZANGU KWA KILA MMOJA ATAEWEZA KUNIPA MSAADA WA AINA WOWOTE ULE
WENU, SULEIMAN
SASA BASI KAMA KUNA MTU YEYOTE ANAEWEZA KUNIELEZA UPATIKANAJI WA KAZI HAPO, NAJUWA KWAMBA ILI KUINGIA KIURAHISI NISICHAGUWE KAZI, NA NIKO TAYARI KUFANYA KAZI YEYOTE ILE HATA KAMA YAKUSAFISHA NIKIZINGATIA SIJUI LUGHA,
MUHIMU IWE NI KAZI YA MDA MREFU KIDOGO ILI KUWEKA MAMBO SAWA KUMUDU KUTAFUTA CHUMBA NA MENGINE NITAHITAJIA KAZI YA MDA MREFU, ISIWE KAZI YALEO ,KESHO USUBIRIE SIMU NYUMBANI,
NINAOMBA SANA KWA WALE WENYE KUJUWA ZAIDI KUHUSU GERMANY KUNIPATIA MAELEZO ZAIDI KUPITIA E MAIL YANGU HII ...mmbongo5@hotmail.com
NATANGULIZA SHUKRAN ZANGU KWA KILA MMOJA ATAEWEZA KUNIPA MSAADA WA AINA WOWOTE ULE
WENU, SULEIMAN
Mdau wewe utakuwa ni wale wale ndugu zetu waliokwama wa kule UGIRIKI...!!!
ReplyDeletePana njia nne (4) za kukunusuru:
UKAE UKITAMBUA DUNIA UMESHAFILISIKA (KAMA ILIVYOKWISHA FILISIKA HIYO UGIRIKI UNAYOIKIMBIA SASA) NA SUALA LA KAZI NI GUMU DUNIA NZIMA.
1.Nenda au wasiliana Ubalozi wa Tanzania hapo Ujerumani wakubebe ingawa umeshapata Uraia wa Ulaya lakini utakuwa bado ni ndugu yetu uombe hata kazi ya muda ya Ukalimani au kupika Chai ya Wageni Ubalozini.
2.Kaa huko ujishikize tukutumie mizigo (lakini sio biashara chafu) ili ubane tugawane, lakini uwe mwaminifu.
3.Omba hao Wandugu waliopo Ujerumani wafungue Shule ya Chekechea ya Kiswahili (Day care centre) ili ufanye kazi ya kulea watoto wakati wazazi wao wakiwa kazini mchana.
4.Ukishindwa ajira hizo (3) juu huko Ulaya ni bora urudi Bongo aidha Ujitambulishe Ubalozi wa nchi yako hapa Bongo ili ufanye kazi za kuwa Kiungo kati yao na sisi Watanzania, ama vipi unaweza kujiajiri kwa kwenda kukata mkaa Kaliuwa-Tabora !
KAZI KWAKO!!!
Vipi kaza ya kubeba 'BOKSI' nayo unaweza?
ReplyDeleteGermany hakuna kazi kipande. Wenyewe wanafanyakazi zote hizo maana hata mfagiaji anapata malipo mazuri sana. Kima cha chini Germany ni euro 10. Europe sasa kazi hakuna maana zote zimechukuliwa na Wapolo na jamaa wengine waliojiunga na EU. Jaribu kujiajiri mwenyewe kama kazi za hand carwash, housecleaning, gardening, walk the dog, lollypolly, taxi, kila la heri.
ReplyDeleteWewe si Mtanzania kutokana na Sheria ya Uraia ya Tanzania.
ReplyDeleteUmesema unamiliki hati ya kusafiria (Passport) ya nchi moja ya Ulaya. Kama una Passport ya nchi moja ya Ulaya au nchi yoyote ile duniani ukiachilia ya Tanzania, basi unakuwa umeukana uraia ya Tanzania
Sema tu utabaki Mtanzania kinafsi, ila kisheria na ki-documents wewe si Mtanzania
Talking about stating the bloody obvious. If you dont have any constructive comments stay silent.
DeleteKazi Ujerumani uombwa kwa vituo vya kutoa ajira. Wasiliana nao. Kama hujui kijerumani, utakuwa na shida kidogo. Utahitaji kuwa na social security card pia.
ReplyDeletewewe unaishi ulaya na una pasi ya ulaya-unauliza maswali kama hayo.humu nani atakupa jibu,mpaka umepata pasi ya ulaya u should know better
ReplyDeleteUK has fallen back into recession, the Economy has shrank by 0.2% during the first quarter of this year, many other European countries will join the que.
ReplyDeleteNakutakia kila la kheri kupata hiyo,hali huku mamtoni ni ngumu, nakushauri chukua kazi utakayoipata, hata kama ni ya kusubiri simu.
Kama Ulaya kamasi zimekutoka njoo Marekani ulee wazee Vikongwe kwa kuwafunga nepi za Pampers !.
ReplyDeleteUnaweza kuja huku Marekani ulee Mateja na Mataahira, usitegemee kazi ya Kibosi !.
Je upo tayari?
Ahhh Ulaya imekutaaa wewe rudi nyumbani Tanzania nyumbani ni nyumbani uje ulime na Pasipoti yako ya Ulaya utaiweka Darini kwanza!
ReplyDeleteMtikisiko wa Uchumi na Kifedha umekamata sana huko Majuu.
ReplyDeleteAcha ubishi rudi Tanzania uje kufanya ajira Binafsi kama:
1.Umachinga,
2.Uchome Chips,
3.Kuokota vyma chakavu,
4.Kuokota chupa za maji na mifuko ya plastiki,
5.Siku hizi hata kuelekeza watu mitaa Mjini ni kazi na inalipa!,
6.Ufanye kazi za Ususi wa Rasta Saluni za kike au uwe Kinyozi,
7.Pana Vyoo vya Manispaa mijini utakuwa Cashier (Mkusanya fedha) kwa vile Umakaa Majuu utawahudumia Wageni huku Bongo vizuri,
8.Kuchoma Vitumbua,Maandazi na Chapati Jioni na Usiku Mjini kwa Wahindi,
9.Kuwa Mchuuzi wa mboga mboga Sokoni Kariakoo kazi ni kuamka saa 10 za usiku na Gunia lako tupu begani ukifika unawahi nafasi,unapewa mzigo wa mboga mali kauli bila kulipa unauza ukimaliza unakata faida yako unarejesha fedha jioni kwa Dalali, siku imekwisha.
10.Kuchoma mahindi na Kuuza Juisi za Ukwaju N.K. !
Bongo shida lakini sio kihivyo angalau uwezekano unapatikana mkono kwenda kinywani!
Mtikisiko wa Uchumi na Kifedha umekamata sana huko Majuu.
ReplyDeleteAcha ubishi rudi Tanzania uje kufanya ajira Binafsi kama:
1.Umachinga,
2.Uchome Chips,
3.Kuokota vyma chakavu,
4.Kuokota chupa za maji na mifuko ya plastiki,
5.Siku hizi hata kuelekeza watu mitaa Mjini ni kazi na inalipa!,
6.Ufanye kazi za Ususi wa Rasta Saluni za kike au uwe Kinyozi,
7.Pana Vyoo vya Manispaa mijini utakuwa Cashier (Mkusanya fedha) kwa vile Umakaa Majuu utawahudumia Wageni huku Bongo vizuri,
8.Kuchoma Vitumbua,Maandazi na Chapati Jioni na Usiku Mjini kwa Wahindi,
9.Kuwa Mchuuzi wa mboga mboga Sokoni Kariakoo kazi ni kuamka saa 10 za usiku na Gunia lako tupu begani ukifika unawahi nafasi,unapewa mzigo wa mboga mali kauli bila kulipa unauza ukimaliza unakata faida yako unarejesha fedha jioni kwa Dalali, siku imekwisha.
10.Kuchoma mahindi na Kuuza Juisi za Ukwaju N.K. !
Bongo shida lakini sio kihivyo angalau uwezekano unapatikana mkono kwenda kinywani!
Ya nini tabu ?
ReplyDeleteUst. Suleiman unahangaika bureee Ulaya rudi Bongo ukabidhiwe Madrassa ufundishe !
Pambana bwana Sule.Maisha ni mapambano.Tegemea maoni ya kuku-blast hapa na kukutatisha tamaa.Hao wajerumani wametutawala na kutunyonya hao ilitakiwa wakupatia ajira kama fidia kwa mababu zetu(utani)
ReplyDeleteDavid V
Habari wabongo wenzangu,mimi ni mtanzania ninayeishi Europe,ndugu yetu Seleman hujatueleza uwazi vizuri,kama lugha inayokupiga chenga ni ipi?na je unakibali cha kuishi nchi gani?maana wako watanzania ambao watakusaidia ila sasa kibali gani?Mdau Europe.
ReplyDeletePasipoti yako ya Ulaya utaiweka Darini kwanza!....this is so funny n painful advice.
ReplyDeleteWith that being written, my advice is try brazil(kamalizie savings zako pande hizi kabla hujarudi bongo,life z too short)...u know what im talkin about!
Ulikimbilia Ulaya ukijua maisha ni bata daily eeh? Hadi UKAUKANA uraia wako!!! Kula joto mwanangu.. Huku bongo raha tu kimtindo... OOH, uliomba msaada wa KAZI.. Sorry i FORGOT.. WHAT IS YOUR PROFESSION SIR?
ReplyDeleteChiggs.
Walioko Ujerumani, wanafanya kila jitihada kukimbia, wewe unataka kwenda huko? Watu siku hizi wakimbia ulaya, waenda USA na CANADA. NAkushauri na wewe uangalie uwezekano wa kujiripua hukohuko Canada. Otherwise, uko ktk hali ngumu. Ungekuwa msichana, ningekukubalia uende Ujerumani. Maana kule kama ukikosa kazi, ungeweza jiuza mwenyewe, ukapata pesa nzuri sana, na ukaiongezea nchi kipato, kwani utalipa kodi. Lakini sharti uwe msichana mwenye mvuto.
ReplyDeleteDuuh umenishitua sana mtu wangu!!
ReplyDeleteMajuu bila sera nomaaaa
Sasa tutakuita raia wa wapi mtasha wangu kwani bongo huruhusiwi tena imekula kwako mazima!!
Boys b4 you change your sitizenship you must think twice!!!!!
Duh! haya maono/maoni yanayotolewa humu mimi homa.
ReplyDeleteWivu huleta chuki, na chuki huleta maangamizi(kifo).
Mdau mmoja huko juu uliyesema kwamba bwana suleiman siyo mtanzania tena kwa sababu ana pasipoti ya Ulaya; haupo sahihi. Kuna tofauti kati ya uraia na utaifa. Watu wengi sana hudhania kwamba utaifa na uraia ni kitu kimoja chenye majina tofauti. Unaweza kubadilisha uraia kwa kuandika kwamba "mimi siyo tena raia wa nchi fulani". Lakini utaifa haubadilishwi namna hiyo. Suleiman anaweza kuwa raia wa Ulaya, lakini utaifa wake utaendelea kuwa utanzania.
Utaifa ni kama kabila, haubadiliki isipokuwa baada ya vizazi kadhaa.
mazee wasikukatishe tamaa, ujerumani bado wako sawa kiuchumi ukilinganisha na nchi nyingine za ulaya, lugha wala isikupe shaka utajifunza wakati ukiwa huko, mimi nimerudi bongo na nimerudi sababu makaratasi yamekataa, wewe kwa kuwa sheria tayari unayo wewe nenda tu, swala la kupata kazi kabla haujafika huko, kwa ujerumani sahahu ndugu, labda hiyo kazi huwe umeisomea, hizi za kina sie wewe nenda, mwenzio nilikuwa natembea restaurant moja mpaka ingine mpaka nikapata kazi ya msaidizi wa jikoni, na kwakuwa sikuwa mvivu, nikawa najifunza kupika vyakula vyao, ikaja kuwa nami napika tu, mpishi wao alipoondoka nikawa mimi ndiyo mpishi nikapatiwa na msaidizi, lakini as i said tatizo makaratasi, mimi nilijilipua na ujerumani makaratasi kutoa kama mwenye bahati mbaya kama mimi ni 10 years, me nikaona ni kupoteza muda tu, nimejipeleka mwenyewe nikarudi kusema za kweli nilisave vijisent na kwa kuwa ni muangaikaji, nina biashara zangu hapa na mambo si mabaya namshukuru Mungu, ulaya ni kuzuri kwenda kutafuta msingi wa kufanyia kitu, lakini kama unataka hela, aisee hela hipo hapa tz, hakuna tunachotengeneza wenyewe kila kitu kutoka nje ni biashara, kwahiyo usife moyo wewe nenda kajaribu, ukishindwa umeshindwa hayo mambo ya kutafutiwa kazi kabisa, nadhani ilikuwa ulaya ya zamani kabla nchi hazijaungana, kila la kheri Mungu atakusaidia
ReplyDeleteJAMANI KUSEMA UKWELI ULAYA KUMEKUWA KUGUMU SANA TENA SANA, HAKUNA KAZI KABISA, NIMEKAA HAPA UK BARIDI KIBAO ILA KWA SASA NATAKA KURUDI NYUMBANI TENA SIO SIKU NYINGI BY AUGUST NAFUNGA VILAGO VYANGU...THANK GOD NIMESOMA MPAKA MASTERS SO WACHA NIKAHANGAIKE HOME TU, ULAYA HAKUFAI KABISA KWA SASA...WAZUNGU WENYEWE WANAPANGIMBIA HAPA.SISI WAPIGA BOX TUNAGOMBANIANA KAZI, MASIHA YA ULAYA YAMEBAKIA UFAHARI TU KWAMBA UPO ULAYA ILA HAMAN TENA CHA MAANA ZA DI YA KUPATA HELA YA KULA TUU.
ReplyDeleteHIVI WEWE KAMA HIO NONDO FAKE YA KI- NIGERIA UMENUNUA KWA FIX YA KUJIFANYA WEWE TAYARI UMEISHA KUWA NA URAIA WA KIZUNGU SHAURI YAKO UNGEWAAMBIA WAKAKUFUNZA KWANZA FIX YA KUDANGANYA ÍLI IWE INAONEKANA KAMA KWELI. WEWE UNAWEZA KUWA UNAISHI ULAYA HALAFU HATA SHERIA ZA EU HUZIJUI? SWAIN MKUBWA ! RUDI KWENU TEMEKE KAÅALULE SAMAKI NA DAGAA NCHANGA.
ReplyDeleteHALAFU UNAONEKANA HATA SIO WA KIMJINI WEWE YAANI HATA UJUZI HUNA KWANI UMEKUJA LINI HUKO ALBANIA?
AU UMEUZIWA CNONDO YA KITURKIMENISTAN, UKADANGANYWA NI YA ULAYA?
RUDI BONGO SWAIN WEE
HIVI WEWE KAMA HIO NONDO FAKE YA KI- NIGERIA UMENUNUA KWA FIX YA KUJIFANYA WEWE TAYARI UMEISHA KUWA NA URAIA WA KIZUNGU SHAURI YAKO UNGEWAAMBIA WAKAKUFUNZA KWANZA FIX YA KUDANGANYA ÍLI IWE INAONEKANA KAMA KWELI. WEWE UNAWEZA KUWA UNAISHI ULAYA HALAFU HATA SHERIA ZA EU HUZIJUI? SWAIN MKUBWA ! RUDI KWENU TEMEKE KAÅALULE SAMAKI NA DAGAA NCHANGA.
ReplyDeleteHALAFU UNAONEKANA HATA SIO WA KIMJINI WEWE YAANI HATA UJUZI HUNA KWANI UMEKUJA LINI HUKO ALBANIA?
AU UMEUZIWA CNONDO YA KITURKIMENISTAN, UKADANGANYWA NI YA ULAYA?
RUDI BONGO SWAIN WEE
Suleiman huku Germany hakuna kazi za aina yako, afadhali jaribu UK maana walau kuna kazi nyingi za kufanya, hawa jamaa wa Germany kazi nyingi zinafanywa na wenyewe na Waturuki ambao wengi wao ni raia kutokana na historia yao.
ReplyDeleteShauri zenu na nyie mliobadilisha uraia bila kufikiria mara mbili, mkae mkijua ninyi sio watanzania wala hamna haki ya kumiliki chochote kile hapa bongo. Kaane mkijua hata mkija lazima mkumbuke sheria za immigration, sio zaidi ya siku 90 hata kama mama yako kafariki wewe huna haki huku wala huna haki ya kumiliki chochote hapa bongo hata kama ulijenga nyumba halafu ukenda Ulaya na kubadilisha uraia wewe ukijulikana basi mpaka nyumba yako itachukuliwa na serikali kwani huna mkataba wa kumiliki jitu hapa kwetu tanzania , Mlijifanya kukimbilia huko UK na marekani na kubadilisha uraia bila kutafakali kwa kina sasa mtajijua huku wewe sio mtanzania na nikikujueni mmoja mmoja naunguza picha IMMIGRATION POLISI mnyang`anywe mali zenu huku kwani sio raia ninyi na mna miliki vipi mali huku kwetu tanzania? Jengeni huko huko ulaya huku nyie sio watanzania .
ReplyDeletemdau ILALA
Usikate tamaa Bwana Suleiman, bunch of haters in here Damn!!! c'mmon people, where is ndugu philosophy, Jamaa ameuliza swali kama huna jibu shut up, stop hating. Pamoja katika dua mkuu, umenikumbusha wahenga hapa " anayetafuta hachoki, hata akichoka..... Mie siko EU, nakushauri ujaribu unyamwezini kama ukiweza, kila la heri, nina imani utakuwa sawa, Usiwajali waoshwa vinywa humu, kudra zinatoka from one and only " Mungu"
ReplyDeletewadau mnapoitaja ulaya muwe makini. hizi nchi zinajitegemea. ulaya kama hunaelimu yajuu na inayokubalika,ukasoma na kuifahamu lugha yao vizuri unawezakupatakazi. szani kama nirahisi kupata kazi Bongo? sisi huku Scandinavia tunakula bata. KAribuni sana. elimu itumie bwana
ReplyDeleteMdau wa ILALA, kama unayoyasema ni sahihi sasa kwanini kila siku mnalia kwamba ardhi yenu wanapewa wawekezaji wageni wakati wasiokuwa raia hawana haki ya kumiliki chochote?
ReplyDeleteArdhi, migodi, viwanda, vyote vinamilikiwa na wageni. Kisha unawaambia watu kwamba hawaruhusiwi kumiliki chochote.
Ukweli unabakia kwamba mtu mwenye uraia wa ulaya ana haki kuliko mtanzania hapa bongo. Na hata polisi wa bongo hawezi kumnasa kibao raia wa ulaya, wakati wewe watakusukutua kama mpira wa kona.
Na kwa taarifa yako, wanaotuongoza wengi tuu watoto wao/ndugu zao wana paspoti za ulaya pia. Na za bongo pia wanazo ingawa sheria ya nchi hairuhusu hilo.
Kalaghabaho wee...
Thank you. Tell these wankers. Watu wengi humu upeo mfupi. Akili sio shule tu. Waswahili wengi uwezo wetu wakufikiri duni. Tunabaniana humu wakati wengine wanakula nchi.
DeleteAma kweli ukiisoma hii taarifa ya huyu jamaa seleiman hapa, na ukaangalia hizi comment watu wanazotowa ndio utakuta
ReplyDeleteni jinsi gani ya baadhi ya watanzania walivyowajinga tena wakutupwa, jamaa kauliza kitu safi na rahisi sana kama huna jibu haina haja wewe kuandika hapo, unatukana, unasema sio mtanzania ....nk hayo yamekujaje hapo tena jamaa kaulizia watu wanaoishi germany ambao watakuwa na uelewo wa haya masuala ya ulaya sio wewe unaekaa ILALA, ambae mwisho wako ni julias nyerere air port kusafirisha mtu pale, jamani tuacheni ujinga uliokuwa hata haukusaidii chochote
Nenda usisikilize watu. Kama huna pesa nenda "Homeless" kabla ya saa saba za mchana ukajiandikishe, watakupa pa kulala na chakula ukale church. Nunua dictionary la kijerumani na kingereza ili ujifunze lugha maana wajerumani hawasemi lugha nyengine. Tafuta hosteli za Generator, chumba unashare na mademu kwa siku Euro 10. Tafuta agency wa kazi. Lakini kama unataka pesa tu kwanini usije UK hapa. Kazi za Carehome mbona nyingi tu, usisahau driving licence ukija hapa.
ReplyDeleteMdau
Beds
mimi nawashangaa hao wanaomchokonoa mwanzao jibuni mlichoulizwa kama unakaa ujerumani au unajua kuhusu lililoulizwa kama si hivyo tulia kimya waachie wanaojua...yanakuhusu nini mengine... aah watz bwana...
ReplyDeleteNAMI NI MTANZANIA.....SINA JIBU KUU LA KUMPA MSHIKAJI SULEIMAN COZ AM NOT IN GERMANY....ILA USHAURI WANGU NI AS A MAN JUST HUSTLE HARD AND BELIEVE IN YOURSELF AND TRUST IN GOD...YOU WILL MAKE IT THROUGH.....UJUMBE MKUU NI KWA WATU AMBAO WANAONGEA SELA ZISIZO ZA MATUMAINI AMA KUONEKANA NI MAJUNGU....JAPOKUWA HUJULIKANI ILA YAONYESHA WAZI NI JINSI GANI UNA-AKILI FINYU NA JINSI ULIVYO MBINAFSI WA MAWAZO MALI JE????HII NDO ISFA MBAYA YA SISI WATZ..'ASILIMIA KUBWA' WAPO HIVYO ANGALIA MAONI YA WENGI HUMU...CHUKI NA UBINAFSI. TUBADIRIKE WANDUGU....mzee wa kurekebisha tabia MM
ReplyDeleteMaoni yenye roho mbaya kama haya hutolewa na watu wa aina mbili.
ReplyDelete1)Kwanza; watu ambao wameshindwa kwenda Ulaya.
2)Pili; Watu ambao wamewahi kwenda ulaya lakini wameshindwa kubakia Ulaya.
Na inawezekana kabisa wengi wao wameandika maoni yao huku wakiwa wamevaa nguo za mtumba ambazo zimeshavaliwa na akina Suleiman wa Ulaya.
Sasa hili kundi la pili ndiyo baya zaidi kwa sababu lina hasira sana na huwachukia wale ambao wameweza kubakia Ulaya ki-makaratasi.
Mimi binafsi nitaamini kwamba maisha bongo ni mazuri kuliko Ulaya siku mtakaponiambia kwamba Tanzania siku hizi imeacha kuagiza nguo za mitumba kutoka Ulaya.
NYIE WA TANZANIA MWENZENU ANAWAOMBA ADVICE NYIE MNA MPA MAJIBU YA KUNYA YANI WA BONGO WANAFIKI SISI, HAPO AKIJA KUWA MTU MAARUFU DUNIANI MTAANZA KUJIPENDEKEZA OOH MTANZANIA MWENZETU YULE,,,,,,,NA NDO MAANA HATUENDELEI....KAKA MI NAKUSHAURI JIANGALIE WE MWENYEWE HAMNA MTANZANIA HATA MMOJA ATAKAYEKUSAIDIA...UKIISHI ABROAD NI BORA UFANYE URAFIKI NA WA NIGERIA LAKINI CYO WATANZANIA WENZAKO.......WANAFIKIIIII KISHENZI...UR A CHAMP DO YOUR BEST WHATEVER DOESNT KILL U ITS MAKE U STRONG
ReplyDeleteKwa TAARIFA YENU PASIPOTI YA TANZANIA IPO JUU ZAIDI YA:
ReplyDeletePASIPOTI YA:
1.UGIRIKI (ILIYOKWISHA FILISIKA)
2.URENO (INAYOPUMULIA MASHINE)
3.HISPANIA (AMBAKO BIASHARA ILIYOBAKI NI MADAWA ***UNGA*** NA KUOA AU KUOLEWA NA WAZUNGU WAZEE VIKONGWE)
BORA MDAU SULEIMANI UNGEKUWA NA PASIPOTI YA MSUBIJI AU MALAWI INGESAIDIA INGEKUWA NAFUU ANGALAU!
ZAIDI YA HAPO,
1.HATA KADI YA KUPIGIA KURA YA TANZANIA INA THAMANI KUBWA SAANA ZAIDI YA PASIPOTI YA BAADHI YA NCHI ZA ULAYA!
2.VITAMBULISHO VYA UTAIFA VINAVYOANZA KUTOLEWA VITAKUWA JUU ZAIDI YA PASI ZA ULAYA, ANGELIENI JUZI TU URENO WAZUNGU WALIKUWA WANAUZA MAJUMBA YAO KWAO URENO HUKU WAKIHAMISHIA AKIBA ZAO BENKI NA HISA KWENDA MSUMBIJI NA KUHAMIA MSUMBIJI KWA MAISHA YA KUDUMU !,,,HIYO NDIO DALILI KUBWA KABISA YA KUFILISIKA KWA ULAYA
bwana suleiman achana na haters. ushauri wangu ni kuwa nenda UK au Holland mambo safi. boksi la kumwaga. huko ujerumani unaweza kuwaste time tu.
ReplyDeleteEwe Ndug. Suleiman bwana mkubwa:
ReplyDeleteChukua uamuzi wa Ujasiri wa kurudi Tanzania mara moja,
Hiyo Pasipoti ya Ulaya haina faida mara utakapotua Uwanja wa Ndege na utakapoingia nyumbani Tanzania.
Nduguzo tutakusaidia ''INGAWA UMESHAKUWA NA PASIPOTI YA NJE TUTAKUBEBA KAMA MWANANDUGU'' hayo mambo ya Uraia wako wa Ulaya utaweka kapuni kama Mdau juu alivyokwambia,,,Pasipoti yako ya Ulaya weka Darini kwanza!
Vitambulisho Muhimu hapa nyumbani ni:
1.Kadi ya KUPIGIA KURA.
2.Kitambulisho cha Manispaa ch Ukazi.
3.Kutakuwa na Uraia wa nchi zaidi ya moja muda si mrefu,,,tutakubeba utafuata taratibu ya kupata KITAMBULISHO CHA TAIFA ''NATIONAL IDENTITY CARD'' ambazo ndio zinaanza kutolewa sasa.
4.Baada ya muda kiasi utaweza kuirejesha Pasipoti yako ya Tanzania na huenda mwaka 2015 Ukapiga kura kumchagua Raisi kupitia C.C.M ,Raisi wa Tanzania!
KUMBUKA'' UNAWEZA KURUKA MKOJO UKAKANYAGA KINYESI'' !!!
ZINGATIA MUDA, UMESHAKAA HUKO ULAYA UKAPOTEZA MUDA WAKO MWINGI HIVYO USIZIDI KUPOTEZA MUDA, RUDI TANZANIA.
Wasalama Alekoum kaka Michu pamoja na kikosi chako cha blogi yetu tukufu, nakuomba nitupie swali langu katika blogi yetu,najua wamo wasomi na waungwana ambao wanazijua sheria na busara ya kuishi hapa duniani,wajinga nao wamo,badala yakutoa mchango wa maoni wao watakandia tu, yote hayo ni sawa, jamii lazima tutofautiane.MIMI niko huku bara la America,na kukaa kwangu huku,kwa kweli nimejifunza adabu ya kufanyakazi,sijilaumu kuja huku bali nashukuru sana, sasa nataka kurudi kwetu na nitautumia huu uelewa wangu kwetu bongo,Shinyanga,nimerudi mara kwa mara bongo,na nilichokiona ni kwamba ,vijana wengi niliosoma nao huko huko Bariadi wana maisha mazuri kunishinda hata mie huku,wana nyumba,wana wake zao na watoto,mimi huku nilijindanganya kuoa mzungu ,ndoa haikudumu ila nimezaa naye na nalipia mtoto kisheria mpaka atakapotimiza miaka 18 na kwa vile anakaa na mama yake ,mimi hanioni kama baba tena na sina mamlaka naye,hata kumkanya siwezi,ana heleni puani,gololi kwenye ulimi,nywele leo kapaka rangi hii kesho kijani n.k Bariadi asinge behave namna hii, cha ajabu yuko secondary lakini hajui kitu,sijawahi kumuona na kitabu anajisomea,yeye nicomputer tu na marafiki na anatumia neno F kila mara. nabaki najiuliza je ?? kweli watoto hawa ndiyo future ya hizi nchi ??? na hizi nchi ukimgusa mwanao kwa kumshikisha adabu,basi anakuitia polisi. Swali langu ni hili,mimi nataka nirudishe passipoti yao nirudi kwetu Bariadi,bahati nzuri shamba huko ninalo na nitapata mke wa kinyamwezi ambaye hata chai au ugali atanipikia, yaani heshima ndani ya nyumba,mzungu yeye ilikuwa ananiendesha tu kama gari bovu na matusi juu,kitendo cha ndoa ,mpaka yeye ajisikie. Jamani kuzeekea huku ni fedheha na ni mateso,mliojisahau kununua kibanda au kiwanja kwenu (bongo) itakula kwenu,mimi nionyesheni tu namna ya kurudisha hili passipoti lao,na je hii miaka niliyowafanyia kazi huku na kulipa kodi,akiba yangu ya uzeeni nitakapofika hiyo miaka 65 wataituma bongo ??? kama nilivyosema mwanzo hii blogi yetu ina wasomi na wajinga pia wamo kama huyo jamaa wa Ilala-lakini , katika msafara wa mamba ,kenge nao wamo.wasalam alekoum.
ReplyDeleteUPEPO UMEGEUKA!
ReplyDeleteDunia ina tabia au utaratibu wa mabadiliko ktk maisha ambayo yanaakisiwa na vitu vingi ikiwemo maendeleo na changamoto.
Mfano miaka ya nyuma Afrika ilikuwa ikipokea wafanya biashara wengi kutoka bara Arabu na Asia miaka hiyo,,,lakini kwa sasa Waafrika ndio wanaokwenda zaidi nchi hizo kwa biashara.
Miaka ya nyuma Waafrika wamekuwa wakikanyagana na kukakamaliana na Maafisa wa Uhamiaji na Ubalozi ili kwenda kwao,,,LAKINI KWA SASA WACHACHE WAZUNGU WENYE AKILI WANAHAMA ULAYA NA KUJA AFRIKA !,,,AMINI USIAMINI TENA ZAIDI NI KUWA BAADA YA ULAYA KUFILISIKA WIMBI HILI LIMEKUWA KWA KASI.
MFANO MAJUZI HUKO PORTUGAL (URENO) WALIRIPOTIWA WAZUNGU WAKIUZA MAJUMBA YAO NA KUHAMISHA AKIBA ZAO WAKIHAMIA MSUMBIJI KWA MAKAZI YA KUDUMU.!!!...WENYE NCHI WANAIKIMBIA ULAYA YAO ,WEWE JE?,,,SULEIMANI UPO HAPO?
SULEIMAN,
ReplyDeleteWala usipate tabu, ungali Kijana hakuna sababu ukakaribisha shinikizo la damu, kuwaza na kuwazua!
kwa sasa pana mpango wa Makazi ya bure kwa Waathirika wa Mafuriko ya Desemba 2011 Udhamini wa Serikali,,,rudi Tanzania (LAKINI PASIPOTI YA ULAYA FICHAAAA) moja kwa moja utaungana na wenzako hukoo Mabwe Pande!!!.
WANAOUNGA MKONO ULAYA:
ReplyDeletePana Anonymous wa Thu Apr 26, 12:10:00 PM 2012
Anamalizia.....katika msafara wa mamba ,kenge nao wamo.wasalam alekoum.
Suleiman wasiliane na huyo jamaa ambaye ana Uraia wa Marekani na kuwa ana nia ya dhati ya kuachana nao ili arudi Bongo akiwa anayo mengi aliyoayona kuhusu ubaya wa Uraia wa nje ya kumnufaisha Suleiman.
Pia Mdau wa anaemalizia....Tanzania siku hizi imeacha kuagiza nguo za mitumba kutoka Ulaya.
Anonymous wa Thu Apr 26, 07:15:00 AM 2012.
UKWELI KWA SASA HAPA TANZANIA...SUALA LA KUVAA ****MITUMBA***** SIO SHINIKIZO AU HALI KWA KUWA NGUO MPYA ZIPO ZA KUZALISHWA HUMUHUMU NDANI (KWA UBORA WA JUU KABISA) NA PIA ZINAZOTOKA HUKO HUKO MAJUU (ITALY, FRANCE, UK,US, CANADA e.t.c),,,,PESA YAKO TU....KWA HIYO KUAMUA KUVAA MITUMBA NI UAMUZI WAKO KULINGANA NA UWEZO WAKO KIPESA, UKIWA NAZO PESA KWAMWE HUTAVAA MITUMBA...MPO HAPO?
Moja kwa rudi Tanzania na uchukue Kadi ya Uanachama wa Chama cha Mapinduzi C.C.M....!!!
ReplyDeleteKARIBU SANAAA...!!!
NASHUKURU KWA KUWA SIKWENDA ULAYA:
ReplyDeleteNiliwahi kuhangaika sana miaka ya nyuma kutafuta kwenda nje ya nchi lakini sikufanikisha !
Mwishowe nimekuja kuona kumbe Mungu akipanga kuna faida zaidi kwa vile kama ningeenda huko ningeishia kubebeshwa Mabox bureee.
Wote niliokuwa nao na walifanikiwa kwenda , wengine wamerudi wakiwa chali na pesa hawana, huku waliobaki huko ni wabeba mabox!
MIMI NILIOBAKI HAPA TANZANIA NAMSHUKURU MUNGU SAAANA KWA KUWA KWA SASA NINA MAISHA YANGU NINAMILIKI KAMPUNI YANGU MWENYEWE NINA SHUGHULI ZANGU NA NINAINGIZA KIPATO !
KITU AMBACHO HATA KAMA NIKITAKA KWENDA HUKO NJE NI KWA MATEMBEZI MAFUPI TU ,NINAWEZA KWENDA MUDA WOWOTE KWA KUWA VIGEZO NINAVYO,KWA SABABU KILA KITU CHANGU KINAENDA VIZURI TU HAPA TANZANIA!.
MUNGU NI MKUBWA SAAANA!!!!
Hi kam Bado unatafuta kazi ..kazi Kai zipo kibao hapa ujerumani usiwasikilize hao..mimi naishi hapa ujerumani miaka 10..niko munich ni..ni nguvu yako tu kama utaweza kufanya kazi masaa 10kwa siku utapata pesa nzuri tu ..
ReplyDeleteKama bado unatafuta kazi njoo munich kazi zipo kibao...usisikilize wat.u. huko bongo maisha ni mangumu sana kama huna mtaji..ni nguvu yako tu .kama.utafanya kazi kwa bidii utapata pesa za kuanzisha biashara bongo..ukafanikisha ndoto zako..
ReplyDelete