Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mamia ya wakaazi wa jiji la Tanga leo baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kesho katika sherehe za Mei Mosi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi nchini (TUCTA) Bw. Nicholaus Mgaya leo baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kesho katika sherehe za Mei Mosi zinazofanyika kitaifa mkoani humo.
Glob ya jamii tunaomba maelezo kutoka kwa mpiga picha kuhusu hayo mapokezi yaliyojaa bendera za CUF.Walikuwa 'wanamsanifu' rais au walikuwa wanaonyesha Umoja tulionao sisi waTanzania bila kujali vyama??.Sina mbavu..Sasa nimekubali..Kweli ukitaka kupunguza 'stress' ingia kwenye Blog ya Jamii..!
ReplyDeleteDavid V
kweli nimeamini kuwa wapwani wote ni ndugu mmoja ...hapa utapata picha halisi ilivyo hapana ccm hapo wanampokea rais wa nchi hii
ReplyDeleteila ni cuf ndio wako juu huu wanaonesha uzalendo wao cuf kuwa sio watu wa chuki bali niwapenda watu na amani
cuf juu.....
kazi kwelikweli, bado natafakari kwanini kapokelewa na watu walioamua kuvaa nguo na kushika bendera za CUF, ingelikuwa bendera za CCM nisingeliogopa sana maana ni chama chake. Pongezi nyingi kwa walioamua kushika bendera ya taifa
ReplyDeleteNaona huyu mwanahabari ni CUF, lakini hongereni sana kwa kutokuwa na kinyongo.
ReplyDeleteEndeleeni na moyo huo huo.
natoa hoja tu, kumekuwa na spelling errors sana katika habari za humu ndani si dhambi ila nadhani kupitia kile unachoandika kabla ya kukirusha inapendeza zaidi kila siku nikisoma lazima kunakuwa na errors. kama hii imeandikwa rais kuwa "MHENI" rasmi nadhani ni mgeni au?
ReplyDeleteCUF oyee wafundisheni ustaarabu wale wa chama cha kususa na kuandamana. Hapo wananchi pamoja na kuwa wengi wao ni CUF lakini wanampokea kwa furaha na bashasha kiongozi wa nchi. Na huo ndio ustaarabu sio mitusi kashfa na upuuzi usio na maana. Tanzania ni yetu sote bila kujali itikadi ya vyama!
ReplyDeleteUnamaanisha Lusinde au? hata iweje walio wengi tushafunguka akili kuhoji na kudai haki si upuuzi funguka akili ndugu
ReplyDeleteKwa mara ya kwanza hebu tusikie Hotuba ya Mei Mosi "iliyokwenda shule!".Tuone aibu kumlipa Mtanzania kima cha chini cha shs 120,000/= wnegine wanapata hata shs 80,000/= kwa mwezi!Tumechoshwa na hotuba za "tupo katika mchakato","tuko mbioni","infact,maandalizi yamefikia pazuri","watanzania kaeni mkao wa kula,wahisani tumesha washika pazuri","utafiti wa awali unaonesha kwamba uchumi wetu unachupa kwa kasi ya ajabu!,kwa hiyo tutarajie neema itashuka","wenzetu nchi marafiki wamekubali kuingia ubia na sisi,kwa hiyo ajira za kumwaga ziko mbioni",bla bla bla bla bla & blaaaz! ee mwenyezi Mungu tusaidie,utupe mkate wetu wa kila siku na utusamehe makosa yetu kama tunavyo wasamehe waliotukosea,usitutie majaribuni,siku zote na milele,amina!
ReplyDeletepolisi wa Mwanza mpooo,na wale machizi ambayo bado hamjabadilika,igeni mfano wa Tanga, siyo mapanga na visu kwenda kukata kata wabunge wa chadema,aibu tupu huko Mwanza,na mpaka polisi eti wanatetea CCM !!!! Polisi ni chombo cha raia siyo chama. Zebedayo
ReplyDeleteSiasa kwa sasa imegawanyika zaidi!
ReplyDeleteDalili ya kushamiri kwa CUF ni kuwa watu wana mwamko wa Siasa za Kistaarabu na sasa ili kuukabili huu ushindani wa Kisiasa CCM inatakiwa ijipange zaidi.
Wajameni cha ajabu hapo ni kipi hasa? Hivi tumeshasahau kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar imeundwa kwa collabo ya CCM na CUF. Hapa wana-CCM B wanamkaribisha kiongozi wao...naomba kutoa hoja!!
ReplyDeleteSawa kabisa anony:may 01:10:21:00
ReplyDeletekimahesabu CUF=nusu CCM