Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mamia ya wakaazi wa jiji la Tanga leo baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kesho katika sherehe za Mei Mosi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na  Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi nchini (TUCTA) Bw. Nicholaus Mgaya leo baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kesho katika sherehe za Mei Mosi zinazofanyika kitaifa mkoani humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Glob ya jamii tunaomba maelezo kutoka kwa mpiga picha kuhusu hayo mapokezi yaliyojaa bendera za CUF.Walikuwa 'wanamsanifu' rais au walikuwa wanaonyesha Umoja tulionao sisi waTanzania bila kujali vyama??.Sina mbavu..Sasa nimekubali..Kweli ukitaka kupunguza 'stress' ingia kwenye Blog ya Jamii..!

    David V

    ReplyDelete
  2. kweli nimeamini kuwa wapwani wote ni ndugu mmoja ...hapa utapata picha halisi ilivyo hapana ccm hapo wanampokea rais wa nchi hii

    ila ni cuf ndio wako juu huu wanaonesha uzalendo wao cuf kuwa sio watu wa chuki bali niwapenda watu na amani

    cuf juu.....

    ReplyDelete
  3. kazi kwelikweli, bado natafakari kwanini kapokelewa na watu walioamua kuvaa nguo na kushika bendera za CUF, ingelikuwa bendera za CCM nisingeliogopa sana maana ni chama chake. Pongezi nyingi kwa walioamua kushika bendera ya taifa

    ReplyDelete
  4. Naona huyu mwanahabari ni CUF, lakini hongereni sana kwa kutokuwa na kinyongo.

    Endeleeni na moyo huo huo.

    ReplyDelete
  5. natoa hoja tu, kumekuwa na spelling errors sana katika habari za humu ndani si dhambi ila nadhani kupitia kile unachoandika kabla ya kukirusha inapendeza zaidi kila siku nikisoma lazima kunakuwa na errors. kama hii imeandikwa rais kuwa "MHENI" rasmi nadhani ni mgeni au?

    ReplyDelete
  6. CUF oyee wafundisheni ustaarabu wale wa chama cha kususa na kuandamana. Hapo wananchi pamoja na kuwa wengi wao ni CUF lakini wanampokea kwa furaha na bashasha kiongozi wa nchi. Na huo ndio ustaarabu sio mitusi kashfa na upuuzi usio na maana. Tanzania ni yetu sote bila kujali itikadi ya vyama!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 01, 2012

    Unamaanisha Lusinde au? hata iweje walio wengi tushafunguka akili kuhoji na kudai haki si upuuzi funguka akili ndugu

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 01, 2012

    Kwa mara ya kwanza hebu tusikie Hotuba ya Mei Mosi "iliyokwenda shule!".Tuone aibu kumlipa Mtanzania kima cha chini cha shs 120,000/= wnegine wanapata hata shs 80,000/= kwa mwezi!Tumechoshwa na hotuba za "tupo katika mchakato","tuko mbioni","infact,maandalizi yamefikia pazuri","watanzania kaeni mkao wa kula,wahisani tumesha washika pazuri","utafiti wa awali unaonesha kwamba uchumi wetu unachupa kwa kasi ya ajabu!,kwa hiyo tutarajie neema itashuka","wenzetu nchi marafiki wamekubali kuingia ubia na sisi,kwa hiyo ajira za kumwaga ziko mbioni",bla bla bla bla bla & blaaaz! ee mwenyezi Mungu tusaidie,utupe mkate wetu wa kila siku na utusamehe makosa yetu kama tunavyo wasamehe waliotukosea,usitutie majaribuni,siku zote na milele,amina!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 01, 2012

    polisi wa Mwanza mpooo,na wale machizi ambayo bado hamjabadilika,igeni mfano wa Tanga, siyo mapanga na visu kwenda kukata kata wabunge wa chadema,aibu tupu huko Mwanza,na mpaka polisi eti wanatetea CCM !!!! Polisi ni chombo cha raia siyo chama. Zebedayo

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 01, 2012

    Siasa kwa sasa imegawanyika zaidi!

    Dalili ya kushamiri kwa CUF ni kuwa watu wana mwamko wa Siasa za Kistaarabu na sasa ili kuukabili huu ushindani wa Kisiasa CCM inatakiwa ijipange zaidi.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 01, 2012

    Wajameni cha ajabu hapo ni kipi hasa? Hivi tumeshasahau kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar imeundwa kwa collabo ya CCM na CUF. Hapa wana-CCM B wanamkaribisha kiongozi wao...naomba kutoa hoja!!

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 01, 2012

    Sawa kabisa anony:may 01:10:21:00
    kimahesabu CUF=nusu CCM

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...