Ile sherehe ya Muungano wa Tanzania na Utamaduni wa Tanzania ambayo kila mwaka inaandaliwa na Jumuiya ya Watanzania Roma mjini Rome, na kusherekewa na Watanzania wote nchini Italy mwaka huu itafanyika siku ya Jumamos tarehe 28 april 2012 kuanzia saa kumi na moja jioni mpaka Lyamba, kwenye ukumbi wa KARISPERA CLUB 69 ulipo kwenye mtaa wa VIA ANGELO EMO 69, mjini Roma.Kutokana na ombi la Watanzania wengi, Mwaka huu sherehe hizi zitasherekewa mpaka usiku mnene.Uongozi wa Jumuiya unapenda kuwajulisha Watanzania wote waishio Rome na Italy kwa ujumla kuwa mnaomba muwasiliane na Mwenyekiti wa jumuiya Mh.Leonce au katibu ndugu Andrew Chole Mhella kupitia e-mail hii www.watanzaniaroma.yahoo.it au kwa simu namba             0039-3479094800       ili muweze kupata taratibu za kushiriki kwenye sherehe hii.Uongozi unawaomba pia Watanzania wote mfike kwa wingi kwenye kikao cha mwisho ili kuweza kuweka mambo sawa kabla ya sherehe. Mkutano utafanyika jumamosi ijayo tarehe 21 aprili kwenye Mtaa wa Via Principe Amedeo 70, uliopo maeneo ya Termini Station.Kwa maelezo zaidi tutembeleeni hapa www.watanzania-roma.blogspot.com.

Andrew Chole Mhella,
Katibu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ankal Michuzi mbona hauiweki ile video post ya merehem Steven Kanumba
    please iangalie kama ikiwa nzuri nitafurahi uki post kwenye Blog / Asante from Mussa Ally

    link : http://www.youtube.com/watch?v=5fiRghjGPew


    email. mussaally@hotmail.com

    ReplyDelete
  2. Asante Andrea.Humu duniani kuna watu huwa 'ni vichwa'-J.K Nyerere alikuwa 'kichwa'.Kila nikisoma/nikiangalia kinachotokea kwa sasa kati ya Sudan ya Kusini na Sudan(Khartoum na Juba) nakumbuka moja ya hotuba zake alipokukuwa akisisitiza muungano...kwamba mkitengana tu hamtabaki salama..ni kama kula nyama ya....ndicho kinachotokea pale Sudan.TUDUMISHE MUUNGANO WETU(nategemea kupata upinzani hapa!)

    David V

    ReplyDelete
  3. Andrew Chole MhellaApril 16, 2012

    Habari za asubihi Ankal! tafadhali naona usahihishe e-mail address naona imeandikwa kichina kidogo. Inasomeka hivi watanzaniaroma@yahoo.it. Kazi njema.

    Katibu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...