![]() |
Hayati Jane Mkami Mponzi |
Familia ya Eng. Gabriel Mponzi wa Oyster Bay, Dar es salaam, na familia ya marehemu Dr.Allan Makange wa Kibaha, Pwani, zinapenda kutoa shukrani zake za dhati kwa wote walioshirikiana nao kwa namna moja au nyingine kwenye kipindi kigumu cha msiba na kuhitimisha safari ya mwisho ya mpendwa wao Jane Mkami Mponzi.
Ni vigumu kutaja mtu mmoja kuwa ndiye aliyekuwa na msaada zaidi, ila hatuna budi kutoa shukrani zetu kwa madaktari, wauguzi na wafanyakazi wa hospitali ya Aga Khan kwa jitihada zao za kuokoa maisha ya Jane. Maparoko na mapadre wa kanisa katoliki la Mt. Petro Oyster Bay, Dar es Salaam pamoja na wale wa Ipamba Iringa na wanakijiji wake wote. Jumuiya ya Moyo Mtakatifu wa Yesu ya Oyster Bay Dar Es Salaam; IPP Media; Vodacom Tanzania; Africa Media Group; wamiliki wa blog mbalimbali Tanzania; majirani na marafiki zetu wote, asanteni sana.
Shukrani yetu kubwa ni kwa Mungu Mwenyezi kwa kutupatia zawadi ya maisha ya Jane hapa duniani, na tutaishangilia zawadi hii kwa kumsifu na kumtukuza Mungu siku zote za maisha yetu.
Tunapenda kuwakaribisha wote kwenye mkesha maalum wa kuyaenzi maisha ya Jane tarehe 13 Aprili 2012 kuanzia saa 11 jioni nyumbani kwa Eng.Mponzi #39, Br. Msasani, Oyster Bay. Pia kutakuwa na Misa ya shukrani kwenye kanisa la Mt. Petro Oyster Bay siku ya Jumamosi 14 Aprili kuanzia saa 12.30 asubuhi na baadae tutamalizia na chai nyumbani Oyster Bay. Wote mnakaribishwa sana.
“Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia mwokozi,
Bwana Yesu kristo; atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili
wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe
chini yake” Wafilipi 3:20-21
Jane daima tutakukumbuka. Mungu aendelee kuwafariji ndugu jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu.
ReplyDeleteMr & Mrs Moses Sabuni, Cyprus, Northern Turkey
R.I.P Jane, nilikufahamu toka 1995 ulikuwa jirani yangu, ulipenda kunitania kuwa mimi ni " NJUKA" ulipokuwa ukisoma kisutu girls.
ReplyDeleteKwame Ibwe, PhD.
who was this lady? main functions of the lady? any update! I did not know her before her death.
ReplyDeleteWewe Anon wa 3 hapo juu kama huna kitu cha kusema tafadhali kaa kimya. Nimesoma na Jane pale Waldorf College na alikuwa mcheshi na mtu mpenda watu. Ingawa umeondoka too soon, bado tunakukumbuka. May you rest in peace. Natoa pole kwa familia ya Mzee Mponzi, ndugu na marafiki wa Jane wa karibu.
ReplyDeleteYou will be missed.
Class mate wa Jane (1999-2001).
Grand Forks, ND
ANNON of 02:24:00 PM...You are one of the Idiot i never knew Youexist!! Kwa nini una comment wakati aujui kinachoongelewa? Kama aumjui just say R.IP, and shut ya mouth..IDIOT
ReplyDeleteTry to respect other peoples feeling, Anyway Rest in Peace my cousin JANE, I will always treasure the moment we had at school,
Mbona mnakuwa wakali?? Mwenzenu kauliza vizuri. Maana hata mimi sikuwa namjua, na mpaka sasa sijamjua kuwa yeye alikuwa nani. Sasa jamani mkitueleza vizuri kuna tatizo gani. Au mwenzangu hamkumuelewa, maana mimi naona hakuuliza kwa ubaya!
ReplyDelete