Ndugu Watanzania pamoja na marafiki:
Ninaandika habari ya kufariki dunia kwa Ndugu Christina Chacha, kwa moyo mzito na wenye shinikizo, uso uliojaa simanzi, na ubongo uliogandamizwa. Ndugu yetu mpendwa ambaye wengi wetu humwita tu Mama Chacha, alishindwa na maradhi  alfajiri ya 3/31/2012 kule nchini Afrika Kusini. Mipango ya kusafirisha maiti inaendekea wakati huu kutoka Afrika Kusini kuja hapa Marekani. Mume wa marehemu Ndugu Ezra Chacha ambaye aliondoka hapa nchini Jumatano, 3/28/2012, yuko Afrika Kusini akishughulikia mipango hiyo ya kumsafirisha marehemu, kwa ushirikiano na ndugu na jamaa walioka hapa Marekani. 
Uongozi wa  jumuiya ya Watanzania katika eneo letu la Ghuba ya San Francisco (Bay Area) na vitongoji  vyake,  unaomba ushirikiano wa kila mmoja wetu katika kuwafariji na kuwasaidia kifedha  familia ya Ndugu  Chacha, kwa vile gharama za msiba huu ni kubwa, kama picha ya kumsafirisha marehemu inavyodhihirika. Familia ya Ndugu Chacha inatoa shukurani kwa juhudi za awali amabazo tayari zimefanyika.
 Binafsi ninaomba tuwe na moyo wa ushupavu na uthabiti  katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, maana jumuiya yetu imepokonywa mtu ambaye alikuwa rafiki na shujaa wa jumuiya yetu katika majira yote.  Tutaendelea kuwataarifu  kufuatana na upokelewaji wa habari zinazohusika.  Kwa mawasiliano:
 Anwani:
5024 Santa Rita Road
Richmond, CA 95803
Simu:
(510) 222-7308 – Hm
(707) 656-5157 – Cell
Hapo awali baadhi ya watu walichangia wazo zuri kwamba iwepo account ambayo itatumika kuweka pesa za shughuli hii ya msiba. Ningependa kuwapa taarifa kuwa hiyo accout imefunguliwa na nambari zake ni kama ifuatavyo:
Routing #121000358
Account#0693571257
Name on the account: Ezra Chacha.

Asanteni na nitafurahi kuwaona wote kesho

Warioba
Phone# 707 6565157 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Poleni sana wafiwa. Pamoja na maelezo mazuri ya mipango ya mazishi,swali kubwa hapa kwa wadau litakuwa hivi,marehemu kafia A.kusini ambako ni karibu sana na tanzania ukilinganisha na california-USA,kwa nini marehemu asizikwe tanzania? Au huko hana ndugu/wazazi,labda hili lingetolewa ufafanuzi kabla ya watu wengi kuuanza kuhoji kulikoni

    ReplyDelete
  2. poleni na msiba

    Mnamsafirisha kutoka wapi kwenda wapi?

    Imekuwaje hamumuziki Tanzania? itasaidia watu mkieleza sababu ili mpate michango zaidi

    RIP

    ReplyDelete
  3. Poleni na Msiba!

    Wandugu Watanzania huko California Marekani na Wakurya kama mnavyoona Afrika Kusini ni angalua karibu na huku TZ kuliko huko US hata kwa njia ya barabara kwa nini msije kuzikia hapa Tanzania hata kama mnao Uraia wa huko Marekani?

    ReplyDelete
  4. Poleni sana wafiwa na Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
    Lakini kama ambavyo wengine wamehoji, huu msaada unaombwa ambao ni gharama kubwa sana kusafirisha mwili kutoka South Africa hadi California, kwani mwili usipelekwe nyumbani Tanzania ambapo ni karibu na gharama ni nafuu zaidi?
    Wahusika naomba muweke maelezo mazuri ili kupunguza maswali ambayo ni obvious.
    Sisi hapa US tumezowea kusaidiana kuchanga pesa ili ndugu zetu wazikwe nyumbani, na wale ambao kwa mapenzi yao huamua wasisafirishe huzika hapahapa. Hili linahitaji maelezo lieleweke vizuri.

    ReplyDelete
  5. Swali hilo la kwanini wasimpeleke akazikwe Tanzania, hata mimi nilikuwa nalo, lakini baadae nikakumbuka kwamba yawezekana marehemu Christina alikuwa mzungu kwahiyo kwao kwa kuzaliwa ndiko waliko penda akazikwe sina hakika hata hivyo waulizeni vizuri 'otherwise' ni vizuri angepelekwa kule Mara ni karibu zaidi na gharama itakuwa ndogo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...