Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) Paul Chizi (katikati) akikata  utepe kuzindua rasmi safari za ndege hiyo kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza wikendi hii.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) Paul Chizi akiongea na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza mara bada ya kuzindua safari za ndege mpya ya Shirika hilo aina ya Boeing 733-500 wikendi hii.
 Mhudumu wa Ndege wa ATCL ambaye hakufahamika jina mara moja akimhudumia mmoja wa abiria wakati wa uzinduzi wa safari za ndege ya ATCL aina ya Boeing 737-500.
 Ndege ya ATCL  aina ya  Boeing 737-500 inavyoonekana kwa mbele
 Wahudumu wa ndege wa Shirika la ATCL wakipozi mbele ya Kamera ya blogu hii.
Abiria wakishuka kwenye ndege aina ya  Boeing 737-500 ya ATCL kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakati wa uzinduzi wa safari za ndege hiyo wikendi hii. Ndege hiyo itafanya safari za kila siku za Dar es Salaam-Kilimanjaro-Mwanza mara mbili kwa siku.

Na Mwandishi wetu.

MARA baada ya wiki moja tu baada ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kupata ndege aina ya Boeing 737-500 iliyoanza rasmi safari za Dar es Salaam-Kilimaanjaro-Mwanza wikendi hii, Shirika hilo limeanza mchakato utakayoliwezesha kupata ndege nyingine kati ya wiki tatu au sita zijazo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya safari hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Paul Chizi alisema shirika lake linatarajia kupata ndege nyingine aina ya Boeing ambayo italiwezesha shirika hilo kufanya safari za nje zikiwemo Dar es Salaam-Lusaka, Dar es Salaam-Harare and badae Dar es Salaam-Dubai.

“Tumeanza utekelezaji wa mpango kazi wetu wa muda mrefu ambao utatuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
“Katika mpango wetu ,tunatarajia kupata ndege nyingi na bora zaidi. Kwakuanzia,tunarajia kupata ndege nyingine katika kipindi cha wiki tatu mpaka sita na ndege hiyo itatuwezesha kuanza safari za kimataifa,’ alisema Chizi.

Chizi aliwataka wananchi pamoja na mashirika mbalimbali kuunga mkono jitihada za Shirika lake na kuahidi kuwa shirika hilo litazingatia utoaji wa huduma bora kwa bei nafuu. “Mafanikio ya shirika yatategemea mchango wa wadau mbali mbali. Tunaomba wananchi watuunge mkono ilituweze kupata mafanikio zaidi,” alisema.

Chizi alisema kuwa katika wiki chache zilizopita kampuni yake ilizindua tovuti ambayo itasaidia katika kuboresha huduma ya ukataji tiketi kwa wateja kwa wakati wao na kuboresha utoaji huduma wa kampuni.

 “Kitu cha kujivunia ni kuwa wateja sasa wanaweza kutaka tiketi kupitia mtandao bila kufika katika ofisi zetu au kupitia mawakala wetu kama ilivyo zamani,” alisema.

Nae Jaji Mstafu wa Mahakama Kuu ambaye alipata nafasi ya kusafiri kwa kutumia ndege mpya ya shirika hilo aliomba Serikali kutoa ruzuku kwa Shirika hilo na kusisitiza kuwa uboreshaji wa shirika hilio utaongeza pato la taifa kupitia sekta ya Utalii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2012

    TUNASHUKURU KUNA NDEGE. ONYO
    1. VIONGOZI WAACHE KUWAPIGIA SIMU WAKURUGENZI WAKE ZAO NA FAMILIA KUSAFIRI KWA MKOPO WASIOLIPA.

    2. WAWE BAHILI KAMA PRECI.. AIR KWANI UNALIPA LAKI 4 TOKA KIA HADI DIA UNAAMBULIA KOROSHO ZA 500 NA JUICE YA 200/- KKWA KUANZA TUWE BAHILI BAADAE TUJUE LA KUFANYA.

    3. TUACHE KUPEANA TENDER KINDUGU TUTAHARIBU HIKI KIDOGO TULICHONACHO

    4. UBISHOO WA NGUO ZA KILA AINA KWA WAHUDUMU UISHE HIZO WALIZONAZO ZINATOSHA

    5. WAWEKE BAYANA HUKO KUKODISHA KUNALIPWAJELIPWAJE NA WANADHANI WATAWEZA KUNUNUA YAO SIO SUALA LA MCHAKATO WA KUPATA NYINGINE HOW? KWA MKOPO AU KUKODI?

    6. NASHAURI WALE WALIOKAA AIRTZNANIA TOKA ENZI HIZO NA HASA WALIOINGIZWA NA MKURUGENZI ALIEONDOKA WAONDOLEWA NAOMBA ANGALIENI VYETI

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 20, 2012

    I hope hii haina kideri na ufanisi utaongezeka pia.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 20, 2012

    Hongera saana ATCL shirika la Taifa letu sasa kuweni macho kabisa kila Raia alipe nauli halali tuu hakuna cha mgodo wake na Rais au baba yake hapo mtakuwa na mashirika mengi ya ndege yanawangooja saana maa kuna utalii mwingi saana Tanzania.Pia itakuwa vema kuweka hub ndogo mwanza kwa ajiri ya Bukoba na shinyaga na tabora kigoma.Pia nyingi mmejionea jinsi watanzania wanavyowatakia kila jema safari ya kwanza tuu mwanza Ndege karibu Robo tatu kujaa kabisa so kuweni makukini mwanzo mgumu saana ila najua kila mtu akiwa tayari kufanya kazi kwa ajili ya Taifa mtafika mbali saana keep up and see you next month to mwanza --s.maziku in Amsterdam

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 20, 2012

    GO GO GO ATCL tuko pamoja msituangushe fuateni ushauri mnaopewa taratibu tutafika. Jamani watanzania makosa tulishayafanya na tunajua kabisa ni nini kinatuangusha hivyo tujirekebishe kama tunataka kusonga mbele tufanye kazi kitaalam haya mambo ya kujuana hayatatufikisha popote. Na hii ni kwa mashirika na taasisi zote za umma

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 20, 2012

    GO GO GO ATCL,GO GO CHIZI tunaomba route moja huku nchi za WEST AFRICA mkipata hiyo long range jet..Tafadhali

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 20, 2012

    mi nahisi wizara ya uchukuzi na hata wizara ya fedha kuna watu wako kwenye pay roll ya prec.. air.hainiingii akilini hata kidogo kwa nini airline ya taifa haipewi ushirikiano wa kutosha toka serikalini,lawama zinatupiwa kwa watu wasiohusika,mimi kama mtanzania ninaamini kabisa ukifanyika uchunguzi wa kutosha katika wizara tajwa hapo juu watagundulika pandikizi wa matatizo ya airtanzania.
    Inaniuma sana kuona precision inatunyanyasa watanzania mfano mdogo ni pale ndege ya airtanzania ilipopata ajali kigoma asubuhi mida ya saa 4.ilipofika mchana yake precision walipandisha nauli kwa zaidi ya laki moja.kwa kweli tulihangaika sana.ni hapo ndipo nikajiuliza maswali mengi jeuri hawa watu wanatoa wapi?je ni watanzania wenzetu hawa kweli au ndio walewale mafisadi wanaojali matumbo yao tu na si utaifa?
    Tafadhali serikali naomba mlifuatilie hili la uchunguzi ktk wizara hizo.
    Mungu ibariki Airtanzania

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 20, 2012

    Mukiacha undunization na kufanya biashara kwa ushindani kama mashirika mengine mtafanyikiwa.

    ReplyDelete
  8. Nawapongeza sana ATCL, sasa tuchape kazi sawa2, naamini baada ya muda kidogo tutasikia hata mnakuja Njia panda Ulaya (Amsterdam)sitashangaa, ebu oneni hayo maoni hapo juu jinsi watu wanavyowatakia heri, mjue ya kuwa kweli tulimiss ndege yetu watanzania. Kila la heri

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 21, 2012

    Tukiacha unafiki, tutafanikiwa! Ndani ya serikali kuna watu wanasaidia ndege binafsi zipate kazi (safari) za serikali. Inawezekana wana maslahi binafsi au la! Tujifunze Rwanda! Wao wameweza sisi tunashindwaje? Vilevile 'Air Hostess' nao waangaliwe! Au hairuhusiwi kuwabadilisha? Wanaonekana ni akina mama zaidi!!

    ReplyDelete
  10. Hongereni sana ATL,si mnaona jinsi ambavyo watanzania walikuwa na kiu ya kutumia ndege ya shirika la, mkumbuke kuwa huduma yenu ilikuwa bora zaidi nchini enzi hizo,nakumbuka hata tangazo lenu ITV wakati huo lilikuwa la kuvutia hadi unatamani ukapande ndege hiyo. Nawatakia heri na hata muonekane viwanja kama njia pand ulaya (Amsterdam).TUKO NYUMA YENU

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 21, 2012

    Go ATCL , its about time nasi tuwe na ndege yetu. hiyo route ya Dubai muhimu sana maana nikifika Dubai, lazima niingi bongo na nyie...home sweet home in our own plane.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 21, 2012

    Nashauri maafisa masoko wa ATCL waanze na wateja wote ambao ni wafanyakazi wa Serikali wanaoutumia usafiri wa anga kwenye maswala yao yote ya kikazi na kuna route za ATCL, waishauri Serikali sasa iache uteja kwenye mashirika binafsi ya ndege mpaka inapobidi iwe hivyo kwani ndege hii kama ni ya uhakika ni bora kuitumia ili shirika letu ATCL liweze kusimama, Kila la heri na nimaamini uongozi wa ATCL sasa utakuwa umefanya utafiti wa kina mpaka kufikia uamuzi wa kuleta ndege hii na nyingine zitakazofuatia.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 21, 2012

    "Ndege hiyo itafanya safari za kila siku Dar-Kilimanjaro-Mwanza mara mbili kwa siku"!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 21, 2012

    Jamani kila mtu anafurahi kuona ATC imefufuka! tunaomba watu wafanye kazi kwa kujituma na moyo mmoja wa kutumikia nchi! ushauri umetolewa, kuacha undugunization, kupanda ndege kwa mkopo! na pia tunasikia kindege kimoja wafanyakzi 800 kulikoni? hebu fanyeni m restructure hiyo kampuni ! tupo nyuma yenu na tunataka mpaka mwakani muwe mmeshapata ndege 10

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...