Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde inaeleza kuwa Mchezaji wa Timu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam na Timu ya Taifa ya Rwanda, Patrick Mafisango (pichani) amefariki Dunia kwa ajali ya Gari alfajiri ya leo majira ya saa kumi hivi wakati akiwa njiani kurejea nyumbani kwake. 

Globu ya Jamii inaendelea kuwatafuta viongozi wa timu ya Simba ya Jijini Dar ili kupata taarifa zaidi juu ya Kifo cha Mchezaji huyo. Hivyo tuvute subira mpaka hapo Globu ya Jamii itakapo kuja na taarifa kamili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Shio ConradMay 17, 2012

    Bwana ilitoa na bwana ametwaa, kapumzike kwa amani mpendwa wetu Patrick Mafisango. Tulikupenda sana wanasimba.

    ReplyDelete
  2. R I P Patrick Mutesa Mafisango u were my model in TZ will miss u r fightness in the pitch

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 17, 2012

    Habari hizi Michu ni za kweli huyu bwana amepata ajali maeneo ya Chang,ombe akirejea nyumbani toka matembezini,kiukweli ni habari za kusikitisha sana na hakuna jinsi zaid ya kumwombea.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 17, 2012

    nimeumia sana. Umuhimu wake msimbazi ulikuwa mkubwa sana. Kiungo we2 ndo ka2toka. Nikikumbuka mechi ya juz sudan. Alicheza kwa moyo sana. Pigo kwe2 wanamsimbazi. RIP MAFISANGO

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 17, 2012

    RIP! If it was meant Return If Possible, then would have been happy! We will miss u Mafisango!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 17, 2012

    Nimesikitika sana baada ya kusikia hizi taarifa redio one, Ndugu yetu Patrick Mafisango umetangulia kapumzike kwa amani.

    ReplyDelete
  7. Mwangwitwa ChrisMay 17, 2012

    Wanamsimbazi tujipe moyo wa uvumilivu ktk kipindi hiki kigumu,R.I.P Patrick Mutesa Mafisango

    ReplyDelete
  8. Godlove NkyaMay 17, 2012

    Mafisango utakumbukwa daima kwa jinsi ambavyo ulikuwa ukihasisha wachezaji wenzako uwanjani.Ulikuwa chachu ya mafanikio ya klabu ya simba kwa msimu wa 2011-2012. R.I.P Mafisango.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 17, 2012

    Poleni mashabiki wa simba! RIP mafisango.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 17, 2012

    RIP Mafisango. Tunawapa pole familia na mashabiki na Taifa zima kwa pigo hili.
    Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 17, 2012

    rip patric mafisango

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 17, 2012

    RIP patrtic mafisango tulikupenda ila mungu kakupenda zaid

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 17, 2012

    Inauma kumpoteza mtu muhimu wana msimbazi,pumzika kwa amani mpendwa wetu!daima utakumbukwa kwa juhudi zako.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 17, 2012

    Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Pumzika kwa amani!

    ReplyDelete
  15. dah! ebwana bonge la pigo,
    Mafisango, kiungo mapafu ya mbwa, anakaba, anamalizia pasi ya mwisho kufunga...aaaahhh nimeumia sana, kiungo ana mabao 14 kwa ligi za huku africa? dah, basi bwana, ila mafisango..ni pengo kubwa.
    daaahhh pumzika kaka, tunashukuru kwa mchango wako kaka.

    ReplyDelete
  16. dah mafisango?? aahhh ebwana nimeumia mnoo..kiungo mapafu ya mbwa, kila kona ya uwanja yupo, ball control ya kufa mtu, kiungo mabao 14? dah ebwana hata siamini ila aahh PUMZIKA SALAMA KAKA, ila mchango wako ni mkubwa mno, dah pumzika kaka wengine tunafuata.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 17, 2012

    Nami ninapenda kuchukuwa nafasi hii kuwapa pole wapenzi wa Simba na ndugu na marafiki wa Rwanda na wazazi wake huyu ndugu yetu Patrick.
    Ni kwamba mtu akifa kumbukumbu yake imefungwa hivyo hatuwezi kusema tunamwombea maana Mungu ameishafunga record zake na hakuna kitakachobadilishwa tena kwa sasa na Mungu. So naungangana na wana ndugu wote kusema poleni simba na wazazi na ndugu wa karibu kuwapa pole kwa msiba huu. Mungu awasafirishe salama kwenda kumpumzisha huyu mpendwa wetu.
    Amina

    ReplyDelete
  18. RIP umeondoka kipindi kibaya zaidi. kwani tulikuhitaji msimbazi tusheherekee karibu mwaka mzima ubingwa ulichangia kuuleta msimbazi mwaka huu...... tutakukumbuka daima.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 17, 2012

    Lahaulah, mungu ameweka mahali pema peponi, kwa muda mfupi Mafisango aliiweka Tanzania katika daraja la juu la soka katika Afrika licha ya kwamba alikuwa ni raia wa kigeni.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 17, 2012

    mungu amrehemu ila jamaa alikuwa anakifaa cha nguvu ...si mchezo alikuwa nakitumia kisawasawa inaelekea

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 17, 2012

    rest in peace... bongo watu wataendelea kufa kila kona na kila siku na tutaendelea kumsingizia mungu hali ikijulikana kuwa ni tararibu mbovu na usalama uliozezeta wa taifa zima

    huku ughaibuni hii nchi ninayoishi tunaweza kukaa hata miezi 6 tukaona kwenye habari mtu mmoja labda amepata ajali.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 17, 2012

    R.I.P Patrick,huyu jamaa nilimwona akicheza mara moja tu Uwanja wa Taifa Simba na Setif.Mpira alikuwa 'anaujua'.Pole wachezaji wa simba,mashabiki wa Simba,familia,ndugu jamaa na Marafiki.

    David V(Yanga)

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 17, 2012

    Ukipendacho wewe na M-Mungu na yeye anakipenda vilevile

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 17, 2012

    Mafisango umetutangulia na Roho yako ipumzike kwa amani. Amen

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...