Samahani sana Anko, naomba uweke hii hoya yangu kwenye libeneke lako ili niweze ku-share mawazo yangu na watanzania wenzangu popote walipo. Nimeshindwa kuvumilia kukaa na mawazo haya moyoni mwangu kutokana na jinsi hali ya Muungano wetu inavyojadiliwa na kuhusishwa na Katiba mpya ambayo mchakato wake umeanza kushika kasi.
Kama alivyowahi kusema Mh. Zitto “idadi ya wapinga muungano inazidi kuongezeka siku hata siku. Ukiwauliza kwa nini hawataki muungano wanasema aah, basi tu. Kama ni Mzanzibari atasema Tanganyika wanatutawala. Kama ni Mtanganyika atasema Wazanzibari wamezidi kelele, tunataka Tanganyika yetu. Lakini ni lazima tuurekebishe Muungano huu. Ulivyo sasa utavunjika tu. Kuulinda muungano ni kuufanyia marekebisho makubwa”.
Kusema kweli hoja yangu kubwa iko hapa, na inatokana na sababu kubwa mbili zinazofanya nikose imani kabisa na wanasiasa wetu. Moja, ni hii tabia ya wanasiasa wengi kutosema ukweli kuhusu kwanini wazanzibari wengi hawataki muungano. Sijui kama ni kweli kwamba hawajui wazanzibari wanalilia nini hasa? au hawajafanya utafiki wa kutosha kujua kwanini wazanzibari wengi wanapinga huu muungano?
Jamani, tatizo kubwa la wazanzibari si udini kama baadhi wanavyodhani, si wabara wanaoishi au kufanyakazi Zanzibar, si wakristo wanaopenyeza ukristo Zanzibar, si uwiano wa nafasi za ajira katika taasisi na mashirika ya umma, na wala si mafuta kama wengine wanavyofikiria. Haya na mengine ambayo sikuyataja ni geresha tu, ila shida kubwa ya wazanzibari ni UTAIFA.
Wazanzibari wanaona kwamba kuwa kwao ktk muungano kumeua kabisa nchi yao. Wanataka wajulikane na mataifa mengine kama nchi. Wanaamini wakijulikana kama nchi na mataifa mengine watapata fursa nyingi ambazo wamekuwa wakizikosa kwa kuwa ndani ya muungano.
Tena ukiongea na wazanzibari kuhusu marekebisho ya muungano, watakwambia wanataka muungano kama wa nchi za Ulaya au kama ule wa EAC (shirikisho) ambapo kila nchi inajulikana kama nchi ndani ya muungano.
Kwa hiyo shida kubwa ya wazanzibari iko hapa! Na ukitaka kutimiza kiu ya wazanzibari maana yake utavunja muungano wa sasa (kitu ambacho serikali ya JK haiku tayari kukiona), halafu sasa ndo mkae mjadili kuhusu hilo shirikisho.
Sababu ya pili ya msingi wa hoja yangu, ni kuhusu marekebisho ambayo wanasiasa wetu wanapendekeza yafanyike ili kuulinda muungano. Kusema kweli hapa ndo nachoka kabisa, maana mapendekezo yao mengi yanaangalia zaidi maslahi yao binafsi na ya vyama vyao kuliko wananchi wanaowaweka katika madaraka.
Wabara wengi, Chadema, CUF n.k wanaamini kwamba hoja ya kuwa na serikali tatu ndo itakuwa suluhisho la matatizo ya muungano. Binafsi nasita kuamini hilo kwa sababu hoja ya serikali tatu itakuwa haijategua kitendawili cha utaifa wa wazanzibari, hivyo wataendelea kuupinga tu muungano.
Kwa maana hoja hii itakuwa ni mzigo bure kwa serikali katik kuziendesha hizi serikali tatu, na utakuwa ni ufujaji wa pesa za walipa kodi. Isitoshe ni hoja yenye kulenga kuwapa ulaji wanasiasa kwa kuwatengenezea nafasi nyingi za kisiasa.
Ngoja nimalizie hoja yangu kwa kutoa angalizo. Mchakato wa katiba mpya umeanza. Serikali imeishaahidi kuwa itahakikisha mchakato unamalizika kwa wakati ili katiba mpya iweze kutumika katika uchaguzi mkuu ujao.
Hizi zinaonekana kama habari njema sana kwa vyama vya upinzani na watanzania kwa ujumla ambao wamekuwa wakilalamikia mapungufu yaliyomo katika katiba ya sasa katika kuhakikisha demokrasia ya kweli inatendeka katika kuchagua viongozi wetu wa kisiasa.
Lakini nyuma ya pazia kuna hili! Watu binafsi, vyama vya siasa, na taasisi mbalimbali vinashauri baada ya kuandaa rasimu ya katiba mpya basi ipelekwe kwa wananchi kupigiwa kura ya maoni (referendum). Huu ni ushauri mzuri lakini kutokana na hali ilivyo nashawishika kusema uchaguzi ujao unaweza kufanyika kwa kutumia katiba ya zamani, unajua kwanini?
Kuna kila dalili kuwa wananchi wengi hasa wa Zanzibar hawawezi kupitisha rasimu ya katiba mpya ambayo haitatambua utaifa wao. Kwa maana hiyo kuna uwezekano mkubwa wa katiba mpya kukataliwa na wananchi. Je hali hii ikitokea itakuwaje? Kumbuka uchaguzi mkuu utakuwa umekaribia, je itabidi rasimu ikafanyiwe marekebisho kwanza halafu irudi tena kwa wananchi kupigiwa kura ndo uchaguzi ufanyike?
Au itabidi uchaguzi ufanyike tu kwa katiba ya zamani? Au je itabidi serikali iliyopo madarakani iendelee tu hadi katiba mpya itakapopatikana ndo uchaguzi ufanyike?
Wadau nawasilisha!
hapa sina comment ndugu yangu, umefanya utafiti wa kweli, na hayo yote uliyoyasema yapo juu ya mstari...
ReplyDeleteIna ingia akilini kua viongozi hawayaoni hayo, uliyoasema au wanayachukulia ni mambo ya kupita hawafanyi kua kuna mkazo na kujua ni wajibu wao kufanya ina shangaza sana kuona usomi wao ni wa fikra finyu na sijui vigezo gani vinawafikisha ngazi za juu kushindwa kuamua maamuzi mengine ni rahisi yakitiliwa umuhimu,kiukweli viongozi ndio wenye kuleta tafrani maana ni very slow kutimiza majukumu badala yake wanachosubiri ni watu toka nje waje watoe ushauri na waufate hata kama hauendi na watachokikata wengi,I agree your dead right.
ReplyDeleteMatatizo makubwa yaliyozuka ktk nchi yetu siku za karibuni ni mtu au vikundi vya watu wachache kuwasemea wengine ktk masuala mabali mbali.
ReplyDeleteImekua jambo la kawaida kusikia watu wachache mfano; wanaharakati, magazeti, NGOS na hata vyama vya siasa vyenye uwakilishi mdogo wakisema" Wtza au W'bari wanataka hivi au hawataki vile".
Kitu cha kujiuliza hapa ni, wanatumia vigezo gani kuyasema haya? ukweli ni kwamba: jumla ya wanachama wa vyama vote vya siasa, na watumiaji wa vyombo vyote vya habari ni sehemu ndogo tu ya Watza.
Lakini kubwa zaidi hapa ninaloliona, kama nilivyosema wiki iliyopita kwenye hoja ya Zitto ni kwamba; wengi kati ya "VIHERE HERE" wa kuvunja muungano wanaangalia maslahi yao binafsi.
Mfano kuna Mz'bari hajawahi kufika bara hata siku moja, hana asili wala jamaa ndugu zake wengi wapo Uarabuni. hivyo haoni haja ya muungano.
Vile vile kuna Mtanganyika hajawahi kufika Z'bar hana ndugu wala maslahi yoyote, ndugu zake wengi wapo nchi jirani, haoni haja ya muungano.
Sasa tuwauliulize wanaoshabikia hayo wanaangalia pia maslahi ya wenzao ambao walikua 'disavantaged' upande mmmoja wa jamuhuri na kufaidika upande mwingine au ndio shauri yao?
Mimi natahadharisha, ktk nchi yetu kuna JAMII na MAKABILA yanajifanya bora kuliko wenzao na ndio wanaoshabikia haya si uzalendo wala nini wajue hii 'ngoma' ikidata haitaishia hapo na wao hawabaki salama!..tutagawana mao sana!
Mdau ingawa unasema wanasiasa hawajafanya utafiti.. sina uhakika kama wewe umefanya utafiti.. unaposema Wazanzibari au wantanganyika "wengi".. maana ya "wengi" ni wangapi? wewe umeongea na wangapi ili tulinganishe na idadi ya wakazi.. huenda hata hujaongea na watu 100. Utafiti pekee unatakiwa uwe umehusisha kati ya 10% hadi 20% ya idadi ya wakazi wa eneo husika, ndipo unaweza kutoa hitimisho. Mengi ya tunayoongea ni kutokana na watu wachache tuliowasikia au kuongea nao.
ReplyDeleteMtoa Hoja ya Haja unaelewa nini Wazanzibari wanataka "UTAIFA". Sinashaka, wale wote wanaobeza hili iko siku wataungana na kilio cha wazanzibari cha UTAIFA WAO na kuachana na dhana potofu zinazojaribu kubeza hili jambo. kwani hili sio jipya katika dunia hii yameshatokea na yataendelea kutokea na hakuna wa kuzuwiya lisitokee.
ReplyDeleteTaifa la Zanzibar ndio dira ya wazanzibari.
Mdau nakuunga mkono 100%. Dhana kubwa ya falsafa ya Mwalimu Nyerere, Kwame Nkrumah na Sekou Toure ni kuwa baada ya nchi za Kiafrika kupata 'uhuru wa bendera', ili Afrika iwe ni bara imara ni lazima nchi zetu za Afrika ziungane. Mpaka sasa, Muungano wa Tanzania ndio muungano pekee uliofanikiwa katika Afrika nzima. Lakini tusiishie hapo. Hatua itakayofuate ni kuunganisha Afrika ya Mashariki na Afrika kwa jumla. UFUMBUZI: Mfumo wa Muungano wetu utazamwe vizuri na kufanyiwa marekebisho stahili. Of course tunajua kuwa kuna watu wanaotumiwa na mijitu yenye siasa kali ambayo inatumia dini zetu (Uislamu na Ukristo) kutaka kutusambaratisha. Mijtu hiyi kwa upande wa Waislamu ni mawahabi wenye kuvaa suruali na kanzu fupi na kufuga madevu machafu na kwa upande wa Wakristo ni madhehebu kama tano za kilokole (kama wale wachungaji sita waliokiri kuhusika na kuingiza heroin na cocaine Zanzibar ili kuhujumu Waislamu). Huu si wakati wa jazba. Huu ni wakati wa kutumia busara na kufikiria kistratejia. Mungu ibariki Afrika. J. Mosha, Arusha.
ReplyDeletetatizo sio utaifa kama watu wanavyosema kwani kuna watu wamenufaika na utanzania kutoka zanzibar,tatizo ni ubinasfi ambao umetawala mion mwao watu ndio wanaopekea kuitaji utaifa wa uzanzibari.je utaifa utafanya wananchi wapate elimu bora,makazi bora,maisha bora?tuache ubinafsi na mahitaji ya mipaka ya wakoloni,tuwe na fikira juu ni jinsi gani wananchi wetu wa zanziba na bara watakuwa na makazi bora,maisha bora na elimu bora
ReplyDeleteKwa idadi ya Wazanzibari ilivyo ndogo UTAIFA una manufaa makubwa kwao kuliko hivi sasa. Kwa mfano mdogo tu wanakosa fursa nyingi kwa kukataliwa kujiunga na OIC ikiwemo mikopo isiyo na riba, nafasi za investments na hata za kielimu. Hata mimi ningekuwa Mzanzibari ningetaka UTAIFA kwani kiukweli wamebanwa tuache kuzuga zuga hapa. Tuwaruhusu wajiunge na OIC uone kama hizi kelele hazitapungua.
ReplyDeleteMdau wa 01 Juni, 09:51:00 AM 2012, mvurugano (muungano) huu umedumu kwa miaka 48, si kwasababu ni mzuri au vipi, ila ni kwasababu hauna 'mfumo' wenye kueleweka na umekuwa unalindwa na 'madikteta'. Vinginevyo, usingefika hata miaka 10 tangu kuzaliwa kwake! Nikikuuliza wewe, uniambie ni aina gani ya muungano,tunayoifuata; Federation, confederation n.k? Basi utashindwa kunipa jibu. Imefikia hatua hadi watu wengine(nikiwemo mimi binafsi), kushangaa kwamba, pamoja na mapungufu na matatizo yote yanayoukumba "mvurugano' huu, lakini bado umeweza kudumu hadi leo!
ReplyDeleteJuhudi za kuunusuru mvurugano huu, zimekuwa zikifanyika tangu miaka ya 90, kwa kuunda Kamati na Tume mbali mbali, kwa upande wa SMZ na SMT, lakini mpaka leo, hakuna kilicho-prove success! Kwaiyo, inaonekana dawa ya kumaliza kero za mvurugano huu, ni KUUVUNJA TU. Kama kutakuwa na haja ya kuungana, basi tutaungana kwa heshima na taadhima! Na kama hakuna haja hiyo, basi tutaendelea na maisha kama kawaida.
Tatizo la waZanzibari (kama alivyosema Muandishi wa makala), si dini wala si makabila, bali ni MUUNGANO tu. Serikali ya Tanganyika (iliyojificha kwenye kivuli cha jina la 'Tanzania'), imekuwa ikiibana Znz, katika kila nyanja, hususan kwenye zile taasisi ambazo ni 'sensitive ones', na ambazo zinaifanya 'nchi' ihesabiwe kama nchi! Kuwa na serikali ya SMZ(kama ambavyo waTanganyika wengi wanalalamikia), ni 'kiini macho' tu. Ile ni serikali ambayo haina mamlaka hata ya kujiamulia mambo yake yenyewe. Ikitaka kufanya chochote kile, hata kama kipo nje ya mvurugano, inabidi ipate 'ridhaa/kibali' kutoka kwa 'watawala' wetu Tanganyika.
Tafadhili, waTanzania msitupotezee malengo yetu, tunachokitaka sisi waZanzibari ni'ZANZIBAR YETU HURU'!!!
Kusema ukweli mchangiaji hoja hujasema vibaya ila kwanini swala la muungano halirekebishwi?na mie kwa upande wangu nalaumu sana viongozi wetu na c wat wala waz wote ni ndugu ttz Upo kwenye mijitu inayojali hali zao tu
ReplyDeleteMimi naomba neno Moja tu. Jina la Tanganyika lirudishwe kwenye katiba mpya.
ReplyDeleteJina la Tanzania ni la kubuni tu ndio maana halina mashiko.
Jina lenye Mashiko na Mafanmikio kwa nchi yetu ni Tanganyika.
Majina ya kubuni huwa hayana nguvu yoyote. Majina yaliyoibuka yenyewe kutoka asili ndiyo yanakuwa na mafanikio.
Ahsante
namunga mkono na miguu yangu toke aliye toa madaa hii, kwamba sisi wazanzibar tunachokitaka ni KUTABULIKA KWA UTAIFA WETU PERIOD, you are very right man,wanaosema bla bla na poroja za vijiweni waache wasema mwisho watachoka,ngoma hii si ndogo na hatoisha leo itakesha kila leo mpaka kijulikana kibichi au kipevu.
ReplyDeletealiyetoa comment wa mwisho kaniwacha hoi eti ubinafsi, eti utaifa utafanya wanachi wapate elimu bora,makazi bora na maisha bora, OF COURSE, JAPO KUWA ITAKUWA JITIHADI YAKO NA SERIKALI YAKO OF COURSE BILA YA UTAIFA UTAYAPATA WAPI HAYA YOTE, NAONA SOMO LA CIVIC NA HISTORY HULIJUI WEWE BORA NENDA KASOME NA USOME VIZURI HISTORY YA ZANZIBAR HALAFU UJE UTOE HOJA YA HAJA YAKO SAWA BWANA MDOGO.
ALIYESEMA WAISLAMU WANA VAA NGUO VUPI NA KUFUGA NDEVU CHAFU SI DHANI KAMA ZIMO KAMA KWELI YEYE NI MFUASI WA BWANA WAKE WA BINGUNI,JE HAKUWA NA NDEVU JE ALIKUWA AKIVAA MAVAZI GANI,WACHA HIZO KASUMBA ZA WAKOLONI WAKO WAZUNGU WALIOKUJENGEA HISIA YA KUVAA SUIT AND TIE NA KUNYOA NDEVU,
DUME DUME LA KWELI LA BENGU BASI ANA KUWA NA NDEVU TOKA ENVI HIZO KATIKA MAANDIKO YOTE YA DINI,YESU ALIKUWA NAZO JE ALIKUWA MCHAFU NA PIA ALIVAA KAZU WEWE DANGANYA TOTOZ CHEKECHEA SI SISI BWANA TUMESHAELIMIKA LONG TIME NA KUSTAARABIA NDO MAANA TUNA TAKA "UTAIFA WETU"
TIZAMA HAO WATU 6 TENANI WALOKOLE WANATULETEA HIZO HEROINES HALAFU MNASEMA MNAMUOGOPA MUNGU NA MNAKUWA MAKANISANI KUABUDU WACHENI HIZO KICHAKA CHENI CHA KUJIFIJA KATIKA UJINI WENU KITAKWISHA TUTAKAPO PATA "UTAIFA WETU"
AMIN/AMEN
Viongozi wetu wamekosa upeo wa hekima. Washauri nao pia ni wa kulaumiwa kwani wamejikita zaidi na masilahi ya kibinafsi.
ReplyDeleteTuweke upande kelele za wazanzibari na wahafidhina wetu wa kitangayika.Kimantiki, sisi tunaonekana kuwadhibiti wazenji. Zaidi ya kutoa nafasi chache ktk Serikali Kuu na za masomo ktk vyuo vyetu, bila ya kutafuta sisi tunafaidika vipi kutoka ktk muungano huu, uali la msingi la kujiuliza: MUUNGANO KAMA MRADI WETU WA KISIASA, UMEWASAIDIA NINI WAZANZIBARI (Sio viongozi)?
Wakati umefika kuwacha danedane, turekebishe kwa makusudi mfumo wa Muungano wetu kwa kulaza msingi wa VIVUTIO VYA ZIADA ili waondokane na dhana ya kujitenga.
TAHADHARI WA VIONGOZI WETU: Zanzibar iliyojitenga itakua ni kensa isiyotibika, kwa hio kwa hekima (sio mabavu wala ujanja),Viongozi wetu haraka wachukue hatua madhubuti, kwani AWAKENING SPRING inanyemelea Afrika Mashariki! Wahenga wanasema: Jenga ufa kabla ukuta kuporomoka.