Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakisalimiana na mchezaji soka nyota wa Uingereza anayechezea Los angeles Galaxy ya Marekani,   David Beckham,  walipokutana uwanja wa ndege wa Heathrow jijini London Jumatano, muda mfupi kabla ya Rais Kikwete na Mama Salma kuelekea Washington DC kuhudhuria mkutano wa G8 kwa mwaliko wa Rais Barak Obama wa Marekani. Bekham ameonesha nia ya kutembelea Tanzania kama mtalii siku za karibuni na Rais Kikwete amemkaribisha kwa mikono miwili, akimhakikishia kwamba licha ya kuwa na mashabiki wengi ambao watafurahi kumuona pia atafurahia vivutio kibao vya kitalii. 
Picha na mdau Amos Msanjila

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 17, 2012

    Tunamkaribisha beckham hasa sisi washabiki wa man u.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 17, 2012

    Mhe. Raisi JK mkaribishe Tajiri Beckham aje atuchangie na sisi kwa Utalii atakao fanya kwetu!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 17, 2012

    I wish ningekutana na Beckham nimpe maelezo ya kina juu ya uzuri na vivutio vya nchi yetu Tanzania is the best of Africa.

    Kipepeo Tours

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 17, 2012

    SAFI SANA JK UKIPATA NAFASI NA ICON KAMA HAO UNAITUMIA FULLY

    KARIBU BECKHAM

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 17, 2012

    JK: Hi David, I am JK, and this is my wife Salma, I am president of Tanzania.
    DB: Hello, JK, nice to see u, Tasmania, is that an island off Australia?
    JK: No, in Africa.
    DB: Oh! sorry, is that near Kruger national park?
    JK: No, east coast.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 17, 2012

    Aje awekeze katika soka la vijana aanzishe shule angalau 1 ya soka la vijana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...