TAREHE 5 - MEI - 2012, UTAKUWA UMETIMIZA MIAKA MIWILI TANGU MWENYEZI MUNGU ALIPOKUTWAA TOKA HAPA DUNIANI. PAMOJA NA KWAMBA KIMWILI HAUPO NASI, KIROHO TUNAKUKUMBUKA DAIMA.

UNAKUMBUKWA DAIMA NA WATOTO WAKO FLORIDA, ILLUMINATA, LIBERATA, DUNSTAN, JOYCE NA EDWIN PAMOJA NA WAKWE, WAJUKUU, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI.

IBADA YA MISA YA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU MWALIMU RUTAGERUKA ITAADHIMISHWA SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 5 - MEI - 2012, KATIKA KANISA LA PAROKIA YA BIKIRA MARIA MAMA WA HURUMA, TANKI BOVU, MBEZI BEACH, DAR-ES-SALAAM, SAA 12.30 ASUBUHI.

BWANA ALITOA, BWANA ALITWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE. AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2012

    Kristu......Naomba niungane na familia katika kumbukumbu hii kama "Omwijukulu".

    David V

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2012

    Huyu mzee skumfahamu binafsi, bali nilimfahamu kupitia binti yake mmoja niliyesoma naye na hatimaye kufanya nae kazi. Kutokana na masimulizi ya huyo binti anaonekana alikuwa ni mzee mwenye busara sana. Pole sana rafiki yangu Joyce na Da Florida.
    Libe na Ilumi. Poleni sana

    ReplyDelete
  3. Babu tulikupenda sana ila Mungu alikupenda zaidi na amekuchukua ili upumzike milele, unakumbukwa sana na Wanamusibuka,wenyeji wote wa Bukoba vijijini,Bukoba mjini, Mkoa wa Kagere na Tanzania kwa ujumla
    RAHA YA MILELE UMPE EH BWANA NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE APUMZIKE KWA AMANI AMEN
    G. Muchuruza

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 04, 2012

    Mwenyezi mungu amrehemu baba yetu mpendwa amweke mahali pema peponi. Amina.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 05, 2012

    napenda kuwashukuru wote kwa salaam hizo za upendo. Hususan namshukuru kwa dhati Kaka Michuzi kwa kurusha hilo tangazo na kulipatia nafasi kubwa na muafaka. Mungu awabariki. Mola amulaze pema peponi. Amina

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...