Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali (Mst) Joseph Simbakalia akisalimiana na Meneja wa NMB Kanda ya Kusini Bw. Thomas Kilongo huku wakishuhudiwa na Meneja wa Mahusiano Bi. Shy-Rose Bhanji wakati wa kukabidhiwa msaada wa Madawati kwa Shule za Mkoa wa Mtwara.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Joseph Simbakalia (wa kulia) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 15 kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Kusini Bw. Thomas Kilongo wakati wa kukabidhiwa msaada huo utakozinufaisha Shule za Msingi katika Wilaya za Masasi na Newala.
Meneja wa Mahusiano Benki ya NMB Bi. Shy-Rose Bhanji akitoa maelezo kwa Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kuhusiana na msaada huo na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Benki ya NMB na wananchi kwa ujumla katika kuhakikisha maendeleo ya elimu katika nchi yetu.
Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Mhe. Farida S. Mgomi akila kiapo cha utii mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Joseph Simbakalia. Wakuu wa Wilaya wengine wanne waliapishwa ili waweze kuanza rasmi kutekeleza majukumu yao ya kitaifa.
Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Mhe. Festo S. Kiswaga akipokea vitendea kazi baada ya kuapishwa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa kama ishara ya kuanza rasmi kutumikia taifa katika wadhifa wake wa Mkuu wa Wilaya
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Joseph (wa nne kutoka kulia) Simbakalia na katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bw. Yusuf Matumbo (wa tatu kutoka kushoto)wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wakuu wa Wilaya wapya walioapishwa jana. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Festo S. Kiswaga, Mkuu wa Wilaya ya Newala Mhe. Christopher E. Magala na kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe.Wilman K. Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe.Farida S. Mgomi na Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe. Ponsiano. Picha zote na Beatha Hyera, Afisa Habari Mtwara
Hivi unaweza kuwa mbunge at the same time umeajiriwa kwingine? Hapo namzungumzia Bi au Mheshimiwa Shy-Rose. Je unaweza kuwa mbunge na pia mfanya biashara?
ReplyDeleteIna. Maana ubunge aw Shyrose ni part time au?
ReplyDeleteHata mie sijaelewe, nilidhani ukishajiingiza kwenye siasa unaatakiwa kuachia mambo yako ya private sector? Je, hii sio conflict of interest? Naomba wanasheria au wadau mnaojua mnielimishe.
ReplyDeleteMdau1