Mh. James Mbatia
Mh. Janet Mbene
Uteuzi huo unaanza mara moja.
Mh. Janet Mbene
![]() |
| Profesa Sospeter Muhongo |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa wabunge watatu wapya kwa mujibu wa mamlaka ya uteuzi aliyo nayo chini ya Ibara ya 66(i) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wabunge hao wapya ni Profesa Sospeter Muhongo,
Bi. Janet Mbene na Bwana James Mbatia.
Bi. Janet Mbene na Bwana James Mbatia.
Uteuzi huo unaanza mara moja.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
3 Mei, 2012





.png)
Naona maandalizi ya kupata mawaziri wapya watakaokuwa ktk baraza la mawaziri yameshika kasi. Hongera Prof. Sospeter na Bi. Janet. Ndo kama hivyo, UWAZIRI mmeshaupata. (Huu ni mtizamo wangu lakini). Kwa Mbatia, hongera kuingia mjengoni (wewe ni wa upendeleo maalum, si kwa ajili ya uwaziri)
ReplyDeleteHongera sana Prof. Sospeter. Najua wewe ndiye Waziri wa Nishati na Madini ajaye. Hongera pia Bi. Janet, kwani wewe ndiye Waziri wa Afya ajaye.
ReplyDeleteMwaka huu tutaona na kusikia mengi.
ReplyDeleteNaona Mheshimiwa Rais amefanya kweli. Tusikilizie baraza!! Nadhani hapa atakonga nyoyo za Watanzania!! Tusubirie
ReplyDeletehapo kuna waziri wa madini, waziri wa fedha na uchumi na waziri wa uchukuzi
ReplyDeletehao wawili cv zao ni nzuri sana sijui huyu mbatia
Mawaziri wapya hao inaonekana....
ReplyDeleteHongera mheshimiwa rais wetu mpendwa,..kwa kuteua watu makini na wazalendo bila kijali chama
ReplyDeleteHureeeeeee! Profesa Muhongo!!!! Hakika hicho ni kifaa. Ni bingwa wa jiolojia katika Afrika na dunia. Huyu anaweza kuifaa sana Serikali, hasa ikizingatiwa kuwa hawezi kudanganywa na wezi wa madini yetu. Kila kitu anakijua. Namtakia kila la heri na Baraka tele. Akishirikiana na Kafumu, watafumua kila kitu.
ReplyDeleteSafi sana. Tunamuambea Mwenzi Mungu ampe hekima kwa hili na amfungulie njia iliowazi na yenye kheri na yeye, Kila mwenye nia mbaya Mwenzi Mungu aiangamize nia yake. Inshallah.
ReplyDeleteYametimia. Kuna watu hapo watateuliwa kuwa mawaziri kwenye baraza jipya. Ngoja tusubiri.
ReplyDeleteWalete waleteee......Prof.Muhongo kila la heri tumeshanusa damu unakoelekea...Kila la heri Prof.
ReplyDeleteDavid V
Hongera sana wabunge wateule. Bwana michuzi, napendekeza utuwekee CV zao tafadhali.
ReplyDeleteHaya naona maandalizi ya baraza jipya la mawaziri yameanza....!!
ReplyDeleteFanya kweli mheshimiwa,wakati unakwenda..
ReplyDeletehongereni nyote mliochaguliwa Mungu awatangulie katika majukumu yenu.
ReplyDeleteMore on Profesor Sospeter Muhuho
ReplyDeleteHawawezi kuwa mawaziri mpaka waapishwe kuwa wabunge. Itamlazimisha rais kuitisha kikao cha bunge ili kuwaapisha hawa wateule wake kama anataka kuwapa uwaziri ktkt baraza lake jipya tunalolitegemea.
ReplyDeleteMama Janet Mbene ni kichwa ila Wah walimpiga chini kwenye ubunge wa Afrika Mashariki - wakaamua kuchukua baadhi ya vilaza na kuwapa kura nyingi. Wakachukua wale ambao akili imeshachakachuliwa na hongo!! AIBUUU!!
ReplyDeleteJAMANI EEH MDINI NANI, AU HAPA IMEKAA VIZURI?? JENDA, UKANDA NA NANIHII...JE?? KAKA MISUPU HII USIITIE KAPUNI...
ReplyDeleteduh mkullo na ngeleja kwishnei......hapo naona tumeshapata waziri wa nishati na madini pamoja waziri wa fedha.mbatia wewe umepewa tu ili uingie mjengoni ukaongeze kasi ya kuikaba koo serikali.wewe sio uwaziri tafadhari usije ukaanza shona suti ya kuapishiwa.
ReplyDeleteEagerly awaiting the cabinet now.
ReplyDeleteProf. Muhongo anajulikana kwa kutotaka kabisa rushwa na kazi za blabla.
ReplyDeleteTena hapendi kabisa watu vilaza, wezi wa mitihani na wezi wa mali ya Taifa.
Ingekuwa uwaziri Mkuu unajaribiwa, basi rais amjaribu tu kwa probation ya six month utasikia mziki wa Prof. Sospeter katika Wizara zote. Wote tutamkubali. Namkumbuka huyu don pale mlimani na pia alipoanzisha ICSU- Bondeni kwa Madiba.
Kama Kikwete Ataamua kuweka wapinzani ktk Serikali Nawaomba CHADEMA Wasikubali kuwamo. Upinzani utakuwa Umekufa Itakuwa kama CUF Na CCM Zanzibar Tafadhali CHADEMA tubaki kuwa Wapinzani
ReplyDeletemi nasubiri dk Slaa aanze kuwatoa kasoro hao jamaa.
ReplyDeleteHongereni sana. Mungu awalinde katika kazi yenu mpya!
ReplyDeleteHIVI INAWEZEKANA WATEULE HAWA KUWA MAWAZIRI KABLA HAWAJAAPISHWA RASMI KUWA WABUNGE KATIKA MKUTANO UJAO WA BUNGE?
ReplyDeleteNDO KUSEMA BARAZA JIPYA LITATANGAZWA MWEZI UJAO?
TUSUBIRI TUONE.
TUNAOMBA CV ZAO TAFADHALI NA WANATOKA WAPI WALIKOKUWA
ReplyDeleteWANAFANYA KAZI. HILI NI MUHIMU SANA.
HONGERA SANA KWA MABADILIKO
Hongereni sana wateuliwa kwani Mungu huwajua watu wake na wenye haki wataishi kwa haki ya Mungu. Hongereni sana.
ReplyDeleteAnkal, nimebahatika kuwajua hawa wabunge wateule watatu kwa mbali au kwa karibu. Auntie Janet ni rafiki ya familia. Nilishiriki katika kampeni ya Bw Mbatia 2010 na mjomba wangu aliwahi kufanya kazi chini ya usimamizi wa Prof. Muhongo. Hawa wote watatu ni watu wa busara na wachapakazi wenye sifa ya uongozi. Natumai hili litakuwa fundisho kwa mawaziri wabadhirifu na mafisadi na nchi yetu itafungua ukurasa mpya katika utawala bora. Kweli Mheshimiwa JK umefanya kweli.
ReplyDelete"Mcheza kwao hutuzwa". Pongezi kwa Prof. Sospeter Muhongo. Professor amekuwa consultant kimataifa kwa miaka mingi, sasa zamu yetu Tanzania "kufaidika" na usomi ni kipaji chake. Hali kadhalika, Janet Zebedayo Mbene amekuwa mshauri wa mashirika mengi ya kimataifa ikiwemo EAC. Huu ni mwanzo mzuri Mheshimiwa Rais Kikwete.
ReplyDeleteKwa maoni yangu, suala sio uwezo wa mtu binafsi, bali ni utashi wa kisiasa wa wanoendesha nchi. Huo professor anaweza akaja na mapendekezo mapya mia mbili tisini, lakin kama hakuna utashi wa kisiasa, hakuna hata pendekezo moja litatekelezwa. Honereni kwa mlioteuliwa
ReplyDeleteFrancis
Mnadhani cv ndo inachapa kazi!Mbona hamjifunzi nyie,kwani waliomo katiak baraza hawana cv?
ReplyDeleteMnaotaka CV use google...
ReplyDeleteHongera sana Mheshimiwa Mbatia binafsi nakukubali.