Mh. James Mbatia
                                                                 Mh. Janet Mbene 
Profesa Sospeter Muhongo 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa wabunge watatu wapya kwa mujibu wa mamlaka ya uteuzi aliyo nayo chini ya Ibara ya 66(i) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wabunge hao wapya ni Profesa Sospeter Muhongo, 
Bi. Janet Mbene na Bwana James Mbatia.


Uteuzi huo unaanza mara moja.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
3 Mei, 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2012

    Naona maandalizi ya kupata mawaziri wapya watakaokuwa ktk baraza la mawaziri yameshika kasi. Hongera Prof. Sospeter na Bi. Janet. Ndo kama hivyo, UWAZIRI mmeshaupata. (Huu ni mtizamo wangu lakini). Kwa Mbatia, hongera kuingia mjengoni (wewe ni wa upendeleo maalum, si kwa ajili ya uwaziri)

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 03, 2012

    Hongera sana Prof. Sospeter. Najua wewe ndiye Waziri wa Nishati na Madini ajaye. Hongera pia Bi. Janet, kwani wewe ndiye Waziri wa Afya ajaye.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 03, 2012

    Mwaka huu tutaona na kusikia mengi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 03, 2012

    Naona Mheshimiwa Rais amefanya kweli. Tusikilizie baraza!! Nadhani hapa atakonga nyoyo za Watanzania!! Tusubirie

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 03, 2012

    hapo kuna waziri wa madini, waziri wa fedha na uchumi na waziri wa uchukuzi
    hao wawili cv zao ni nzuri sana sijui huyu mbatia

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 03, 2012

    Mawaziri wapya hao inaonekana....

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 03, 2012

    Hongera mheshimiwa rais wetu mpendwa,..kwa kuteua watu makini na wazalendo bila kijali chama

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 03, 2012

    Hureeeeeee! Profesa Muhongo!!!! Hakika hicho ni kifaa. Ni bingwa wa jiolojia katika Afrika na dunia. Huyu anaweza kuifaa sana Serikali, hasa ikizingatiwa kuwa hawezi kudanganywa na wezi wa madini yetu. Kila kitu anakijua. Namtakia kila la heri na Baraka tele. Akishirikiana na Kafumu, watafumua kila kitu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 03, 2012

    Safi sana. Tunamuambea Mwenzi Mungu ampe hekima kwa hili na amfungulie njia iliowazi na yenye kheri na yeye, Kila mwenye nia mbaya Mwenzi Mungu aiangamize nia yake. Inshallah.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 03, 2012

    Yametimia. Kuna watu hapo watateuliwa kuwa mawaziri kwenye baraza jipya. Ngoja tusubiri.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 03, 2012

    Walete waleteee......Prof.Muhongo kila la heri tumeshanusa damu unakoelekea...Kila la heri Prof.

    David V

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 03, 2012

    Hongera sana wabunge wateule. Bwana michuzi, napendekeza utuwekee CV zao tafadhali.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 03, 2012

    Haya naona maandalizi ya baraza jipya la mawaziri yameanza....!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 03, 2012

    Fanya kweli mheshimiwa,wakati unakwenda..

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 03, 2012

    hongereni nyote mliochaguliwa Mungu awatangulie katika majukumu yenu.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 03, 2012

    Hawawezi kuwa mawaziri mpaka waapishwe kuwa wabunge. Itamlazimisha rais kuitisha kikao cha bunge ili kuwaapisha hawa wateule wake kama anataka kuwapa uwaziri ktkt baraza lake jipya tunalolitegemea.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 03, 2012

    Mama Janet Mbene ni kichwa ila Wah walimpiga chini kwenye ubunge wa Afrika Mashariki - wakaamua kuchukua baadhi ya vilaza na kuwapa kura nyingi. Wakachukua wale ambao akili imeshachakachuliwa na hongo!! AIBUUU!!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 03, 2012

    JAMANI EEH MDINI NANI, AU HAPA IMEKAA VIZURI?? JENDA, UKANDA NA NANIHII...JE?? KAKA MISUPU HII USIITIE KAPUNI...

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 03, 2012

    duh mkullo na ngeleja kwishnei......hapo naona tumeshapata waziri wa nishati na madini pamoja waziri wa fedha.mbatia wewe umepewa tu ili uingie mjengoni ukaongeze kasi ya kuikaba koo serikali.wewe sio uwaziri tafadhari usije ukaanza shona suti ya kuapishiwa.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 03, 2012

    Eagerly awaiting the cabinet now.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 04, 2012

    Prof. Muhongo anajulikana kwa kutotaka kabisa rushwa na kazi za blabla.

    Tena hapendi kabisa watu vilaza, wezi wa mitihani na wezi wa mali ya Taifa.

    Ingekuwa uwaziri Mkuu unajaribiwa, basi rais amjaribu tu kwa probation ya six month utasikia mziki wa Prof. Sospeter katika Wizara zote. Wote tutamkubali. Namkumbuka huyu don pale mlimani na pia alipoanzisha ICSU- Bondeni kwa Madiba.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 04, 2012

    Kama Kikwete Ataamua kuweka wapinzani ktk Serikali Nawaomba CHADEMA Wasikubali kuwamo. Upinzani utakuwa Umekufa Itakuwa kama CUF Na CCM Zanzibar Tafadhali CHADEMA tubaki kuwa Wapinzani

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 04, 2012

    mi nasubiri dk Slaa aanze kuwatoa kasoro hao jamaa.

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 04, 2012

    Hongereni sana. Mungu awalinde katika kazi yenu mpya!

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 04, 2012

    HIVI INAWEZEKANA WATEULE HAWA KUWA MAWAZIRI KABLA HAWAJAAPISHWA RASMI KUWA WABUNGE KATIKA MKUTANO UJAO WA BUNGE?

    NDO KUSEMA BARAZA JIPYA LITATANGAZWA MWEZI UJAO?

    TUSUBIRI TUONE.

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 04, 2012

    TUNAOMBA CV ZAO TAFADHALI NA WANATOKA WAPI WALIKOKUWA
    WANAFANYA KAZI. HILI NI MUHIMU SANA.
    HONGERA SANA KWA MABADILIKO

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 04, 2012

    Hongereni sana wateuliwa kwani Mungu huwajua watu wake na wenye haki wataishi kwa haki ya Mungu. Hongereni sana.

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 04, 2012

    Ankal, nimebahatika kuwajua hawa wabunge wateule watatu kwa mbali au kwa karibu. Auntie Janet ni rafiki ya familia. Nilishiriki katika kampeni ya Bw Mbatia 2010 na mjomba wangu aliwahi kufanya kazi chini ya usimamizi wa Prof. Muhongo. Hawa wote watatu ni watu wa busara na wachapakazi wenye sifa ya uongozi. Natumai hili litakuwa fundisho kwa mawaziri wabadhirifu na mafisadi na nchi yetu itafungua ukurasa mpya katika utawala bora. Kweli Mheshimiwa JK umefanya kweli.

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 04, 2012

    "Mcheza kwao hutuzwa". Pongezi kwa Prof. Sospeter Muhongo. Professor amekuwa consultant kimataifa kwa miaka mingi, sasa zamu yetu Tanzania "kufaidika" na usomi ni kipaji chake. Hali kadhalika, Janet Zebedayo Mbene amekuwa mshauri wa mashirika mengi ya kimataifa ikiwemo EAC. Huu ni mwanzo mzuri Mheshimiwa Rais Kikwete.

    ReplyDelete
  30. Kwa maoni yangu, suala sio uwezo wa mtu binafsi, bali ni utashi wa kisiasa wa wanoendesha nchi. Huo professor anaweza akaja na mapendekezo mapya mia mbili tisini, lakin kama hakuna utashi wa kisiasa, hakuna hata pendekezo moja litatekelezwa. Honereni kwa mlioteuliwa

    Francis

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 04, 2012

    Mnadhani cv ndo inachapa kazi!Mbona hamjifunzi nyie,kwani waliomo katiak baraza hawana cv?

    ReplyDelete
  32. Malaika, GroningenMay 04, 2012

    Mnaotaka CV use google...
    Hongera sana Mheshimiwa Mbatia binafsi nakukubali.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...