Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar amezindua rasmi programu ya kiswahili inayofundishwa na Chuo Kikuu cha Indiana. Porgramu hii (ya kufundisha Kiswahili)ni ya kwanza nchini Marekani ambapo wanafunzi wanaosoma Kiswahili wanapata ufadhili kutoka Serikali Kuu ya Marekani. Wanafunzi hao pia watapata fursa ya kusoma Chuo Kikuu cha Zanzibar kwa mwaka mmoja kama sehemu ya programu hiyo.
Pichani Balozi Maajar akipongezwa mara baada ya kumaliza hotuba yake iliyoelezea historia ya Kiswahili nchini Tanzania na kazi kubwa iliyofanyika ya kukuza Kiswahili na kuunganisha Taifa. Hotuba hii ilipokelewa vizuri sana ambapo pia ilielezea pia ilielezea umuhimu wa wanafunzi wa Kimarekani kujifunza Kiswahili. Pichani umati wa wageni wakimsindikiza Balozi Maajar kwa makofi huku wamesimama.



HII nimeipenda, huyu mama aendelee na kuchapa kazi.
ReplyDeleteMwenye enzi akuzidishie ndugu yangu Alwiya oh. I mean Prof. congratulations
ReplyDeleteSafi sana. Hii ina maana sasa Kiswahili kinafundishwa katika vyo vikuu zaidi ya 400 duniani na kutangazwa na vituo vya redio zaidi ya 70 nje ya TZ (vikiwemo VOA, BBC, FRI, Deutschewelle, All India Radio, Radio Misri, China, Urusi, Kongo, Kenya, n.k.). Shaaban Robert alisema "Titi la mama tamu, lingine haliishi hamu". Pia pongezi kwa Balozi Mwanaidi.
ReplyDeleteNini faida lakini ya kueneza Kiswahili? Uchumi wa nchi yetu waweza kukua kwa kufanikiwa kupata vyuo vingi kunakofundishwa Kiswahili, au vituo vya habari kunakotangazwa Kiswahili? Mimi nadhani Kiswahili kinaweza kutusaidia kuinua uchumi wetu kama tutafundisha wanafunzi wetu kwa kutumia Kiswahili, ili wanafunzi waelewe masomo yao vizuri, na waweze kuwa wabunifu.
ReplyDeleteChuo kinachofundisha Kiswahili ni Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar.
ReplyDeletesisi wenyewe tukikandia kiswahili hao wanatakakukifundisha safi sana tubadirike tupende vyakwetu
ReplyDelete