Na Mwandishi wetu,Arusha

SERIKALI imetakiwa kuunda mpango wa muda mfupi utakaoweza kupunguza ugumu wa maisha kwa wananchi kutokana na mfumuko wa bei unaoendelea hivi sasa hapa nchini.

Hayo yalisemwa na Mchumi, mtafiti na mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dk. Honest Ngowi alipokuwa akiwasilisha mada kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo wananchi, yaliyokuwa yameandaliwa na Shirika la Hakikazi Catalyst la jijini hapa, yaliyowashirikisha wananchi wa ngazi mbalimbali kutoka mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara.

Dk Ngowi alieleza kuwa mfumuko wa bei unaongeza ugumu wa maisha kwa ongezeko la bei la mara kwa mara na hivyo kupunguza uwezo wa watu kununua bidhaa na huduma kutokana na mapato yao kutoongezeka, unaweza kutatuliwa kwa muda mfupi na wa kati, iwapo serikali na wad au watadhamiria kufanya hivyo.

Alisema swala muhimu ni kupunguza athari za mfumuko wa bei kwa makundi yote likiwemo la wafanyakazi kwa kuongezewa mishahara inayoendana na hali halisi ya ugumu wa maisha.

“Hii ni kwa sababu kama mfumuko wa bei unaongezeka bila kuongeza kipato cha mfanyakazi ugumu wa maisha utazidi. Suluhisho lingine ni kwa serikali kupanga na kusimamia bei za bidhaa muhimu kama vile chakula, usafiri na madawa.” Alisema.

Aliongeza kuwa njia nyingine ya kupunguza mfumuko wa bei ni serikali kutoa ruzuku kwa baadhi ya huduma na bidhaa muhimu kwani itapunguza bei anayolipa mnunuzi kwa sababu sehemu ya bei hiyo hulipwa na serikali, kama vile ruzuku inayofanywa kwa pembejeo za kilimo au vyandarua.

Akizungumzia jawabu la kudumu la mfumuko wa bei, Ngowi alisema kati ya mkakati mkubwa na endelevu wa kudhibiti mfumuko huo ni kushughulikia masuala ya kimfumo yanayosababisha mfumuko wa bei.

“Masuala haya ya kimfumo ni pamoja na kushughulikia na kutatua tatizo la umeme, miundombinu kwa maana ya barabara, madaraja na hata masoko kwa ujumla lakini sana kwa ajili ya kusafirisha pembejeo za kilimo cha mazao ya chakula na mazao yakishazalishwa,” alisema.


Alisema kuna haja pia ya kushughulikia uimarishaji wa thamani ya shilingi ili kupunguza mfumuko wa bei unaotokana na kushuka kwa thamani ya shilingi.

Mhadhiri huyo alisema suala hilo linawezekana kwa kuweka mazingira yatakayowezesha kuongeza uuzaji wa bidhaa na huduma nje ya nchi na kupunguza manunuzi yasiyo ya lazima toka nje ambayo hupunguza fedha za kigeni na kufanya shilingi kuwa dhaifu.

Kuhusu mambo ambayo serikali imefanya na kama ni sahihi, Ngowi alisema serikali kupitia Benki Kuu (BoT), imekuwa ikijaribu kupunguza mfumuko wa bei kwa kutumia sera za kifedha.

Alisema hili limefanyika kwa kupunguza fedha katika mzunguko ambayo ni njia mojawapo ya kupunguza mfumuko wa bei unaotokana na kuwa na fedha nyingi kupita kiasi katika mzunguko.

Alieleza kuwa kwa Tanzania, tatizo kubwa linalopelekea mfumuko wa bei kuongezeka sio kuwa na fedha nyingi katika mzunguko bali ni masuala ya uzalishaji na usafirishaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 02, 2012

    kingine ambacho serikali inatakiwa ni kukataza matumizi holela ya dora,kwani yamekuwa holela kiasi kwamba mpaka baadhi ya baa zinuuza bia kwa dora,mlimani city bidhaa unatajiwa bei kwa dora, then wanaconvert to T shngs kwanini kusiwena mfumuko wa bei( hapo serikali imerega)

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 02, 2012

    UTATUZI WA KITENDAWILI CHA UCHUMI:

    Vitu ambavyo ni mojawapo wa Mchawi mkubwa wa kuendelea kwa matatizo ya kiuchumi kupelekea ugumu wa Maisha (mfumuko wa bei za bidhaa hadi kupanda kwa gharama za maisha) na kudorora kwa Thamani ya Shilingi ni:

    WASIHANGAIKE SANA WATAZAME HIVI:

    1.MAFUTA/Nishati
    Hili ndio zimwi namba moja la matatizo ya kiuchumi kwa sababu, serikali imajikita sana kutafuta fedha za Kuendesha nchi kupitia Kodi ya mafuta kitu ambacho kinapandisha gharama ya kila kitu(gharama za vyakula,usafiri,nishati n.k),,,mfano Mshahara ukipanda na bei za bidhaa zote papo hapo maradufu zinapanda!.

    2.VYANZO VYA MAPATO/Sekta za Uchumi
    Tumebarikiwa kuwa na vitu vingi mno vya kuweza kupata vyanzo vya mapato na kuachana na (Uchumi unaotegemea Kodi ya mafuta pekee).

    ::::::PANA HITAJIO LA HARAKA LA KUBUNI VYANZO VIPYA VYA MAPATO (Badala ya Utegemezi ktk Uchumi wa Kodi ya Mafuta) MIONGONI MWA NEEMA LUKUKI TULIZO JAALIWA:::::

    Tulivyo barikiwa navyo:
    -Gesi asilia LNG, Hii ingechukua nafasi kubwa kwa kushusha gharama za nishati na kuondoa utegemezi wa Uchumi wa Kodi ya mafuta, kwa kubadili mifumo ya magari na mitambo kutumia gesi badala ya Mafuta.

    Mwanzoni Gas ilikadiriwa kuwepo ni 4.3 Trilion Cubic Feet (4.3 TCF), na juzi tu imepimwa imepatikana ya kufikia 7.1 Trilion Cubic Feet (7.1 TCF) Ukwasi wa ziada unaoweza kututoa ktk utegemezi wa nishati ya Mafuta.

    -Tuna Makaa ya mawe Coal, Shale stones (mawe ya nishati)

    -Uranium, tutafute njia za haraka za kuzalisha Nishati kupitia Urani ili kupunguza pengo la mahitaji ya nishati yanayozidiwa na kazi ya kukua kwa Uchumi na maendeleo.

    -Dhahabu pia imeongezeka ktk hazina iliyokadiriwa awali na sehemu nyingi sana zimegundulika kuwa na dhahabu ya kutosha, (PIA KWA NCHI YENYE AKIBA KUBWA YA DHAHABU NI MARA CHACHE KUKABILIWA NA MATATIZO KAMA YA KUSHUKA KWA THAMANI YA FEDHA KWA KUWA AKIBA YA DHAHABU HUSAIDIA KUILINDA THAMANI YA FEDHA YA NDANI)

    -Tuna Chuma (Steel), Nickel na manganese

    -Tuna Bahari na maliasili nyingi sana,

    -Sekta ya Utalii imeongezeka kwa kuchangia pato la Taifa lakini kwa kiwango hicho bado ni chini sana ukilinganisha na (Thamani ya urithi wa Utalii tuliyonayo), miaka ya nyuma hadi KENYA ambayo tumeizidi kwa vivutio ilikuwa na mapato ya Utalii kutuzidi ,lakini kwa sasa tumeizidi, lakini tunaweza kuwa na mapato mara kama zaidi ya 20 ya Kenya,,,Rekodi ya mapato ya Taifa kwa Sekta ya Utalii (MWAKA 2011) Tanzania iliingiza US$ 4.8 Billion na Kenya iliingiza US$ 1.3 Billion,,,kama tutautumia Utalii kwa tija tunaweza kupata kwa Mwakamara zaidi 20 ya pato la Kenya yaani US$ 26 Billion au zaidi.

    N.K

    HIVYO BASI ILI MAMBO KUWA, WACHUMI NA WADAU WAKISHIRIKIANA NA POLICY MAKERS NA MAMLAKA, KINACHOHITAJIKA ILI KUFANYA UTEKELEZAJI NI 'PROJECT MANAGEMENT'/ SEQUENCE OF ORDERS YAANI MLOLONGO WA UTEKELEZAJI WA MAMBO KUUNDA ILI KUFIKIA LENGO KWA KUTUMIA TULICHO NACHO KAMA HAPO JUU.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 02, 2012

    Zaidi ya hapo naendelea......

    UTATUZI WA KITENDAWILI CHA UCHUMI:

    Kulingana na mzunguko wa kiuchumi haujakaa sawa kama Profesa anavyosema ktk Makala hii ni kuwa Mfumuko wa bei unapiganiwa kupitia njia za fedha tu yaani (Monetary Policy) huko Benki kuu kwa kubana mzunguko wa fedha kitu ambacho imethibitika hakitoi matokeo yanayoridhisha.

    Yaani chungu kina mafiga matatu yasiyolingana kwa ukubwa:

    INATAKUWA KULINGANA NA MAJAALIWA TULIYO NAYO KTK RASILIMALI ZOTE MADINI NA MALI ZIWEKWE KTK MASOKO YA HISA (Stocks):

    -Gas
    -Uranium
    -Gold
    -Coal
    -Steel
    -Nickel
    -Diamonds

    Mfano, kwa Ukubwa wa Uchumi wetu kwa wingi wa Rasilimali ilitakiwa Idadi ya Stocks zilizokuwa Listed ktk DSE ziwe zaidi ya 50+ ambazo Kenya tuliowazidi ktk rasilimali Masoko yao ya hisa NSE (Nairobi Stock Exchange) wanayo.

    Kwa ukubwa wa mali zetu tulizojaaliwa ilitakiwa ile tu Activity za Masoko ya Hisa Dar (DSE) ;;;;ile trading floor;;;;;ilitakiwa iwe na ukubwa kama BOT ilivyo au zaidi !

    Tulitakiwa at least kuwa na zaidi ya 150+ Listed Companyies in the DSE !

    Yaani ( Idadi ya makampuni ya hisa yaliyoorodheshwa ktk Soko la Hisa Dar)

    MFUMO WA UCHUMI UWE NA UWIANO KWA:

    1.Financial/Money Market(Central Bank)+Capital Market(Stocks)=MONETARY POLICY

    2.House hold Expenditure(Basket)=FISCAL POLICY

    Hivyo matumizi yetu au kinachoakisi maisha ni hiyo (Fiscal Policy) na kinachotupatia kujikimu kimaisha ni hiyo (Monetary Policy)

    Hivyo Uchumi wetu utaimarika na matatizo ya Kiuchumi (Mfumuko wa bei , kupanda gharama za maisha na kushuka kwa thamani ya Shilingi) kutatulika huku(Ugumu wa maisha kuondoka na hali bora kurejea) endapo utoshelezo wa hayo hapo utapatikana kwa uwiano unaokubalika kwa mujibu wa Kiuchumi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 03, 2012

    Matatizo yetu zaidi yapo Ki Sera na kiutekelezaji na sio kihali kwa kuwa kama Mdau anavyotoa maoni hapo juu Maoni ya Pili na ya Tatu, nchi yetu imejaaliwa na vitu lukuki!

    1.Lazima tukubali kuwa tupo chini ya kiwango cha uvunaji wa rasilimali zetu (Economic Under exploitation), kama mnavyoona nchi imepata US$ 4.8 Billion kupitia njia ya Utalii na ingeweza kupata hadi US$ 26 Billion kama zitavunwa inavyostahili, pia na maeneo mengine ya rasilimali tuna vuna chini ya kiwango.

    2.Ni wazi kuwa Uchumi umeegemea kabisa ktk Uchumi wa Kifedha (Mfano Benki kuu kutatua matatizo ya mfumuko wa bei na kudhibiti kushuka kwa thamani ya fedha), Badala ya kuzingatia upande wa pili wa Uchumi wa mali kupitia Mamlaka ya Mitaji na Dhamana(CMSA) sambamba na Masoko ya hisa(DSE).

    Kama upande wa Dirisha la Ki-Fedha una ugumu, tunaweza kutokea upande wa Dirisha la Mitaji na mali tulizo jaaliwa nazo.

    -Ili mali tulizo nazo ziingie ktk kuorodheshwa Masoko ya Hisa inatakiwe zibadilishwe na kuwa ktk mfumo wa Mitaji kupitia taratibu kama standardization and Patent.

    -Ili dhahabu itumike kucheck Inflation cha Muhimu pia iwe Standardized and Patented and so on.

    Kwa hivyo kushindwa kwetu kutumia tulicho nacho kama hapo ni kama mtu kuwa na mavuno ya kuvunja ghala lakini ukashindwa au ukawa mvivu kutwanga au kukoboa mazao yako ili utengeneze chakula.

    Zipo Mamlaka nchini zinazoweza kufanya kazi hiyo pia Mamlaka za kimataifa kama ISO-1900 , kama TM ziko Gold smith na zingine nyingi tu.

    3.Uwajibikaji na Usimamizi, limekuwa ni Zimwi ambalo ndani yake ndio kuna Ufisadi na mabalaa mengine kibao tu.

    4.Kama Kamati za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,hasa kamati ya kuhakiki Mahesabu ya Umma zinashirikisha Wah. Wabunge wa Vyama vyote nchini huku Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali akiwepo, Sioni sababu kwa nini tusiwe na Mawaziri Mseto ili kuleta Ufanisi zaidi kwa Uwazi na kuiweka Mamlaka ktk hali ya salama zaidi kuliko kuubeba Msafara wa Mamba wakati ndani yake wamo Kenge ('Kenge-Mafisadi') ?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...