Video ya Neema.
Pichani mtoto Neema George aliyegundulika kuwa na matundu matatu kwenye moyo. 
Mtoto Neema George (16) amewaomba wasamaria wema wajitokeze kumchangia fedha ili akapate matibabu ya moyo nchini India.
Miguu ya Neema
Hali ya Neema George inazidi kuzorota siku baada ya siku, miguu ikiwa imevimba, akitaabika katika suala la kula, kuongea na akipata maumivu makali ya tumbo hasa nyakati za usiku.
Baba mzazi wa Neema, George Mugunga (kushoto) anasema kuwa mnamo mwaka 2010 mara baada ya hali ya mtoto wake kuzorota alimfikisha katika hospitali ya Rufaa Bugando kwaajili ya matibabu, lakini mara baada ya vipimo kufanyika vikaonyesha kuwa moyo wa mtoto wake una matundu matatu.
Baadhi ya vithibitisho vya tiba.
Madaktari kupitia kliniki aliyokuwa akipata huduma (Bugando) wamesema kuwa tatizo la neema ni kubwa na haliwezi kupatiwa ufumbuzi hapa nchini bali linaweza kupata tiba Nchini India kwa makadirio ya gharama ya shilingi za kitanzania milioni 25.
Picha za ukutani wakati wa ubatizo wa Neema, katika kipindi hicho ingawa hali yake ilikuwa dhoofu lakini suala la kuvimba tumbo na miguu halikuwepo.
Mbali na kumtegemea mungu kwa kila azungumzalo mtoto huyu anaonekana anaakili sana na mwenye uchangamfu wa ndani tatizo linabaki kuwa anaumwa.
Neema akiwa na mwandishi wa habari hizi Albert G. Sengo aliyefika nyumbani kwa bibi wa mtoto huyu eneo la Butimba mkoani Mwanza kwaajili ya kuchukuwa taarifa zaidi.
Kutokana na kiwango kilichotamkwa kuwa kinahitajika kwa ajili ya tiba nje ya nchi, familia ya mtoto huyu ilikata tamaa  kabisa na kukata shauri la kumpeleka Sengerema kijijini ili akatibiwe na waganga wa kienyeji ndipo bwana Azizi Bukene (ambaye ni jirani yao) akashauri kuita vyombo vya habari kwaajili ya kulifikisha kwa umma kwa msaada.
Nje ya nyumba.
Video
Familia ya mtoto huyu inategemea kilimo kama sehemu ya kipato cha kuendesha maisha ya kila siku, hivyo uwezo wa kufikisha kiwango hicho cha fedha hata kupata matibabu kwa manufaa ya mtoto huyo kuendelee na masomo ni ndoto za alinacha.

Video
Baba wa mtoto huyo aitwaye George Lenatus Mugunga amewaomba wasamaria wema, makampuni, wanasiasa, viongozi wa dini, wafanyabiashara na watu binafsi walioguswa na tatizo la mtoto Neema, kuwasiliana naye kupitia namba za simu ya kiganjani 0755424086 au kufika Ofisi za mkuu wa mkoa wa Mwanza ili kupata utaratibu wa kufikisha msaada huo haraka iwezekanavyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2012

    nashauri kuwekwa na account za benk, mp-pesa, tigo-pesa ili wenye kuwa na kidogo wawasilishe kwa njia hiyo.

    pole sana Neema Mungu atakujalia utapona

    asante

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 31, 2012

    Mimi sielewi kabisa mbona kuna viongozi au ndugu wa viongozi wanapelekwa kutibiwa nje kila leo? Haikai akilini kwangu mtoto kama huyu hali yake siyo nzuri anaomba omba pesa kupata matibabu?? Bado kuna tatizo kubwa wizara ya Afya. Nenda na mbunge huko wizarani, mtapata nafasi ya kwenda nje kutibiwa. Degelavita.

    ReplyDelete
  3. Wekeni namba ya account ya benki ili iwe rahisi kwa wale ambao tuko mbali

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...