Wanafunzi wa shule ya msingi Kising'a Isimani wilaya ya Iringa vijijini wakiwa wamebeba ndoo za maji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mwalimu jana majira ya saa 9.45 asubuhi muda ambao walipaswa kuwepo darasani kama walivyokutwa na mpiga picha wetu.

Na Blog ya Francis Godwin

TABIA ya uongozi wa shule ya msingi Kising'a Isimani wilaya ya Iringa kuwatumikisha kazi wanafunzi asubuhi wakati wa vipindi vya masomo imepingwa vikali na baadhi ya wazazi wanaosomesha watoto wao katika shule hiyo na kuiomba wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi kuingilia kati suala hilo.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi leo kijijini hapo wazazi hao walisema kuwa uongozi wa shule hiyo ya msingi Kising'a kila siku kabla ya watoto kuingia madarasani wamekuwa wakiwatuma katika kazi mbali mbali ikiwemo ya kuchota maji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mwalimu.

Alisema Jonh Kalinga kuwa tayari wamepata kuulalamikia uongozi wa shule hiyo na kuukanya kacha kuwatumikisha watoto hao majira ya masomo ila bado vitendo hivyo vya wanafunzi kukatishwa vipindi na kwenda kufanya kazi za walimu vimekuwa vikiendelea.

Kwani alisema tayari wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ilipata kupiga marufuku watoto kufanya kazi wakati wa vipindi vya masomo ila bado uongozi wa shule hiyo umeendelea kuwatumikisha watoto kazi .


Hivyo alitaka wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi kufika katika shule hiyo ili kujua sababu ya walimu kuacha kuwafundisha watoto hao na badala yake kuwatumikisha katika kazi hizo.


Aidha wazazi hao walisema kuwa kila wakati wamekuwa wakichangia michango mbali mbali kwa ajili ya maendeleo ya shule hiyo ikiwemo michango ya ujenzi wa nyumba za walimu ila wanashangazwa kuona watoto wao hawasome na badala yake wanatumikishwa kufanya kazi ambazo zilipaswa kufanywa na wazazi.

Wanafunzi hao waliokutwa wakiwa wamebeba ndoo za maji walimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa katika shule hiyo kuna ujenzi wa nyumba ya mwalimu unaendelea na kuwa kila siku kabla ya kuingia madarasani wamekuwa wakitumwa kwenda kutafuta maji umbali wa nusu kilomita kutoka shuleni hapo ndipo waweze kuingia madarasani muda wa saa 4 asubuhi .

Mwandishi wa habari hizi alipomtafuta mkuu wa shule hiyo kwa ajili ya kujua sababu ya kuwatumikisha watoto hao kazi mbali mbali za mikono kabla ya kuingia madarasani ,mkuu huyo hakuweza kupatikana huku mwalimu mkuu msaidizi na mwalimu wa zamu katika shule hiyo wakiikimbia ofisi na kumwacha mwandishi wa habari hizi peke yake ofisini.

Kwa upande wake afisa elimu wa shule za msingi katika wilaya ya Iringa vijijini hakuweza kupatikana ili kulitolea ufafanuzi zaidi suala hilo baada ya kuwepo katika kikao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2012

    WATOTO WANAFANYISHWA KAZI MIKOA MINGINE PIA. SHULE MOJA ARUSHA WATOTO WA FORM ONE WANAPASUA KUNI. HAKUNA CHA INSURANCE WALA HUDUMA WANAPOUMIA. HILI LIANGALIWE WAZAZI TUMECHOKA, TUNALIPIA CHAKULA CHA WATOTO SHULENI ILI WASOME SIO WAGEUZWE VIBARUA WA KAZI ZA HATARI NA NGUMU.

    MZAZI

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 01, 2012

    Hivi huu utaratibu wa kuwatumikisha watoto wanapokuwa shuleni huwa una lengo gani hasa? Mimi nilikua katika mzingira hayo na wala siioni faida yake zaidi ya kujisikia nilipoteza sana muda wa kusoma na kuwa mchovu muda mwingi.

    Na isitoshe baada ya shule ukirudi nyumbani nako ni shughuli hizo hizo, ikiwemo na wikiendi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 01, 2012

    Hii ni katika mambo ambayo waziri husika (katika spirit ya uwajibikaji, kama inavyotakiwa kwa wakati huu), anatakiwa alishughulikie jambo hili mara moja na kutoa taarifa ni lipi linafanyika kuzuia utumikishaji wanafunzi namna hii. Kwangu huu ni utumikishaji ambao hautakiwi kabisa kuwepo iwe saa za shule ama wakati mwingine wowote. Wanafunzi wanaweza kufanya na tena kwa makubaliano na wazazi wao na katika wakati ule ambao si wa shule shughuli zenye manufaa kwao wenyewe mfano usafi wa darasa, shule, kusaidia kujenga darasa la ziada nk.

    Nakumbuka miaka 30 iliyopita nilikuwa kati ya watoto tuliopitia utumikishaji wa aina hiyo. Nilikuwa, na sikuwa peke yangu tunatumwa kumuuzia mwalimu askirimu (icecream) zake wakati wa break na alikuwa akitupa hata 15 minutes baada ya break time kumalizia zile zilizobakia. Kwangu wakati ule nilifanya hivyo nadhani kwa kujenga tu mahusiano mazuri na mwalimu, lakini looking back nilitakiwa kusema "no, I can't".

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 01, 2012

    HALI HALISI YA KIJANA WA MIAKA 14. MTOTO ANAAMKA SAA KUMI NA MOJA ASUBUHI KUWAHI SHULENI. AKIFIKA AFANYISHWE MAKAZI MAGUMU (SIO KUMWAGILIA MAUA AU KUSAFISHA DARASA) KAZI HASA KAMA KIBARUA. IKIFIKA SAA MBILI ASUBUHI AANZE MASOMO MPAKA SAA KUMI. ANAKULA MLO MMOJA TU WA MCHANA UGALI MAHARAGE. BAADA YA SAA KUMI ANAINGIA TWISHENI HADI SAA KUMI NA MBILI. SAFARI YA KURUDI NYUMBANI SAA NZIMA (UKIONDOA KUSUKUMWA NA MAKONDA) AKIFIKA NYUMBANI HOI, ASAIDIE KAZI ZA NYUMBANI HADI SAA MBILI. ALE AOGE HOMEWORK HAJAFANYA. HALAFU TUNAULIZA KWA NINI WATOTO WANAFELI?? WANACHOSHWA. HATA MAJINIASI RATIBA HII HAWAIWEZI

    KWA UCHUNGU NAWASILISHA MZAZI

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 01, 2012

    Mara nyingi wadau wanapoongelea kuboresha elimu, ni suala la waalimu na madawati na mtaala wa kufundishia na vifaa, majengo n.k. wadau wakuu wa elimu, wanafunzi na wazazi huwa hawahusishwi kikamilifu. Wanafunzi wakipewa nafasi ya kujifunza na kuboresha elimu, wengi wao watasema kinachowakera zaidi ni mazingira ya hali zao, usafiri, chakula, kazi za nguvu na mijiviboko ya kila siku. Haya yote hayahitaji fedha za kigeni, yanawezekana. Ndugu zanguni hili ni moja wapo ya maswala ambayo yapo ndani ya uwezo wa shule husika kutatua nauliza ni kwanini wanafunzi wawachotee maji walimu? kwanini wazazi walipie chakula cha mchana halafu wanafunzi wajipikie wenyewe? Kwanini wanafunzi wachapwe unifomu zikiwa chafu wakati kazi wanazozifanya ndani ya uniform ni upasuaji wa kuni na usafishaji wa nyumba za walimu? Sheria ya haki ya mtoto iko wazi kabisa, Kwanini haifuatiliwi? Je wanafunzi wamekuwa 'watumishi wa bure ' kwa shule zao? tutafika kweli?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 01, 2012

    Hili ni tatizo la Tanzania nzima. Watoto wanatumikishwa mashuleni kama watumwa. Unasikia watoto wa vijijini wakipass kwenda form one kati ya vifaa vinavyo ni ndoo,jembe, panga na fyekeo. Hapo hapo waalimu wa kutosha hakuna hivyo watoto wanashinda kwenye kilimo na kuchota maji!

    Kama kweli serikali yetu ina uchungu na maendeleo ya nchi yetu inabidi ilipinge vikali swala hili. Hawa watoto ndio wanjenzi wa nchi yetu baadaye je kama hawapati elimu inayopaswa waitaijengaje nchi? Tutaishia kukandamizwa na wageni tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...