Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Dk.Emmanuel Nchimbi, akizungumza na Viongozi wa Jumuiya za Kiislam na Wadau wac Sekta ya Utalii Zanzibar, kuhusiana na fujo zilizotokea juzi Zanzibar, kulia Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Mwema na kushoto Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali. 
Waziri Dk. Nchimbi  akisisitiza jambo katika Mkutano wake na Viongozi wa Dini  kuzungumzia Vurugu zilizotokea juzi katika mitaa ya mji wa Zanzibar.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Mwema, akizungumza katika Mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar Kilimani.
Viongozi wa Jumuiya za Kiislam Zanzibar  wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Dk. Emmanuel Nchimbi, akizungumza nao kuhusiana na matukio yaliotokea katika Visiwa vya Zanzibar.  
Viongozi wa Jumuiya  za Sekta ya Utalii Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani, akizungumzia hali iliojitokeza juzi ya fujo katika mitaa ya Mji wa Zanzibar. na kulani hali hiyo.isitokee tena  ikaharibu  Amani ya Visiwa vya Zanzibar ambavyo vinasifika kwa Amani katika Afrika Mashariki.
Mwandishi wa habari wa Nipashe Mwinyi Sadala akiuliza swalim katika Mkutano huo.uliowashirikisha Viongozi wa Jumuiya za Dini na Wadau wa Sekta ya Utalii kuziungumzia vyurugu hizo..
Mwandishi wa Redio HIT FM, Jacob, alipota fursa ya kuuliza, katika Mkutano huo na Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Nchimbi.    
Ofisa wa Ubalozi wa Marekani aliopo Zanzibar Jefferson Smith, amelipongeza Jeshi la Polisi kwa jitihada zake za kurudisha hali ya Amani katika Mji wa Zanzibar bila ya kutokea madhara kwa Wananchi na kulipongeza kuwakutanisha Viongozi mbalimbali wa Jumuiya ya Dini na Wadau wa Sekta ya Utalii kuzungumza  nao, jinsi ya kuzuiya tatazo hili lisitokee tena.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya ZATO  Zanzibar Abulswamad, amesema yeye amefarijika kwa ujio wa Waziri wa Mambo ya Ndani na IGP,na amelitaka jeshi la Polisi kuzuiya fujo kama hizi zisitokea tena katika Visiwa vya Zanzibar ambavyo huzoretesha shughuli za Kitalii ikizingatiwa wakati huu ni msimu wa Utalii ikizingatiwa Zanzibar ni moja ya nchi zilizokuwa na Vivutio vya Utalii.  






SHEKH. Saleh Zam, akitowa shukrani kwa niaba ya Wanajumuiya za Kiislam Zanzibar baada ya kumalizika kwa Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Polisi Zanzibar. Picha na Othman  Mapara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 30, 2012

    Mbona hakuna wakristu kwenye kikao hicho, makanisa tuchomewe, and then atashikirikishiwi...hiyo ndio bongo.

    Mdau
    Maryland

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 30, 2012

    Dawa ni kuwapa Zanzibar yao. Mnasuluhisha nini wakati kinachotakiwa mnakijua.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 30, 2012

    hawa ni magaidi tu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 30, 2012

    Hawa Wazanzibar Hawaeleweki. Kwa nini wanachoma makanisa? Kwani makanisa yanahusika vipi na masuala ya Muungano? Huku ni kukosa uungwana.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 30, 2012

    WEWE inaonesha ni mmoja wa wale wasioelewa wala kufahamu,na watu kama wewe ndiyo mara nyingi MNACHOCHEA FUJO bila kujielewa kama mnachochoea.Umeshindwa kuelewa kuwa fujo hizo zilifanywa na BAADHI YA WAISLAMU WASIOELEWA MAFUNZO HALISI YA UISLAM na bado unajiuliza kwa nini katika kikao hicho hawakushirikishwa wakristo!!sasa kwa akili yako hao wakristo wakafanye nini katika kikao hicho?
    Jaribu kuelewa kuwa kutowaita wakristo hakuna maana yoyote ya ubaguzi.
    Ulichotakiwa kufanya ni kuunga mkono hizi jitihada za kukomesha fujo kama hizi zisitokee tena, na hapa nachukua nafasi hii kuwapongeza viongozi waliofikiria kuitisha mkutano kama huu ambao kwa njia moja utasaidia kwani hawa mashehe wakitoka hapa itawabidi katika hutuba zao wawafahamishe wafuasi wao UBAYA wa kufanya fujo kama hizi ambazo kiukweli zinatuharibia sana sisi waislam kwani wachache wenye misimamo mikali ndiyo kila mara wanatuharibia uislamu wetu hadi tunaonekana kama dini yetu inasapoti fujo wakati kwamba DINI YETU YA KIISLAMU HAIFUNDISHI MAOVU YANAYOFANYWA NA WACHACHE KWA MASLAHI YAO YA KIBINAFSI. Na kama wao kweli wanajifanya kuitetea dini mbona wamejificha wanaogopa kukamatwa na polisi?
    NAMUOMBA MUNGU ATUZIDISHIE AMANI WATANZANIA WAISLAMU NA WAKRISTO TUISHI KWA PAMOJA KIUPENDO NA TUSIFIKIE ILE HALI YA WAISLAMU WA NIGERIA (AMIN)

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 30, 2012

    Mdau wa Maryland, hoja yako ni sahihi, ila kumbuka kwamba , wakristu si wenye kuchochea fujo wala hutasikia kwamba wamechoma misikiti, sasa basi unapotaka kutibu gonjwa ,ni vyema kuutumia muda wako mwingi kuangalia pale palipooza na upatibu. Mashaka kasema,tatizo siyo gesi wala muungano ni DINI- wenzetu hawa wana itikadi kali, huko Yemen kunawaka moto kila baada ya mwezi, hebu niambie je ?? kuna mtalii anayekwenda yemen ??? sasa subiri kama Mungu atatupa maisha marefu ili tujionee mafuta yatakapokauka huko Uarabuni !!!! watachinjana kila siku. Zebedayo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousMay 30, 2012

      acha hizo ,mafuta yakikauka lini?unaota nn?

      Delete
  7. we are not the same....I CAN BE LIKE U YES U...I PROMISE. They wanna be handled like a silver spoon...come on..dis is 21 st century.
    Don't smile on my face while ur hatin coz I dont like unafiki.

    people forgive but they wont forget...keep that in mind

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 30, 2012

    Huyo mzungu aliyeuliza swali kwa kiswahili ni Mkristo kuliko kakobe...

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 30, 2012

    Wewe Anonymous wa kwanza,unasema viongozi wa kikristo hawajahusishwa!!,,kwani wao wahusishwe wamekosa nini?.hapo hawaitaji kuhusishwa kabsa,,kwani wao hawajui lolote kuhusu vurugu hizi,,wao wamevamiwa tu,,,
    Na nina uhakika hao wavamizi si wacha Mungu,maana katika Qur'an hawakufundishwa kitu kama hicho kuvamia mtu wa dini nyingine,..Wala Mtume Muhammad (S.A.W)hakuwahi kufanya hivyo,,
    Nchi ya Iran niya serikali ya kiislam,,na wana makanisa,na watu wanaenda kuabudu bila bughdha yoyote,,ila wanawake wanafaa kiheshima kabisa,,Hapa UK ni nchi ya Wakristo..lakini wanaruhusu Shule Misikiti,TV mavazi ya Kiislam,,na hata wakristo wanafanya katika TV na Ofisi za Kiislam kwa Amanikabisa,,Sasa Wazenj waliokuwa wachache wanakuwa kama rais wa Ufaransa aliyetolewa,,,Ni kwa kuwa mbaguzi wa rangi na Dini,,Mtu umche Mungu kivyako vyako,,kwani siku ya siku,,kila mtu ataubeba mzingo wake Mwenyewe,,Wala hutapewa Pepo eti kwa kuwa Ulichoma Kanisa au Msikiti!!
    Hiki kitendo walichofanya hawa watu kweli kilaaniwe,,,maana vita ikiamka hapo na wakrito wakarudisha majeshi yao,,Hutamuona wa kusalimika hapo,,Si Baba,Mama wala mtoto,kama sio kifo basi watakuwa walemavu wa viungo,vita haina macho,,,Amani kuivunja ni rahisi sana,,ila kuirudisha nikasheshe,,mpaka wote muwe muisha onja joto ya jiwe na kupoteza maisha na mali zenu na makazi,,,
    Na ikimbukwe kwamba,na hao Wakristo ni wazawa wa Zanzibar wala si wabara.Wakrito wa Bara hawanahaja ya kuhamia Zenj,labda Waislam wachache,,Ila Wapemba na Wazenj sijui waunguja,,ndo wamejaa Dar,Kariakoo,namanga.na wamejenga majumba mazuri sana huko msasani,,Tanga,,na mikoani pia,,Hao ndo wanafaidi Muungano,,na wanaopinga Muungano ni wale wazembe hawataki kujishughlisha,wakatoka kutafuta riziki.wanasubiri pesa wa Watalii!

    Allah Awapeni Imani na Subira!

    Ahlam ,,,London

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 30, 2012

    Wako wasioelewa mambo na hawataelewa kamwe mpaka element ya udini iwatoke. Masheikh wameshasema issue ya Zanzibar haihusiani na uislam. Lakini kuna watu mumeenda mbali kufananisha uislam na kinachoendelea Yemen. Je, Yemen kuna wakristo wangapi wameuwawa au makanisa mangapi yamechomwa moto? Acheni chuki za kidini. Tujaribu kuangalia namna ya kurekebisha na si kuchochea zaidi. Of course, Zanzibar kuna waislam wengi kuliko wakristo, sasa mukichochea munadhani nani ataumia?
    RAI: Tutibu kidonda, tusikiongeze kwa kaa la moto.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 30, 2012

    WEWE ZEBEDAYO,,KAMA UNAKAA UNAMUOMBA MUNGU MAFUTA YAKAUKE UARABUNI,USISHANGAE UKAKAUKA WEWE,,HIYO NI NE'EMA KAWAPA MWENYEZI MUNGU,,,

    KATIKA COMMENT HIZI KUHUSU VURUGU ZA ZANZIMABAR MAFUTA YA UARABUNI YANAINGILIA VIPI???WEWE BORA WATOLEE MFANO WA VURUGU ZA SYRIA,EGYPT,LIBYA..WANAVOUWANA KAMA WANYAMA BILA HURUMA,,NA WAZENJ WANAELEKEA HUKO HUKO,,,LAKINI WACHA KUWA NA HUSDAH ILIYOKUWA NJE YA UWEZO WAKO,,ETI MUNGU AKUPE UHAI USHUHUDIE MAFUTA KUKAUKA UARABUNI,,MUUUH MUUH HIYO ITAKUKOST ZEBEDAYO,,NA KUKUTIA MAWAZO MENGI MNO

    AHLAM ,,,LONDON

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 30, 2012

    Mie swali langu moja kwanini wachome kanisa sio msikiti huo muungano na makanisa wapi na wapi

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 30, 2012

    Ahlam....umeongea vizuri,ila umeharibu mwisho!

    Hao waZanzibari walioko huko Tanganyika, ni wachache tu miongoni mwa wengi.Then, hapa hatuzungumzii maslahi ya binafsi ya waZanzibari,ila tunazumgumzia maslahi ya Zanzibar, kama nchi au taifa!

    Wake up...sister!

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 30, 2012

    lets call a spade a spade and not a big spoon.
    Hivi kama sio issue ya kidini kwanini makanisa yachomwe?Makanisa yanahisika vipi na muungano? halafu hivi mahakaamni au kwenye usuluhisi anakuwepo nani?Mlalamikiwa na mlalamikaji. au mtenda na mtendewa. wakristu walitakiwa wawepo kwenye hiki kikao na wawasikie mashehe kwa masikio yao kuwa Uislamu hausemi hivi bali wanaofanya hivi hawaujui uislam na ni kikundi kidogo si waislamu wote.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 30, 2012

    LEO HII MKO KATIKA MUUNGANO MNACHOMENA MOTO MAJENGO NA KUPIGANA MAWE JE MKIJITENGA ITAKUWAJE ?

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 30, 2012

    We wa mwisho ndo bwege kweli. Sasa ndo umeongea nini..Tatizo watz hatujui VITA hasa za ndani ya jamii na ndio maana tunayafanya haya. yatatutokea puani..Kwanini iwe sehemu za kuabudu? Tatizo la dunia hii ni Siasa ambayo inatouch Dini kwa maslahi ya wanasiasa,raia tuwe makini ili tuwe na Amani.Rastafarian.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 30, 2012

    Wewe wa mwisho nawe umekosea pale uliposema ".... Of course, Zanzibar kuna waislam wengi kuliko wakristo, sasa mukichochea munadhani nani ataumia?
    RAI: Tutibu kidonda, tusikiongeze kwa kaa la moto."
    NINAKUHAKIKISHIA WOTE WATAUMIA, NA TAYARI MAUMIVU NAYAONA. DAWA NI KUTAFUTA AMANI KWA WOTE, BILA KUBAGUA.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 30, 2012

    Zanzibar, nchi ya wasioisha kulalama,watakao haki bila wajibu,asili ya utwana kama unabisha muulize Jamshid. Serikali ya umoja wa kitaifa imewanyima uwanja wa mtanange sasa wamehamia muungano. Makosa ni ya serikali kwani wakichoma mahoteli wanakenuliwa meno. Wakachoma maduka ya wanyamwezi wanaochakarika srkl bado na huku kuchoma makanisa siyo mara ya kwanza. Wao hupenda ugomvi daima na dawa yake ni utawala wa mkono wa chuma kama zile awamu tatu za mwanzo. Najua wanataka kuuza kisiwa hicho Oman ili wapewe tende.
    Ttz mwalijua ila uniq unawaziba macho.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 30, 2012

    UNAJUA UKITANGULIZA HISIA KALI HUWEZI KUWA NA FIKRA ZILIZO HURU: MI NAPINGANA NA WANAOSEMA KUWA WAISLAMU NDIO TU WAFANYAO FUJO KAMA IFUATAVYO: Kule Nigeria inasemekana wakristo ndio walioanza uchokozi kwa waislamu huku wakijipa matumaini kuwa raisi pamoja na baadhi ya viongozi wakuu kwa wakati huu ni wakristo na hivyo watapata utetezi kutoka ktk dola...waislamu walivyoona hawasikilizwi wakaamua kulipiza kisasi...Jambo la pili ni hivi majuzi tu wakristo wa dhehebu la EPHATHA pale mwenge walichoma kiwanda cha vitabu vya dini kinachomilikiwa na waislamu na kwa jeuri hata wakawa wanapambana na police huku wkionywa kwa njia ya kubembelezwa...Ukiangalia vizuri hata matukio ktk hizo nchi mlizozitaja za kiislamu matatizo mengi yanasababaishwa na mataifa ya magharibi ambayo ni maadui wa waislamu kazi yao ni kubuni kila siku mbinu mpya kuwagombanisha raia,...mifano ni mingi lakini kwa watu wanaofatia mambo na hawaongozwi nahisia wako huru,..utaona hata baadhi ya nchi nyingi tu zenye wakristo wengi ni mapigano tu kila siku,..naomba kuuliza kule congo ni nchi ya kiislamu?? kaskazini mwa uganda je kwa yule jamaa kony(gaidi) anapigania amri kumi za yesu,..liberia mumesahau,..ni juzi tu kuna gaidi kubwa kule Norway kama sikosei ameua watu wengi kwa silaha na hatujasikia vyombo vya habari vikishadadi ugaidi wake...kwa habari ni kwamba waliochoma makanisa ni wahuni tu ambao hawaelewi walitendalo na uamsho nia yao ilikua ni njema tu kama wafanyavyo TIC ya wakristo kuitisha makongamano ya waumini wao kuongelea mambo ya katiba na mengineyo...kuweni huru kufikiri ndugu zetu.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 30, 2012

    Tuwe wakweli jamani - tatizo la Unguja si dini, wala uislamu wa nini. tatizo ni UCHUMI umebada sana, Zanzibar kuna njaa sana kwa Wazanzibari wazawa, hawana kazi, maisha duni kila siku. Jiulize biashara zote kubwa kubwa, hoteli, nk zinamilikiwa na nani? Ni wazungu, hasa wataliano, wahindi, wakenya na wabara. Wazanzibar wanawaona raia wa nchi zingine wakija Unguja na kuchuma na kuchuma ili hali wamekaa tu wanaangalia. Ingia hoteli yoyote kubwa Zanzibar, fanya utafiti kidogo utagungua walio katika nafasi za juu za ajira ni wageni na wanzanzibari wengi wanaishia room service na waiters. Hiyo ya kuchoma makanisa, ni hasira tu ya kutafuta mchawi lakini issue ni UCHUMI

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 30, 2012

    wapeni nchi yao vikao mara mia vya nini ukweli wanataka nchi yao angalia hata kwenye picha kushoto yule polisi wana hana muda wakusikiliza mawazo yake yako mbali

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 30, 2012

    Jamani waislam wenzangu hata kama hamjui uislam kama wanavyodai wenzetu wengine,kwa nini kila siku ni sisi? mimi naanza kuwa na mashaka,kwani hakuna wakristo ambao hawajui miiko au matakwa ya ukristo?mbona hatusikii wanaoitwa wakristo kufanya fujo?hivi kwa nini tusiheshimu dini yetu? kusudi wale ambao sio waislamu wajiunge?kwa kweli tumezidi sana na kila siku ni wa kwanza kulalamika eti hatutendewi haki,kila muislam afikirie mambo haya,uislam imekuwa gumzo duniani,kwa nini tusijirekebishe?maana tunaonekana ni wanafiki,tunajiona ni watu wa Mungu lakini matendo yetu ya KISHETWANI.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 30, 2012

    Wazanzibari waelewe:

    Hali ya Uchumi ni tete (ngumu) Dunia nzima na sio uzembe wa Serikali ya Mapinduzi wala ya Muungano.

    Hii ni WORLD ECONOMIC AND FINANCIAL CRISIS matatizo ambayo si Ulaya, Marekani wala huyo wanayemtegemea Mwarabu na 'FALAKI' zake anaweza kuyatatua!

    Wazanzibari wamegawanyika, wapo pia wanaoutaka Muungano na hao wasioutaka, hivyo Mamlaka haiwezi kutekeleza kila matakwa ya watu wote kwa pamoja, impe nani imwache nani?

    Kwa maana hiyo ubora wa maisha au Uchumi Visiwani kuimarika kamwe hautatokana na wao kuvunja Muungano !!!!...inawezekana wakawa na njaa zaidi kama unavyoona hadi nyanya na vitunguu wanaagiza Bara je ukosefu wa hivyo viungo(nyanya na vitunguu) pia hilo ni tatizo linaletwa na Muungano???

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 30, 2012

    tunataka nchi yetu thats is it,mkisema wadini, hatukusoma tunataka nchi yetu wekeni kura ya maoni muone wangapi wanautaka huu muungano muone mbona natubana bana.

    sisi hatushindwi kuendeleza nchi yetu kama mnavyofikiri nyinyi wadanganyika si mnasema sisi ni mzigo baso tutuweni nasisi jujibebeshe wenyewe mzigo wetu mnanganania tu na kututesa bila ya sababu

    tulikuwa tukiishi vizuri sana na ndugu zetu wa kikiristo toka nzi na nzi kabla hajaja huyu baba wa kanisa kutunganisha, kaja yeye imekuwa balaa na kihoja juu ya kihoja katuchafulia ustaarabu wetu, amani yetu, uchumi wetu,serikali yetu na mila na tamaduni zetu na kikubwa dini yetu.

    eti leo tumekuwa mafukara na kutegemea utali na karafuu mnawazimu mnazani nchii hii ndo hivyo tu vya kutegemea.

    kichaka cha mungano ndo maakanisa yanatuletea uhanisi, usagaji,madawa ya kulevya na pombe ili vijana na wazee wetu waharibikiwe ndo maana hamtaki kuachia huu muungano, wakiristo wa zamani tuliokuwa tukishi nao walikuwa waastaarabu sana wazanzibari wenzetu wakiristo wa kibara wanatuletea balaa tupu wakuriya kutujia huku na kutuchafulia amani yetu.

    tumechoma makanisa siyo kwamba hatutaki wakiristo au tunachukia wakiristo ila hatutaki ufisadi huu wa uhanisi, usege, umalaya na ukithirishaji wa madawa ya kulevya

    tumeshaisoma historia yetu sana na tunajua nini tunatokitaka nacho ni NCHI YETU PERIOD NA KWA MUNGU HAKUNA KUBWA INSHALLAH ONE DAY TUTAIPAT NCHI YETU AMIN

    someni historia yenu waislamu wa tanganyika muijuwe msipotoshwe na hao waovu, mlimpeleka baba wa kanisa kuwa raisi kwa nia njema kabisa lakini yeye toka zamani alikuwa na nia mbaya na nyinyi ndo maana akakufanyiyeni aliyokufanyiyeni na hivi sasa sisi sote waislamu wa zanzibar na watanganyika tunaonekana wahuni, hatukusoma na walala hoi na wao wanaonekana ndo wenye maana

    lakini kwa mungu hakuna kubwa inshallah one day tutaipata nchi yetu na kurudisha heshma,mila, desturi, hulka na dini yetu ya kiislamu amin ya rabbi laalamin

    muombeyeni sana baba wa kanisa(nyerere) dua huko alipo kwa sababu kwenye uzima wa milele huko hakuna tena ujanja ujanja wake

    ITALY

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 01, 2012

    Bosi wa ITALY hapo juu:

    Anonymous wa Wed May 30, 11:20:00 PM 2012

    Pamoja na kusafiri kwako na kukaa kwako Italy bado mawazo yako ni mabovu kabisa.

    Ndio maana unaweza kusoma lakini ukawa hujaelimika kama wewe.

    Maneno na fikra hizo haikustahili utoe wewe uliyeelimika huko Majuu!, ingebaki ziwe kwa hawa watu waliofanya fujo Zanzibar wakati wakiutumia Uislamu vibaya.

    Huku ikieleweka wazi kabisa ya kuwa Dini Tukufu ya Kiislamu msingi wake Mkubwa ni Ubinaadam kwanza!!!

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 01, 2012

    Muheshimiwa wa ITALY

    Anonymous wa Wed May 30, 11:20:00 PM 2012

    Mtu anaweza kuelimika kwa njia nyingi tu zikiwemo hizi mbili (2) hapa chini.

    1.Kuelimika kwa Kusoma na akaitumia elimu badala ya kusoma kuvuka Vidato na Shahada bila kuelimika.

    2.Kuelimika kwa mazingira kama wewe ulivyokaa huko nje Italy na Wazungu.

    Inasikitisha sana kwa maoni yako inaonyesha kama hizo athari mbili hapo juu hazijakupata, ingawa upo huko Italy ki fikra unabaki kama hawa uliowaacha Zanzibar waliofanya fujo wakifanya kazi za uvuvi wa Tasi, Pweza na Ngisi !!!

    PAMOJA NA KUSAFIRI KWAKO KUWEPO ITALY KIMAWAZO UMEBAKI BWEGE MTOZENI!

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 02, 2012

    wadau wenzangu sawa kwa kunitusi ni haki yenu, i cant urgue with a fool kabisa.
    mnawaona wale walio nyumbani ni mabwege siyo duu poleni sana ukiwa majuu basi uwe different usijali nchi yako pelekeni ujinga wenu huko,mtajidai waataarabu mmeelimika kumbe vichwa maji

    tukipigania haki ya nchi yetu tunaonekana vinginevyo hata kama tuko majuu lazima tukufuateni nyinyi kama mkia ndo mlivyozoea,

    basi fahamuni nyinyi vicha maji kwamba popote alipo mzanzibar au muislamu wa kitanganyika anayeona uovu wa muungano na anaye itakia kheri visiwa hivi basi atasimaam kikamilifu kutetea nchi yake mpo wakuu vichwa maji

    kukaa huku Italy hakunifanyi mimi niwe tafauti na wenzangu eti kwa vile niko na wazungu MIMI SI MTUMWA BWANA WA WAKOLONI KAMA MLIVYO NYINYI

    NIMESHAAMKA LONG TIME TOKA HAMSINI KWEUSI WAULIZE WANAONIJUA MIMI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...