Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, akioneshwa eneo la ujenzi wa soko la kisasa katika Kijiji cha Mvomero, Kata ya Mvomero , kabla ya kuwahutubia wananchi wa Kata hiyo , Mei 16, mwaka huu.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ( mwenye Kaunda suti) ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, akiangalia hatua za ujenzi wa shule ya sekondari ya watoto wa wafugaji katika Kijiji cha Wafugaji cha Mela, Kata ya Melela, Wilayani humo Mei 18, mwaka huu alipofanya ziara ya kuangalia shughuli za maendeleo ambapo aliahidi kuwaunga mkono kwa kuwapatia misaada mbalimbali kwa ajili ya ujenzi.
Baadhi ya akina mama wa jamii ya wafugaji wa Kimasai wa Kijiji cha Mela, Kata ya Melela, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro, wakimwimbia nyimbo za kumkaribisha Mbunge wa Jimbo hilo, Amos Makalla ( hayupo pichani) ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo alipofanya ziara yake Mei 18, mwaka huu Kijijini hapo.
Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Nassor Seif ,Rehema Kapinga ( kushoto) akipokea seti moja ya Kompyuta yenye thamani za zaidi ya sh: milioni moja ukiwa ni msaada kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, wakati wa mkutano mkuu uliofanyika Mei 16, mwaka huu , eneo la Madizini katika Kata ya Mtibwa.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, akipewa zawadi ya kuku ‘jogoo’ kutoka kwa Mama wa Kimasai , Sarah Bakari alipofanya ziara kwenye Kijiji cha Wafugaji cha Mela, Kata ya Melela, Wilayani humo Mei 18, mwaka huu na kuaahidi kuwapatia misaada mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya watoto wa wafugaji .
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, akionesha kopi ya hundi y ash: milioni tano kwa wananchi wa Kata ya Kibati ,baada ya kuidhinisha kutoka mfuko wa Jimbo ili kuanza ujenzi wa soko la kisasa wakati alipokuwa akiwahutubia Mei 17, mwaka huu ikiwa ni mpango mkakati wa kuwainua wakulima wawezekuuza mazao kwa faida.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Mtibwa, wakiimba nyimbo za kumsifu MBunge wa Jimbo la Mvomero Amos Makalla, ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo baada ya kuwasili shuleni hapo Mei 17, mwaka huu kuwasalimu , Mbunge huyo ameisaidia vifaa mbalimbali Shule hiyo ikiwemo na safaruji na mabati wakati wa ujenzi wa vyumba vya madarasa .
Mwenyekiti wa Kwaya ya Vijana wa Mtibwa wa Kanisa la KKKT, Rick Lucas ( kulia) akimkabidhi zawadi ya mbuzi Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, ikiwa ni ishara ya kuonesha upendo kwake na kumpongeza kwa kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushika wadhifa wa Naibu Waziri wakati wa hafla fupi iliyofanyika Mei 17, mwaka huu eneo la Madizini.Picha na John Nditi,wa Globu ya Jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 19, 2012

    toka nimeaza kukusikia wewe muheshimiwa kma hautageuka mbeleni basi utakuwa kiongonzi bora na mwenye mfano wa kuigwa na nahamini utafika mbali zaidi ya apo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...