Chief editor,
 
Kuna watu matapeli wanataka kutumia issue ya watu kutokuwa na kazi kujinufaisha..nakuambatanishia hii email ya huyu dada(anasema yuko Nicaragua)..alitoa tangazo blog yako akisema kuna internship opportunities huko Nicaragua-Central America so watu watume CV zao.

Mimi nilituma(kujaribu though I have a job) na kuwaambia wenzangu..It was last week thursday,leo ndo katuma haya majibu (hapo chini).Cha kushangaza email ni the same kwa wote waliotuma CV zao..na post ni ile ile!!na worse hicho kipengele cha kutuma pesa ya Visa kwenye akaunt ya mtu!!!Naomba uipublish kwenye blog yako ili kuwatahadarisha watu wasije kuingia mkenge na pia kumwonyesha huyu muhusika kwamba watu si wajinga hivyo!!
Ahsante
Mdau Wako

-------------------------------------------------------------------------------------------------

Habari,

Ninayofuraha kukufahamisha kuwa ombi lako la kufanya kazi na Mercycorps Nicaragua(Central America) limekubaliwa,nimeambatanisha barua ya kukubaliwa ambayo utasaini panapohusika na kuirudisha kwetu.
Kwa mujibu wa sheria za immigration hapa Nicaragua,NGO inatakiwa kukuombea Visa/work permit ili uweze kuja hapa kuanza kazi,kwa sasa hakuna ubalozi wa Nicaragua hapo Tanzania.
Kama ambavyo nilikutaarifu hapo awali unatakiwa kutuma malipo kwa ajili ya kuprocess Visa/Work permit yako mapema kama ambavyo barua ya kukubaliwa kazi inavyojieleza ili kutoa muda mzuri kwa NGO kuprocess kwa wakati ambapo itachukua siku 4 za kazi kupata kibali hicho cha Visa/Work permit.
Sasa katika kurahisisha utumaji wa malipo hayo Management imeomba kutumia account ya mfanyakazi ambaye yeye ana account ambayo ni International Account ambayo benki yake pia inapatikana hapo nchini Tanzania,hii ni kwa sababu ya kurahisisha na kuondoa gharama za utumaji na ucheleweshaji wa kupata malipo kwa wakati.
Kwa hiyo unachotakiwa kufanya ni kubadili hiyo dola $197 kuwa Tanzania shillings ambayo ni sawa na  Tsh.315,200/- ,harafu utadeposit hiyo Tsh.315,200/- kwenye account ifuatayo;
Tafadhali nakuomba uscan na unitumie payslip/Deposit slip baada ya kufanya malipo kwa Sababu Management itaihitaji kwa sababu za kiofisi,

Bank Name: Stanbic Bank
Account Name: Jacob E.E
Account Number: 0140518946701
Visa Card Number: 4313321007132065

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 26, 2012

    Sasa wadau mbona huyu mtu kupata ukweli wake ni rahisi. Cha msingi taarifa hizi zipelekwe polisi na uchunguzi uanze mara moja. Ahojiwe mwenye hiyo akaunti. Watu wa usalama wanajua kulishughulikia kirahisi hilo suala.Nchi nyingi wizi huu upo na wanakamatwaga kiurahisi baada ya muda fulani. Tunaomba tuwekewe kwenye blogu hii kujua yatakyojiri

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 26, 2012

    asante mdau, na mimi nilituma..dada yetu upo?..hebu jitetee humu ndani ya blog ya jamii tuone kama hayo yaliyosemwa hapo ni uongo..pia tuwatume watu tunaowafahamu huku uliko ili waone kama kweli mna ofisi au kazi kama hizo hapo au ni utapeli tu wa kipuuzi?..yaani wapopo sasa wamegeuza kibao kwa staili hii..lakini watakaoliwa ni wajinga bwana.sio wajanja..hapa bongo watu watu ni wajanja kuzidi unavyofikiria dada.pole na kwa heri.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 26, 2012

    Asante mdau, huu unaonekana ni wizi wa mchana. Kwanza Tangazo lilikuwa la internship majibu ni ya kazi vipi hapa? Polisi wakifuatilia watampata huyu mhusika kwani bank details alizotuma zitakuwa ni unique kwa account hiyo iliyoonyeshwa. Ninafahamu kuna Bank duty of secrecy lakini kama Stanbic wakifahamishwa huyu ni tapeli wanaweza kudislose full details halafu jamaa ashikwe shati kaptura.
    Natumai umeokoa wengi walio kuwa wanategemea ku apply.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 26, 2012

    Hahahah,huyu sio demu ni msela flani hivi.Hahaha jamaa kweli kaishiwa yani utapeli wakitoto namna hii eti ''Kampuni imeamua kutumia accout ya mfanyakazi..'':Hahahahah hata km nikweli basi hio kampuni yenu ni bure abisa na ww unaetaka kuwatapeli watu kwa mtaji huu ww ni kilaza sana bcoz hujui namna yakuchombeza watu sidhani hata km unademu ww.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 26, 2012

    RB inatakiwa iandikwe haraka ya kumsaka JACOB E.E ndio Mtuhumiwa No.1 ili amtaje anayedai dada wa Nicaragua.

    Jamaa hayuko huko Nicaragua wala nini, jamaa atakuwa yupo hapa hapa Bongo ni maisha yamempiga na sasa anataka avute chache za nduguze ili ajisogeze kimaisha!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 26, 2012

    Kwa Bongo ilivyo unaweza kuta hao Stanbic hawana information za ukweli za huyo Jacob. Lazima kutakuwa na feki information, picha ya babu yake, jina la mjomba wake aliyekufa miaka 6 iliyopita..!!! KYC hakuna kabisa ni ubabaishaji tu..!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 26, 2012

    daaaaaaaaaaaaaaah yan bora mmenifungua macho, mana jioni hii nimepokea email yake ya kuniambia nimechaguliwa ktk nafasi ya adminstrator. yaani nilikuwa nishawapanga watu wa kuwakopa hiyo pesa ya visa na work permint. MUNGU NI MWEMA

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 27, 2012

    hi hihi ni hii kali sasa company inataka utumie jina la mfanyakazi wake saa yeye mwenyewe alianza kazi lini hapo? halafu upuuzi kabisaa ni pale aliposema ubadilishe hela iwe ya kibongo kutoka hela ya US,HUU NDIO TIRO kwa sababu exchange rate kila ukibadilisha unaliwa wewe. na huyu haupo Nicaragua wala niko Haragwe.

    ReplyDelete
  9. nashukuru Uncle michuzi kwa kuipublish hii kitu mana nilijua wadogo zangu wengi hasa young graduates wangeingia mkenge.Uchunguz wetu usio rasmi benki ya stanbic ni Kwamba huyu jamaa Jacob ezekiel ni mkazi wa sinza na hadi namba yake tulipewa na one of our source from the bank..ajirekebishe kabla hatujamlipua

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 27, 2012

    huyo atakuwa mnaijeria tu. Wapo kibao sinja kijiweni na tabata kule

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 27, 2012

    kwa maelezo yaliyotangulia uchungu huu ni wa wote pamoja na mabloger wetu.ni dhahiri mwajua jinsi ajira zilivyo za shida na mfumo wa elimu unavyowaandaa watoto wetu kuajiriwa.bwana huyu 2011 alitoa tangazo hili jiachie nikasihi akitokea tena wampotezee,nashangaa kaibuka tena na mnalitoa ili hali mwajua wazazi tutajikamua kuwalipia watoto kwa tamaa ya kuendelea kawhudumia wakiajiriwa.lakini pia vyombo husika mwafanyaje?mbona details zipo za kutosha kumshughulikia na ujambazi wa mtandao?fanyeni kazi tunayowalipa nayo ili sote tulijenge taifa letu kwa uadilifu.au mnaletewa kidogodogo akitumiwa?tupeni imani na tulivyowakabidhi dhamana ya utanzania
    ni mimi niliyejeruhwa

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 27, 2012

    Huyu Jocob E E aliwahi kutapeli watu waliokuwa wanatafuta vyuo mwaka 2011 kupitia post yake hapa Michuzi. Wengi walilizwa na alikuwa akitumia namba hiyo hiyo ya account. Alitumia pia mtandao wa Jamii Forum kutangaza utapeli wake kama hivi:

    http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-elimu-education-forum/180004-scholarships-for-tanzanians-2.html

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 27, 2012

    Huu utapeli ubwege?

    Njaa zingine jamani khaaa balaa.

    Mji ukiwa mgumu ni bora kuelekea Kaliuwa Tabora kukata mkaa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...